Tukio hili la kusikitisha la Hanang linanikumbusha maporomoko kama haya yaliyotokea Uganda miaka kadhaa iliyopita , watu walizikwa na udongo , huku vifaa vya uokozi vikiwa Machepeo na Sululu , kiukweli baada ya jambo lile niliona aibu sana kuzaliwa Africa , na hasa Africa Mashariki , nilijiona kama binadamu aliyeadhibiwa mno kwa kuzaliwa kwenye ukanda duni .
Sasa yanayotokea huko Hanang , achilia mbali kutia aibu lakini yanaonyesha kwamba Nchi ya Tanzania imewekeza zaidi kwenye kuumiza Raia wake badala ya kuokoa , ndio maana karibu kila kituo cha polisi kina gari la washawasha lakini Mikoa haina vifaa vya uokozi
View attachment 2834219
Shukrani kubwa kwa Wanajeshi waliofanya kazi kubwa kwa vifaa duni mno !
View attachment 2834214
NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO