Tungekuwa wapi leo bila Rais Samia?

Amejitahidi.
Ana mapungufu yake.
Lakini ukinikumbusha yule Israel mla vichwa, Sina hamu!
Mleta mada hujakosea
 
Ni kweli kabisa Magufuli ndio kaharibu sana Bunge imefikia hatua Spika Ndugai akajiuzulu kipindi akiwa madarakani.
Unataka kumaanisha nini hapa? Kwamba hili nalo tuanze kubishana? Unamaanisha kuwa hujui udhaifu wa bunge ulianza lini na haya ya sasa ni matokeo tu? Enzi hizo CAG anakosoa udhaifu wa bunge mnamuita kamati ya maadili! Tunaposema kuharibu sana bunge unaelewa maana yake kwa upana?

Wewe na huyo Ndugai nyote ni wapuuzi tu kwa sababu mnayoyalalamikia msingi wake mlikuwa mkiushangilia sana.
 
Ila JPM ameshambuliwa sana sijawahi kuona marehemu anachukiwa vile
 
Kwenye bei ungefanya muujiza gani bei zisipande?
 
Sina cha kuongeza

R.I.P JPM
Ila udhaifu wa muhimili(BUNGE) haukuanza Leo wala Jana.

Nakumbuka 1993 kutokana na presha ya G55 chini ya Njelu Kasaka na Alipipi Kasyupa Bunge chini ya Spika Pius Msekwa lilipitisha Azimio la kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika.

Lakini nini kilifuata?

Marehemu Kolimba na John Malechela wanafahamu vizuri.
 
Waachie kivipi? Kwani lini mfumko ulikua chini

Soma niliyekua namjibu aliuliza kitu gani kwanza mkuu.

Umefuatilia ongezeko la bei za vitu kwa kipindi cha miezi minne iliyopita?
 
Uongozi unakufaa mkuu, tena kitengo cha msemaji mkuu wa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…