Tunisia: Mtu mmoja ahukumiwa kifo kwa kuchapisha maneno ya kumkosoa rais Facebook

Tunisia: Mtu mmoja ahukumiwa kifo kwa kuchapisha maneno ya kumkosoa rais Facebook

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Raia mmoja wa Tunisia, Saber Chouchane (56), amehukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la kuchapisha kwenye mtandao wa Facebook, maneno yanayodaiwa kumkashifu Rais Kais Saied na kudhalilisha vyombo vya usalama.

Hukumu hiyo ilitolewa jana Oktoba 3, 2025 na imekuwa gumzo nchini humo.

Mawakili wa Chouchane wamesema mtuhumiwa huyo ni mfanyakazi kibarua mwenye elimu ndogo, aliyekuwa akitoa maoni yake binafsi kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kukamatwa mwaka jana.

"Hakimu wa Mahakama ya Nabeul, amemhukumu kifo kwa maneno aliyoyachapisha Facebook. Ni hukumu ya kushangaza na ambayo haijawahi kutokea," amesema wakili wake, Oussama Bouthalja.

Hata hivyo, wakili huyo amebainisha kuwa tayari wamewasilisha rufaa kupinga uamuzi huo. Wizara ya Haki ya Tunisia haijatoa maelezo yoyote kufuatia hukumu hiyo.

"Hatuelewi kinachoendelea. Sisi ni familia masikini, na sasa tumepata maumivu ya kunyimwa haki juu ya umaskini wetu," amesema mtuhumiwa, Jamal Chouchane.
 
Back
Top Bottom