Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Ushauri wenu kwenu fuatilieni kozi ya social work ipo chini ya wizara yenu, kuna mauza uza mengi sana kwenye hii kozi kwa upande wa cheti na diploma,
Ikikupendeza sms tafadhali kwenye 0765345777 kwa wepesi zaidi Ili kujua shida hasa Iko wapi nimpe mkuu wa Chuo husika. Shukrani
 
Mheshimiwa ubarikiwe sana kwa huu uthubutu wa kusikiliza kero za wananchi.
 
Salaam. Ahsante kwa muda wako na maoni yako. Wizara hii ni ya Jinsia zote. Ndiyo maana sera mpya ya jinsia ya Mwaka 2023 ukurasa wa 22 unaongelea wanaume (male engagement). Ndiyo maana watoto wote chini ya miaka 18 inahusu jinsia zote. Labda useme umekwama wapi na ukakosa huduma gani tafadhali?
Sidhani kama tunahitaji kuonbelewa kwenye sura. Tunahitaji kujumuishwa kwanza kwenye jina lililobeba wizara. Neno wanawake liondoke hapo libaki jinsia
 
Salaam. Ni kweli nilikuwa bize wala si uongo. Ndiyo naingia humu Leo baada ya siku kadhaa. Lakini pia, kwa dharura huwa Nina mbadala wa mawasiliano. Unaandika na kutuma ujumbe kwenda 0765345777 na copy 0734124191. Ahsante sana
Shukran sana mama, Mungu akulipe wema kwa kutusaidia sie wanyonge. Nitafikisha salamu na kumpa namba atume ujumbe kwako. Ubarikiwe mkuu.
 
Kwanza pole nyingi kwa Binti huyu. Pia, huyu Binti kama ana mawasiliano mpe namba yangu ya simu anitumie ujumbe nitamuongoza akikwama.

Utaratibu rasmi ni, aende Dawati la jinsia polisi aandikishe maelezo. Pale atapewa mtaalamu wa ustawi wa jamii atasikiliza shauri hili na kuliongoza kwenye utaratibu.

Upo msaada wa kisheria pia, akihitaji atapewa.
Ahsante Sana

Niwie radhi kuchelewa kujibu, mambo huwa wakati mwingine yanakuwa mengi.
Nimemfikishia ujumbe amefurahi sana mpaka amelia kwa furaha kwa jinsi ulivyompa matumaini. Kwa kweli huyu mwanaume ni shetani sana, inabidi achukuliwe hatua za haraka sana. Bila shaka binti atawasiliana na wewe kwa namba za sms. Asante sana mkuu.
 
Maeneo muhimu ya kuzingatia ni pamoja na:

1. Usawa wa kijinsia na kuimarisha uwakilishi wa kijinsia:
- Kuanzisha mipango maalum ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika maamuzi ya kisiasa na kiuchumi.
- Kuboresha sera na sheria zinazolinda haki za wanawake na kuhakikisha utekelezaji wake.
- Kuhamasisha ajira na fursa sawa za kimaendeleo kwa wanawake.

2. Kukabiliana na ubaguzi na dhuluma dhidi ya makundi maalum:
- Kujenga ufahamu wa jamii kuhusu haki za binadamu na kupambana na mitazamo duni.
- Kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa makundi yenye mahitaji maalum.
- Kuongeza ushiriki na uwakilisho wa makundi haya katika ngazi zote za uongozi.

3. Kuimarisha elimu na ujuzi:
- Kuhakikisha upatikanaji wa elimu bure na ya ubora kwa wote bila ubaguzi.
- Kuhamasisha ushiriki wa wanawake na makundi maalum katika fani za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.
- Kuongeza uwezo wa walimu na wataalamu katika kushughulikia masuala ya usawa na ukweli.

4. Kukuza utamaduni wa haki na usawa:
- Kuendeleza kampeni za mawasiliano ya jamii kuhusu usawa na haki za binadamu.
- Kuhamasisha ushiriki wa jamii katika kuleta mabadiliko ya kimtazamo na desturi.
- Kujenga uwezo wa taasisi za kiraia katika kulinda na kutetea haki.

Ushirikiano baina ya serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia na jamii kwa ujumla ni muhimu sana katika kutekeleza mikakati hii.
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karib
 
Baadhi ya njia bora za kufanya hili ni:

1. Kuunda Nafasi Maalum za Uwakilishi:
- Kutunga sheria na sera zinazohakikisha uwakilishi kamili wa makundi maalum katika bodi, kamati na vikao vya uamuzi.
- Kusimamia utekelezaji wa sera hizi kwa kukagua na kuripoti mara kwa mara.
- Kuunda nafasi maalum za uongozi kwa ajili ya makundi maalum katika ngazi mbalimbali za uongozi.

