Tupac aliwaza mbali sana kuhusu suala la kuleta watoto duniani

Tupac aliwaza mbali sana kuhusu suala la kuleta watoto duniani

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2018
Posts
1,821
Reaction score
3,980
Aliwahi kuulizwa " Kwanini huna mtoto Hadi sasa hivi?" Akajibu " Siwezi kuleta binadamu aje kuishi kwenye duniani hii yenye kutawaliwa na waovu na kila aina ya uovu. Kwa kufanya hivyo nitakuwa nimewatendea watoto wangu uovu mkubwa sana.. "

Ukiyatafakari maneno ya Tupac ni kama alikuwa na hoja... Sasa hivi pia kuna movement ya watu wanao kampeni Rhodi ya kuzaa watoto.. Wanasema " Hakuna binadamu muovu kama yule anae leta mtoto duniani. Kwa sababu unajua kabisa dunia ni ovu na inatawaliwa na waovu na matendo mengi maovu lakini bado unadiriki kuleta watoto duniani. Unafanya hivyo ili iweje?

Unajua duniani kuna magonjwa, kuna kifo etc lakini bado unaleta watoto. Wewe uta kuwa ni muovu na mbinafsi sana" Watu Hao wanaendesha kampeni ya kuwashawishi watu waache kuzaa ili kuwaepusha watoto wao na uovu wa dunia, na kauli mbiu Yao ni " I LOVE MY CHILDREN SO MUCH TO BRING THEM TO THIS EVIL WORLD ".

Ukitazama kwa makini utagundua kuna chembechembe za ukweli ndani yake, hata kwa upande mwingine watu wasio na watoto ndio wanaishi kwa Uhuru na furaha zaidi kuliko watu wasio na watoto. Wema Sepetu anaweza kuwa na furaha zaidi kuliko wewe mwenye watoto. Ikitokea habari " Mtoto kalawitiwa" ni wewe mwenye watoto ndio unakuwa desperately ku coment * Mungu nilindie kizazi changu".


There is something which is not right about the life in this world. Dunia haikuwa tayari kupokea watu ama Sisi ndio hatukua tayari kuishi kwenye safari. Yawezekana tupo hapa duniani kimakosa..
 
Tumeshaongea sana humu kuhusu Hilo , Kuna ukweli mkubwa sana kuhusu bandiko lako

Tatizo ni ile mentality tuliyo mezeshwa na Jamii zetu kwamba binaadamu anapaswa kuzaa lakini in reality Dunia sio sehemu salama Kwa binaadamu
Inatakiwa tufanye mgomo wa kuleta watoto duniani mpaka alie tuleta duniani aje kurekebisha mfumo aondoe watu wapvu la sivyo dunia ikose watu cause haina maana iendelee kuwepo na uovu mkubwa kiasi hiki
 
Inatakiwa tufanye mgomo wa kuleta watoto duniani mpaka alie tuleta duniani aje kurekebisha mfumo aondoe watu wapvu la sivyo dunia ikose watu cause haina maana iendelee kuwepo na uovu mkubwa kiasi hiki
Ni ngumu sana kuhusu Hilo

Do you think Mabepari watakubali wakati wao wanataka watu wazaliane ili wawatumie kwenye project zao
 
kwamba watu wakizaliana wanaendeleza uovu?
ndio akili zako zimeishia hapo?
Kwanini ulete mtu duniani ambae mwisho wake itakuwa ni kufa na siku ya msiba wake watahuzunika watu wengi sana? Hujioni kuwa wewe ni muovu na mbinafsi? Usiejali hisia za watu watakao Lia kwenye msiba wa mtoto wako? Au hujasikia methali isemayo " Mtaka nyingi nasaba hupata mingi msiba"?


Anyways hilo swali Lako ligeuze upande. Ukileta watoto duniani unawaleta kwenye dunia ya waovo so unawaweka kwenye risk ya kuwa victims ya uovu na waovu.
 
Ni ngumu sana kuhusu Hilo

Do you think Mabepari watakubali wakati wao wanataka watu wazaliane ili wawatumie kwenye project zao
Ikitengenezwa kama idea inawezekana... Pia kwa kusoma, sayansi inasema kuna uhusiano mkubwa sana Kati ya mzunguko wa mwezi na wana wake kutunga Mimba, mwezi ukiwa push away from its axis, itaathiri uwezo wa wana wake kupata Mimba. Kama tungekuwa na teknolojia hiyo ingewezakana. Meanwhile tunaweza kutumia dawa na vyakula na vipo vingi tu
 
Kila mtu achague anachoweza lakini nature imeshaweka limit ya kila kitu!.

Sidhani kama tunatakiwa tuache kuzaa ila inatakiwa tupambanie dunia iwe ni sehemu salama kwa viumbe!, so kama tutashindwa kuifanya dunia kuwa sehemu salama basi hio itakuwa ni aibu kwetu wenyewe!.
 
Ikitengenezwa kama idea inawezekana... Pia kwa kusoma, sayansi inasema kuna uhusiano mkubwa sana Kati ya mzunguko wa mwezi na wana wake kutunga Mimba, mwezi ukiwa push away from its axis, itaathiri uwezo wa wana wake kupata Mimba. Kama tungekuwa na teknolojia hiyo ingewezakana. Meanwhile tunaweza kutumia dawa na vyakula na vipo vingi tu
Sijui umenielewa my point is uwepo wa binaadamu ni Benefits Kwa watawala wafanya-biashara and the likes ili waweze kuendelea kutajirika na vizazi vyao viendelee kubaki kuwa kwenye chain ya utawala + utajiri wana hitaji watu

Watu ndio mtaji wa kwanza katika maisha ya opportunities, watauza madawa watakusanya Kodi , watauza mbolea watauza Mavazi watauza silaha watauza vyakula watauza Vyombo vya usafiri etc

So endapo binaadamu tukiwa hatuzaliani Tena it means next 300 yrs to come binaadamu hawato exist Tena duniani

So do you think Hilo kundi la watu tajwa linalo tawala watu katika nyanja mbali mbali litakubali binaadamu watoweke halafu wao wata tajirika vipi !? Kodi watapata wapi !? Bidhaa zao wata muuzia nani Tena !?
 
Back
Top Bottom