Tupac na Biggie wanakuzwa mno

Mkuu chukulia migos au Travis Scott au cardi b au Chance the rapper wakafa leo si mtasema kwa muda mfupi wame achieve makubwa. Point yangu ni kwamba isinge kua kifo leo hawa jamaa wangekua kati legends kama kina dre, snoop na ice cube.
Jiulize kwa nn muziki wa hiphop uko hoi sasa hivi siyo kama kipindi cha nyuma,sababu ni marapa wa kubwa wa sasa wameshindwa kufikia na kupita levels za kina big na PAC so hakuna jipya
 
"You claimed to be a PLAYER but I f*c*d your wife!"
 
Hivi ni kweli 2pac hakuwa mkorofi ni wao ndio walikuwa wanamuanza.
Inasemekana jamaa ilikuwa ukilianzisha basi analimaliza.
 
Hivi ni kweli 2pac hakuwa mkorofi ni wao ndio walikuwa wanamuanza.
Inasemekana jamaa ilikuwa ukilianzisha basi analimaliza.
Ukisikiliza interviews zake, utanoti kitu, jamaa alikuwa mtu fulani mweye akili timamu na kujielewa, hakuwa mwendawazimu kama wengine wanavyomtafsiri, japo hakuna mkamilifu alikuwa na mapungufu yake kama wanadamu wengine sisi tulivyo.

Bifu zake nyingi nizijuazp mimi ni wao ndio walianza kumzingua jamaa.
 
Yaani watu wanaongelea heavy weights wa hiphop afu mtu anakuja kutaja sijui Migos.
 
BIG nadhani kweli, yeye kama yeye hakuwa vile, ila alikuwa na team ya vijana wenye flows nzuri,

Ila Pac was more than a Rapper, alikuwa ni mwanaharakti , Thinker na Futurist pia.
 
Hakuna kama Makaveli the Don mazeeee! Nyimbo zake aliwakilisha sana society aliyokulia utaskia akilia na homicide, issue ya Single mothers kama alivyo experience yeye mwenyewe, alikuwa very angry of the white man system jinsi ilivyo curse watu wa tabaka tofauti hasa Mexicans, African Americans and the rest.

Ngoma bora toka kwake,
- Letter to my unborn child
- Pain
- White man's world
- All eyez on me
- Brenda got a baby
- Killuminate
- Gangster party
- keep your head up
- Dear Mama

Na nyingine nyingi sana, jamaa alikuwa na elimu kubwa sana ya mtaa kutoka kwa ma ex-members wa black panther Akiwepo mjomba wake Platt. Suge alikuja muongezea kiburi baada ya kumpatia backup ya security, production na bills mbalimbali ikiwemo ile ya kumtoa jela.

Christopher Frank a.k.a BIG yeye alikuwa mzee wa game la biashara, flow za kiparty most of the time, reasons why Diddy amekuja kuwa tajiri na Suge kuwa na makesi shazi. Bad boyz walifocus kwenye mpunga zaidi, Death Row/ OutLawz walikuwa kimkakati zaidi na ndio maana utakuta members wa Pac waliitwa kina Gadaffi, Iddi Amin, Hussein na vitu kama hivyo.

BIG anangoma kali pia hasa kwenye album ya born again, my favourite song ni SKY IS THE LIMIT.

Hakuna kama Tupac, Hakuna kama BIG, Hakuna kama Wutang clan, hakuna kama Rakim, hakuna kama KRS ONE, hakuna kama Niggers With Altitude, hakuna kama old school.

BIG ana ngoma inasema YOU'RE NOBODY TIL SOMEBODY KILLS YOU, I guess this is the reason why jamaa wamejulikana sana hasa huku kwetu.
 
BIG nadhani kweli, yeye kama yeye hakuwa vile, ila alikuwa na team ya vijana wenye flows nzuri,

Ila Pac was more than a Rapper, alikuwa ni mwanaharakti , Thinker na Futurist pia.
We unajua kiongozi, pale Bad Boyz kulikuwa na vichwa, kina Craig Mack R.I.P, yule mtoto wa kike Heather B na wengine wengi. Tupac was bigger than Rap itself. A seed of Black panther movement, representing ghetto na mnazi mkuu wa Hennessy. Alichukia sana madawa japo alishakili kuwahi kuuza japo hakutumia maisha yake yote. Nadhani alijionea madhara yake kwa mama yake marehemu Afen Shakur.
 
Joyner Lucas - Devil's Work
 
Huu wimbo naupenda sana lyrics na beats zimetulia πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½

Huwezi amini hii nyimbo ilitoka mwaka 1993 na Pac alikua na miaka 22 tu kwa wakati huo, Tupac acha kabisa.. heshima yake itabaki vizazi na vizazi
 
We si kizaz cha diamond platnumz so huwez mjua 2pac..sikiliza nyimbo ya dear mama,sikiliza ujumbe halaf jiulize kijana wa miaka 20 au 23 anaweza kua na mind ya kusema yale aliyosema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…