Hii ya njiwa imenikumbusha japo haina uhusiano na uzi huu, miaka kadhaa nyuma nipo ofisi fulani; ile asubuhi tumefungua ofisi mara tunakutana na njiwa yupo juu ya desk ya mtu fulani aliyekuwa likizo. Ukizingatia yule njiwa alikuwa amepakwa rangi nyekundu chini ya mabawa halafu ni hawa njiwa wa kufugwa na maeneo yale si makazi ya watu ebana eeeh si kila mtu akaogopa hata kuingia. Sasa kuna mmaza mmoja akaanza kumkandia jamaa aliyekuwa likizo kuwa huwa ni mshirikina na atakuwa anahusika na hilo tukio(na kweli yule mwamba alikuwa na vielementi fulani visivyoeleweka), wote wakamsapoti na wakakubaliana yule njiwa akatupwe chooni.
Niliwapinga nikawaomba yule njiwa nimchukue ama wamwachie badala ya kuuwawa kikatili kwa kutupwa chooni. hoja yangu ilikuwa ni kwasababu dirisha tulikuta halijafunga vizuri hivyo niliamini aliingilia hapo. Ila sikueleweka, wakasema huyu ni jini, basi wakamtupa kwa choo.
Sasa lile tukio lilikuwa habari kuu kwa siku hiyo, hadi pale officer mmoja alipowasili mchana kutokea field huko alikokuwa akitekeleza majukumu yake akasema; jana majira ya jioni aliona watoto(vijana) wakimfukuza huyo njiwa ndipo alipoingia kwa fensi na kubaki juu ya mti, akasema anahisi ndio huyo baadae aliingia ndani.