Tupatiane True Story yoyote ila iwe Fupi na Precise

Tupatiane True Story yoyote ila iwe Fupi na Precise

Mimi mjomba wangu alidharaulika sana na ndugu zake wadamu na baba yake mzazi (babu).
Alibakia na suruali moja ikabidi aanze kutembea usiku mchana analala.Alikuwa anakula mara moja kwa siku( waliokuwa wananunua msosi walikuwa wanatoa shombo nyingi)
Kufupisha stori fedha yake ya kwanza kuipata ilikuwa milioni 18.Siku amekuja nayo wanandugu wakapendekeza ichimbiwe chini.Alimnunulia babu kila kitu mpaka viwembe hilux ilikuja imejaa vitu.Babu yangu alivyoona vile vitu akaanza kulia ila alivipokea kwani alishawahi kumtabiria atakuja fanya kazi stand ndio kunamfaa.Alifanya kazi Sandvik Tanzania licha ya cheti chake cha elimu ya masafa marefu( Hajawahi kukanyaga chuo chochote). Nimechoka kusimulia.Usimdharau mtu usimkatie tamaa mtu.Hiyo ndio stori yangu ya leo.
Asante .
Yupo wapi Sasa hivi
 
Yupo wapi Sasa hivi
Yuko Chunya anaplant huko anafanya shughuli zake .Aliniambia kuanza sasa hivi uncle nimechoka kutumwa nakuulizwa maswali kuanzia asubuhi mpaka jioni ,maswali tu.Halafu watu usiku wanafikiria matatizo mimi asubuhi nitafute masuluhisho.Naacha kazi.Na kweli akaacha .Tena kipindi hicho anakunja karibu m3 .Ila base yake ipo Mwanza .
Oiiii.
 
Miaka ya 2005 nilikuwa natoka tuition na wenzangu sasa kwenye kuvuka barabara wakaniacha nyuma, kulikuwa na kimteremko alafu kulikuwa na baiskeli inakuja😂, wenzangu wakaniambia vuka tuu ipo mbalii ile navuka tu baiskeli nayo imefika😂😂😂😂Nikagongwa na baiskeli bwana.

Ninachoshukuru sikuumia zaidi ya kupata michubuko midogo mdomoni, basi kwenye zile purukushani za kuamka watu kusogea sogea,kuna rafiki yake mama alisogea pia na alikuwa nesi akaniokota akanipeleka kwake akanisafisha tu kidogo nikaenda nyumbani. Nilivyofika nyumbani nikadanganya nimeanguka tu.
 
Yuko Chunya anaplant huko anafanya shughuli zake .Aliniambia kuanza sasa hivi uncle nimechoka kutumwa nakuulizwa maswali kuanzia asubuhi mpaka jioni ,maswali tu.Halafu watu usiku wanafikiria matatizo mimi asubuhi nitafute masuluhisho.Naacha kazi.Na kweli akaacha .Tena kipindi hicho anakunja karibu m3 .Ila base yake ipo Mwanza .
Oiiii.
Kweli maisha yana Siri
Usimdharau mtu wala kumkatia tamaa
Mungu azidi kumtunza
 
Kuna mwaka Nilienda kwa wakala kuweka Hela CRDB Sasa yule jamaa akasema Hana Salio la kutosha nikawa napiga nae story mara vuup Kuna limtu lilikuwa linapita barabarani likaona Hela ilivojichora mfukoni likasogea mpaka pale nilipokuwa likawa linajifanya kama ni limteja nalo

Mara paap likaanza kupapasa kwenye mfuko wangu wakati ambao Mimi naongea na yule wakala nikahisi kama naguswa mfukoni niliondoka bila kuaga yaani nilichukuw vitu vyangu na kusepa kama nakimbizwa bahati nzurii kwenda kuangalia nakuta Hela yote ipo nilishukuru mungu maana ningeibiwa KIZEMBE siku ile
Kariakoo juzi Kati jamaa nikiwa nimebeba kibegi mgongoni jamaa akanifuata kwa nyuma akawa anafungua zipu kwakua Mimi ni mafia / ninja / mbabe/ zee korofii/ mtukutu wa nyaigera e.t.c

