Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Habari za Asubuhi Dada yangu Doroth.
Nimekaa kwenye Sheria kwa muda mrefu , nina uzoefu sasa miaka 24 tangu niingie Kwenye kazi.

Sheria ya mtoto inataka Welfare of the Child na inalinda mtoto , nina maswali machache:-
​
  1. Sheria haiwahusu watoto wadogo wanaojipanga mataa usiku kuomba mpaka saa nane usiku, mataa ya Sta Peters, Morroco, Mwenge, Ubungo , Posta Dar es salaam?​
  2. Sheria haiwahusu watoto wanaobebwa mgongoni na wazazi wao wanaouza maparachichi kwenye mataa ya kwenda masaki hapo St Peters, wanachomwa na jua kuanzia asunbuhi mpaka jioni?​
  3. Sheria haiwahusu watoto ambao mahakama imewapa custody wanawake na wanawake wanazuia waname kuwaona watoto?kama sivyo, wanaume hata wakifanya enforcement mahakama huwa haizingatii, ila mtoto anahitaji mapenzi ya baba na mama .​
  4. Je, Hawa wanaotoa mimba kwa wanafunzi na wanafahamika , hospitali zao na vituo vya afya, wanatoa kisheria?​
 
Sheria inawahusu hao watoto lakini umaskini walionao wazazi wao, unawahusu zaidi.

Umaskini wa wazazi wao ni wa kimfumo toka ndani CCM. Mheshimiwa Waziri Hana uwezo wa kupambana nao.
 
Nashauri vigodoro vipigwe marufuku kufanyika kwenye open grounds, baadala yake vifanyike kwenye kumbi za starehe usiku wa manane.
Uswahilini hufanyika tu hovyohovyo akina dada wakivua nguo mitaani na kuonyesha makalio yao hadharani mbele ya watoto na watu wasiopendelea mambo.

Kuna hii tabia yakina dada kucheza kwenye magari mchana kweupe huku watoto wakishuhudia hayo mambo yao ya hovyo, hili jambo pia lipigwe marufuku na kufanyika kwenye special venues na sio hovyohovyo mitaani.
 
Karibu sana na hongera kwa uchapakazi.
 
Yako mengi ila kwa wizara hii ya maendeleo ya jamii ni Watoto, Wazee, Wajane, na Wafanyabiashara ndogo ndogo.

Kundi la wenye ulemavu liko Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Wizara ya Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu.
Shukrani
Mama ili kupunguza unyanyasaji wa kingono na kisaikolojia ipigwe marufuku wadada kuvaa vinguo vya utupu utupu na vinavyo reveal mwili wao
 
Kuna utofauti mkubwa kati ya ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii. Hili mnalijua ila mnalichqnganya sana na hata wewe binafsi linakusumbua kwelikweli kulifanyia kazi na kuzungumza
Idara ya ustawi wa jamii inajitegemea kabisaaa mbona haina bajet huko halmashauri?
 
KILIO:Nikuombe sana MH, Waziri msikivu namba sana na Mungu atusimamie hili unapoliwakilisha kwa Raisi msikivu,Namba sana Tena sana Kwa Moyo wa unyenyekevu!Tuliowahi kuwa wafanyakazi,tunapita wakati mgumu hasa tuliowahi kufukuzwa kazi!unakuwa mwanachama wa mfuko wa Jamii na umechangia miezi mia na themanini (180)Lakini kwa Sababu ulifukuzwa na mwajiri unaambiwa hustahili kupata Hilo fao la uzee!Kweli Waziri wangu naomba sana mpelekee KILIO hiki Mh:Raisi kuwa watu wanasononeka sana Kwa hili maana linaumiza sana, wengine waliofukuzwa kwa Hila, majungu nk sio sawa Tena kwenye mifuko kuwahukumu mara ya pili.Nao ni watu waliolitumikia Taifa Kwa Uzalendo pia
Wote wafae kupewa mafao ya Uzeeni,wakimbilie wapi na nguvu zimewaishia?
 
Pia linaongeza stress za maisha,maana kama waliopunguzwa Kwa redundancy wanalipwa!,Hawa kuwanyima Kwa sababu ya kufukuzwa ni kuwanyanyapaa Kwa namba Fulani, maana wengine walifungua mashauri mahakamani na wakashinda hizo kesi na kumalizana na mwajiri kistaarabu.Hili wazuri tuokoe wananchi wenu ili tufaidi pia keki ya Utumishi.
 
Unajua hakuna bajeti specific kwa akili ya ustawi wa jamii?
Unajua wewe ni wazir usiyejua tofauti kuua iliyopoa kati ya ustawi na maendeleo
 
mimi kuna kitu hapa hizi sule zamsingi za serekali mtoto ili aanze shule nilazima atoe helo yote yachakula bila hivyo haandikishwi natumeambiwa elimu nibure hii imekaaje
 
wambie maustawi wajamii na maendeleo(wakaimu hawa wa ustawi wajamii) ,waache kula rushwa na kushauri waliotoa rushwa juu ya malezi ya watoto kwenda mahakama za mwanzo badala mahakama za wilaya kwenye kitengo

wananchi wanalalamika sana
 
wambie maustawi wajamii na maendeleo(wakaimu hawa wa ustawi wajamii) ,waache kula rushwa na kushauri waliotoa rushwa juu ya malezi ya watoto kwenda mahakama za mwanzo badala mahakama za wilaya kwenye kitengo

wananchi wanalalamika sana
Naweza kupata taarifa za hao wala rushwa kuja sms 0765 345 777. Maana TAKUKURU wapo ila hamshtaki. Tushirikiane tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…