Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 28,916
- 40,479
Eazy E alikuwa muhuni sana na alikuwa anachana piaMkuu ilikuwa vipi jamaa kumtukana Dre ,wakati anakata roho ,chimba kidogo mkuu
Washkaji zake wa karibu sana walikuwa ni Ice Cube, Mc Ren Yella na Dr. Dre, wakati huo Snoop yupo nyumbani kwao hana hata ishu.
Eazy E alikuwa mtafutaji na alitumia muda na pesa zake kuimarisha kundi lao la Niggaz With Attitude (N.W.A)
Baadae Dr. Dre akamsnitch jamaa baada ya Dre kupata pesa kiasi na akaanzisha kundi lake...mbaya zaidi akamdiss Eazy kuwa kuna siku Eazy alienda kudowea chakula nyumbani kwake na sasa amekuwa masikini
Hicho kilimuuma sana Eazy E na baadae Eazy alipata maambukizi ya HIV kwasababu alikuwa anatembea na mwanamke muathirika anayejiuza ambaye pia kina Dre walikuwa wanamfahamu na kumdharau pia alikuwa anawasambazia madawa (kumbuka katika kundi lao walikuwa hawataki kuoa na walikuwa wanapiga sana wanawake)
Baadae naye Eazy akatunga nyimbo za kumtukana Dre na Snoop kuwa wamepata pesa na kumtelekeza na hata kwenye Interviews nyingi alimtukana sana Dre na snoop
The real Muthaphuking n.k
Ukifuatilia kiuhalisia ni kwamba baada ya vipimo vya Eazy E kujulikana ana ngoma na alivyoanza kuzidiwa na kulazwa hospitalini kina Dre walimtelekeza kabisa na kumuimba vibaya, na wakati huo ''Dearth Row'' ya kina Snoop, Tupac na Dre ndio ilikuwa habari ya Compton - California
Watu ambao walikuwa wana Ule ushkaji wa KWELI kipindi hicho ambao Eazy E hakuwadiss ni Tupac na Ice Cube.