Nikageuka fasta nikashika mkono ukiwa kwenye begi nikamwambia kwa kumaanisha ntamalizana na wewe hapa hapa chap chap
NTAKUTOBOA MACHO sasaivi na mtu yeyote asijue.
Jamaa likawa linatetemeka na nikaliacha linaondoka kwa fadhaa kubwaa sanaa
 
Kariakoo juzi Kati jamaa nikiwa nimebeba kibegi mgongoni jamaa akanifuata kwa nyuma akawa anafungua zipu kwakua Mimi ni mafia / ninja / mbabe/ zee korofii/ mtukutu wa nyaigera e.t.c

Nikageuka fasta nikamwambia kwa kumaanisha ntamalizana na wewe hapa
NTAKUTOBOA MACHO sasaivi na mtu yeyote asijue.
Jamaa likawa linatetemeka na nikaliacha linaondoka kwa fadhaa kubwaa sanaa
Ungelipiga za uso
 
Ki shule shule! Tumetoka class tunawahi kuoga then turudi kula chakula uck.

Sasa kulikuwa na vyoo vya juu ya ghorofa na vingine vipi chini! Ridochi hiyo Eckenforde

Mimi nikawahi choo kimoja ila Nikakuta kimefungwa afu kama Kuna mtu ndani maana nilikuwa naskia maji yamefunguliwa kwenye ndoo!

Nikamwambia yule wa ndani! Oya Chap chap utoke niingie! Nikaa nje namsubiria atoke! Tena nilikuwa na jamaa angu hapo nje.

Gafla maji yakafungwa! Nikajua mtu yule kamaliza ili atoke! Malango ukafunguka na hakuna mtu ndani!

Weee! Tulitoka ndukiiii! Mambo ya Tanga hayo
Huenda ni Ms Corridor alikua anafanya yake
 
Inashangaza! Mi nami nilishangazwa na ndege mmoja kudandia mwewe angani na kubebwa mgongoni wakatokomea kusikojulikana. Kuna siku natembea kando ya ufukwe ghafla mwewe akatua kichwani kwangu bila kuniogopa, nikamtimua aruke, ila hakunijeruhi.
Kuna MWEWE na KUNGURU

miguu ya MWEWE ni zaidi ya KISU kikali Sanaa..
 
Duh aiseee tabia mbaya sana aliyowafanyia jamaa
Hiki Cha Mwisho! 😂

Enzi hizo Bado Tanga hotel ni ya moto inamilikiwa na Mzee Tarimo.

Tumetoka breakfast ya saa nane! Kikombe kimoja Cha chai na maandazi mawili. Tulikuwa hatushibi

Mara papa kushuka kwenye ngazi tunakutana na jamaa yetu, amebeba chapati mbili afu yeye kama anatafuna

Akasema nimewaletea chapati ila mle hapa hapa tusije tukaulizwa tumezipataje! Mimi na jamaa acha tufakamie haraka haraka! Ile tumemaliza yule mleta chapati akaanza kucheka mpk analalala chini.

😳😳😳 Tunajiuliza mbona jamaa anacheka!

Ndo mtu mwingine anatokea anatuambia! Kuna jamaa wa form Three alitoroka kwenda kununua chapati akakamatwa na headmaster

Akamnyang'anya chapati afu akazitupa chini akazikanyanga kanyaga na viatu ndo jamaa akaziokota akaja kutulishaa

😂😂
 
Kariakoo juzi Kati jamaa nikiwa nimebeba kibegi mgongoni jamaa akanifuata kwa nyuma akawa anafungua zipu kwakua Mimi ni mafia / ninja / mbabe/ zee korofii/ mtukutu wa nyaigera e.t.c

Nikageuka fasta nikashika mkono ukiwa kwenye begi nikamwambia kwa kumaanisha ntamalizana na wewe hapa hapa chap chap
NTAKUTOBOA MACHO sasaivi na mtu yeyote asijue.
Jamaa likawa linatetemeka na nikaliacha linaondoka kwa fadhaa kubwaa sanaa
Bila machale Apo tayarii kingekuwa TATIZOOO
 
Back
Top Bottom