Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
MKAZI wa Kijiji cha Mwenge, Kata ya Mtina wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, Neema Athumani (24), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake kwa kumwekea sumu ya panya kwenye soda.
Taarifa za tukio hilo zinadai kuwa mwanamke huyo alitekeleza mauaji hayo Desemba 24, mwaka huu, baada ya kuweka sumu ya panya kwenye soda na kumnywesha mtoto wake Rashfod Tariq, mwenye umri wa miaka minne.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kutekeleza unyama huo, alichimba shimo na kwenda kumzika na baadaye kutoroka kijijini hapo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo mtuhumiwa alikamatwa akiwa safarini kuelekea mkoani Arusha alikodai kuwa alikuwa anaenda kwa ajili ya kufanyakazi za dani kutokana na ugumu wa maisha, baada ya mzazi mwenzake kumtelekeza na kukataa kumhudumia mtoto.
Akiwa chini ya ulinzi wa polisi, mtuhumiwa huyo alikiri kufanya tukio hilo baada ya kupewa masharti na mwajiri wake wa mkoani Arusha kuwa kama anahitaji kazi aende bila mtoto.
Nipashe