Pac alikuwa mtu hatari!! Acha awe king tu wa hip hop heshima inamfaa, mie naona yeye ndio kama alibadilisha game kutoka ile style ya kurap ambayo dunia nzima ilikuwa inatumia mpaka ikawa kila mtu anarap anavyojisikia!! Ndani ya umri mdogo alifanya mambo makubwa katika game ya hip hop!!
Mziki kama mziki ninavyotafsiri mimi mziki ili uwe mzuri aidha uwe unasikilizika(kuburudisha) ama uwe unafunza(maneno fulani kuntu) au uwe na vyote.
1. Kusikilizika music, namaanisha uwe mtamu masikioni, hapa hata km mtu haelewi mashairi, haelewi kilichoimbwa, lakini uwe mziki mtamu masikioni utapendwa, kina psy na gungnam style, sijui usiniseme kama napenda kula kina ali kiba, sijui despacito, unakuta mtu hajui kilchoimbwa au mashairi hayana kitu ila kwakuwa ni mtamu masikioni mwake unakuwa mziki mzuri
2.kufundisha, sijui nitumie neno kufundisha ama nisemeje sijui hapa nazungumzia mashairi kuwa mazuri, yaani mtu anaupenda muziki kwa mashairi na sio kusikilizika masikioni,hapa inalenga wanaoelewa mashairi, unamkuta mtu anapenda nyimbo fulani we unaweza kuita wa kawaida kumbe ni mtu anasikiliza message ya mule!
Hip hop kama hip hop imebase kwenye mziki mzuri wa aina ya pili, wasikilize kina fid q, sijui jigga, eminem, kendrick na wengineo utanielewa hapa, hata kama mziki sio mtamu masikioni ila mashairi yake tu yanamfanya mtu akakipenda kitu..
Turud kwa tupac, pac alikuwa na mziki mzuri kwa kusikilizika hata kama huelew kinachoimbwa na mashairi mazuri kwa pamoja
Sikiliza
Dear mama
I aint mad at cha
Untill the end of time
Keap ya head up
So many tears
Change
Me n my girlfriend
Nakadhalika nakadhalika.
Binafsi namuelewa mno pac anahitaji heshima yake, naamin jamaa alikufa akiwa bado hajafikia kilele chake, ndio kwnza alikuwa anasogea kwenye peak yake sijui angeipata peak yake ingekuwaje, now angekuwa na heshima zaidi, sijui kama asingekuwa mwanamuziki milionea pia, tizama toka alipoanza mpaka kifo chake jamaa alikuwa kwenye graph yake ndio kwanza anapanda.