Heri ya Pasaka wana JamiiForums,
Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.
Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.
Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.
Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.
Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).
Karibuni
mheshimiwa,mimi ninanyanyaswa sana,nilibebeshwa mimba na afisa mtendaji wa kata baada tu ya kumaliza form four,baada tu ya kubeba mimba mwenzang akabadirika mimi sikuhitaj anioe maan sikumuona kama anafuture yoyote,nilihitaji tu nipate matunzo lakini sikupata mpaka nikajifungua mtoto wa kiume na sasa anamiaka mitatu na nusu sipati msaada wowote toka kwa mzazi mwenzangu nahangaika kumlea pekeang mtoto nimefika mpaka ustaw nipate walau hata hel ya sabuni lakin nilioshia kupewa namba za simu ili nikipata shida niwapigie.naomba nisaidie mwanangu apate haki.Natumaini utanisaidia