Tungekuwa na Raisi kama Rutto tungekuwa mbali sana!

Tungekuwa na Raisi kama Rutto tungekuwa mbali sana!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Ukiona huyu jamaa anavyopigania pesa za uwekezaji Maraisi wengine wamebaki kupingana na demokrasia na kuajiri machawa . Kapigania mradi wa Dangote kwa udi na uvumba, kapigania pesa ya afya ya marekani zaidi ya $1.5 B, kituo cha afya zaidi ya $600M . Pesa zote hizi sio za walipa kodi. Sisi tumeishiwa kiasi cha kuuza dhahabu. Sisi tunapigana wenyewe kwa wenyewe kwasababu ya chaguzi za haki yaani tunapigana kwasababu chama kimoja hakitaki wananchi wachague wawakilishi wao kwa uhuru!. Mapigano yameenda mbali hadi ndani ya chama ambacho kimeiba kura kuingia madarakani dah!

New york wiki hii Rutto anafanya mikutano ya wekezaji sisi tuna Makamu anauza sura na kula bata New York. Yaani hata Watanzania wa diaspora hawana hamu ya kuongea na wezi wa kura na wala rushwa.

Wakati wenzetu wanapingana kwa hoja huku kiongozi wa upinzani anataka kunyongwa kwa kupigania haki ya watanzania kuchagua wawakilishi wao kwa uhuru.

Katiba mpya ambayo ingenufaisha nchi hawaitaki maana itapunguza nguvu zao za wizi na kuweka ndugu zao kwenye madaraka. Tuondelee kupigana Mungu yupo nasi
 
Ruto ,elimu anayo kichwani , achana na wale wa elimu mbalimbali
 
kimuangalia tu Rutto na mapungufu yake kukuki! Bado kichwani ana kitu. Ukija kwa yule mwenzangu na mimi wa nchi ya kusadikika, ni majanga matupu.
 
Back
Top Bottom