Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 966
- 6,019
- Thread starter
- #201
Ahsante Sana kwa maswali yako mazuri.Kuna maswali machache huwa najiuliza pasipo kupata majibu
Kwamfano.
Kunafaida gani kumfunga mume au baba wa watoto aliye shindwa kutimiza mashart/mkataba alio wekewa na afisa ustawi wa jamii?
Huenda Labda anashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kipato kidogo alicho nacho au mazingira magumu kikazi anayo yapitia
hatimaye anashindwa kutimiza masharti Kisha anafikishwa mahakamani na kufungwa
Sasa ninge penda kujua kwamba
je! huwa mnajilidhisha vipi Kama ameshindwa kwa makusudi mpaka mna amua kumfunga kwa kosa la kushindwa?
Kingine ninacho jiuliza nikwamba
je! kumfunga huyo baba kuna wa saidia Nini watoto watakao Baki na mama yao au watoto na mama huku nje ya jera
Je Kuna fungu mnalitoa Kama serikali kwa ajiri ya kuwasaidia mama na mtoto/watoto kipindi ambacho baba yao mme mpeleka jera?
Kwa jinsi ninavyo fahamu Mimi hakuna baba anaye weza kuishi kwa amani wakati huku nyuma watoto wake wanatembea uchi,Wana lala njaa, nk
haiwezekani Labda Kama amepaka ziwa hao watoto anaweza kuya tenda hayo
Sasa je!
Kuna hasara gani huyo baba akiachwa huru lakini aka ambiwa kwamba ajitahidi kufikisha mahitaji kadri mungu atakavyo mjaria
iki wezekana hata kwa kutishiwa kitaaramu
je! hili halita kuwa Bora kuliko lile la kumfunga??
Kuna Jambo lingine siku hizi limekuwa Kama biashara kwa wake zetu/wanawake
Kwamba ana kuchunguza kuhusu kazi na kipato chako akishajua aka jiridhisha kwamba kunafaida ataingiza/kutengeneza kutoka kwako Kama mwanaume
Ana amua kuzaa na wewe baada ya kuzaa nawewe Ana Anza kuleta ugomvi wa makusudi ili mgombane/muachane
baada ya kuachana anakimbilia ustawi wa jamii anakuingiza mkataba kisha anaenda kuwinda mwanaume mwingine
Nahuyo mwingine nayeye ana mfanyia hivyo hivyo"
na Hawa ndio wale wanawake ambao Kila mtoto ana baba yake"
Sasa nilitaka kujua kwamba je mnalijua hilo
na mna kabiliana nalo vipi ili kuepusha hizi single parents family?
Je! Ni Nini hatima ya watoto kulelewa na mzazi mmoja?
Na mnapo mfunga baba kwa kushindwa naomba ni rudie Tena kwakushindwa sio kwa makusudi kuhudumia familia yake
Huwa mna fikilia Nini hatima ya upendo wa baba kwa watoto ambao alipelekwa jera kwa ajiri yao?
Lingine ni kwamba je mna fahamu kwamba wanaume Wana nyanya Sika na wanawake?
na hata huko mnako waambia waende hawasaidiwi zaidi ya kuchekwa?
Mwisho niulize kwamba
Je! hakuna namna nyingine ya kunusuru kizazi chetu na malezi ya mzazi mmoja zaidi ya hii iliyopo?
ahsante
Muda huu nitajibu hoja chache tu, maana ziko nyingi, zingine nitaendelea.
Kuhusu baba watoto kufungwa; kwa kifupi kabisa, kufungwa huwa ni hatua ya mwisho kabisa katika mnyororo wa kutafuta amani ya ustawi wa jamii na pale ambapo mahakama imejiridhisha kwa mujibu wa sheria kuwa, ndugu yetu huyu anazo hatia na hana la kujitetea au utetezi wake labda hauna mashiko.
Kuhusu ubora wa sheria; sheria za nchi yetu huandaliwa kwa utaratibu stahiki uliowekwa. Hivyo, iwapo inaonekana kuna kifungu kimepitwa na wakati, ni kutoa maoni tu utaratibu wa mapitio ufanyike.
Ahsante Sana kwa leo, nakutakia usiku mwema na baraka.