Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Habari za Asubuhi Dada yangu Doroth.
Nimekaa kwenye Sheria kwa muda mrefu , nina uzoefu sasa miaka 24 tangu niingie Kwenye kazi.

Sheria ya mtoto inataka Welfare of the Child na inalinda mtoto , nina maswali machache:-
  1. Sheria haiwahusu watoto wadogo wanaojipanga mataa usiku kuomba mpaka saa nane usiku, mataa ya Sta Peters, Morroco, Mwenge, Ubungo , Posta Dar es salaam?​
  2. Sheria haiwahusu watoto wanaobebwa mgongoni na wazazi wao wanaouza maparachichi kwenye mataa ya kwenda masaki hapo St Peters, wanachomwa na jua kuanzia asunbuhi mpaka jioni?​
  3. Sheria haiwahusu watoto ambao mahakama imewapa custody wanawake na wanawake wanazuia waname kuwaona watoto?kama sivyo, wanaume hata wakifanya enforcement mahakama huwa haizingatii, ila mtoto anahitaji mapenzi ya baba na mama .​
  4. Je, Hawa wanaotoa mimba kwa wanafunzi na wanafahamika , hospitali zao na vituo vya afya, wanatoa kisheria?​
 
Sheria inawahusu hao watoto lakini umaskini walionao wazazi wao, unawahusu zaidi.

Umaskini wa wazazi wao ni wa kimfumo toka ndani CCM. Mheshimiwa Waziri Hana uwezo wa kupambana nao.
 
Nashauri vigodoro vipigwe marufuku kufanyika kwenye open grounds, baadala yake vifanyike kwenye kumbi za starehe usiku wa manane.
Uswahilini hufanyika tu hovyohovyo akina dada wakivua nguo mitaani na kuonyesha makalio yao hadharani mbele ya watoto na watu wasiopendelea mambo.

Kuna hii tabia yakina dada kucheza kwenye magari mchana kweupe huku watoto wakishuhudia hayo mambo yao ya hovyo, hili jambo pia lipigwe marufuku na kufanyika kwenye special venues na sio hovyohovyo mitaani.
 
Kuuliza si ujinga nini maana ya mkundi maalumu?
Yako mengi ila kwa wizara hii ya maendeleo ya jamii ni Watoto, Wazee, Wajane, na Wafanyabiashara ndogo ndogo.

Kundi la wenye ulemavu liko Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Wizara ya Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu.
Shukrani
 
Back
Top Bottom