2. Kuimarisha Uwezo na Uwezeshaji:
- Kutoa mafunzo na maendeleo ya uongozi kwa wajumbe wa makundi maalum.
- Kuimarisha rasilimali na uwezo wa vyama vya kiraia vinavyowakilisha maslahi ya makundi maalum.
- Kutoa msaada wa kifedha na kiufundi kwa makundi haya katika kushiriki katika ngazi za uamuzi.

3. Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji:
- Kuhakikisha kuwa taratibu za uchaguzi na uteuzi wa wajumbe wa ngazi za uamuzi ni wazi na haki.
- Kuwezesha upatikanaji wa taarifa na ushiriki wa wananchi katika mchakato wa uamuzi.
- Kuimarisha uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi, hasa makundi maalum.

4. Kuhamasisha Ushiriki wa Jamii:
- Kuanzisha kampeni za mawasiliano ya jamii kuhusu umuhimu wa ushiriki wa makundi maalum.
- Kuwezesha ajira na ushiriki wa wanajamii kutoka makundi maalum katika ngazi za uamuzi.
- Kutoa motisha na kuenzi viongozi kutoka makundi maalum wanaofanya kazi nzuri.

Kwa kutumia mbinu hizi, tunaweza kuwezesha ushiriki na uwakilishi kamili wa makundi maalum katika ngazi za uamuzi.
 
Sawa mheshimiwa. Basi anza mchakato huo. Kwanza naelewa kuwa suala hilo sio la tafiti bali kura. Mchskato wa kuondoa mfumo jike kwenye wizara yako
Wala hakuna mfumo jike. Kwa sasa kiongozi idara ya jinsia ni mwanaume. Na idara hiyo inao wanaume wa kutosha tu.
 
Nimemfikishia ujumbe amefurahi sana mpaka amelia kwa furaha kwa jinsi ulivyompa matumaini,
Kwa kweli huyu mwanaume ni shetani sana, inabidi achukuliwe hatua za haraka sana
Bila shaka binti atawasiliana na wewe kwa namba za sms
Asante sana mkuu
Namsubiri. Shukrani
 
Wala hakuna mfumo jike. Kwa sasa kiongozi idara ya jinsia ni mwanaume. Na idara hiyo inao wanaume wa kutosha tu....
Iitwe wizara ya jinsia na makundi maalum. Kitendo cha kuiita jinsia wanawake na makundi maalum tayari umeshaweka ubaguzi. Kwamba wanawake nao wanaingia kwenye jinsia na kwa wanawake.

Hii naifananisha na kuiita Tanganyika Tanzania bara. Kwamba jinsia implies wanaume. Natamani sana hayo hapo juu yafanyike. Idara ya jinsia kuwa na wanaume haiondoi uhalisia kuwa tunahitaji uwiano
 
Amina, Shukrani
maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii ni vitu viwili tofauti nyie mnachanganya huku mkijua kabisa
idara ya ustawi wa jamii hain bajeti hilo huko halmashauri tunawambia kila siku lakini wapi
DED wa mafia kamwingilia mtoto under 18 lakini mahakama haikumtia hatiani kivipi?
 
Mheshimiwa Waziri Salaam

Wizara yako ni Nyeti sana kwa mstakabali wa nchi.

Naomba shugulikia haya yafuatayo


1. Changamoto ya Ndoa kuvunjika
Ndoa nyingi zinavunjika kutokana na ukosefu maadili kuanzia kwa familia , jamii na hata kwenye Makundi ya utetezi wa haki za wanawake.

Asilimia 95 ya ndoa huvunjwa na wanawake kutokana na makundi ya wanaitwa marafiki na kufuata mkumbo wa makundi mabaya na hatimae mwanamke hukosa utii huanza uzinzi na kuvunja ndoa...Ongeeni na wanawake Wenzenu watambue nafasi ya waume zao.

2.. Wanawake kuzaa kwa upasuaji hili ni janga kubwa zaidi...kila hospitali unayooenda hasa Miji Mikubwa kila mwanamke amezaa kwa upasuaji..Hili suala ni la kibiashara haiwezekani kila mwanammke hasa Dar apasuliwe mwanamke huyo huyo ukimpeleka Songea anazaa kwa kusukuma.

Jamani hili linaharibu sana Wanawake sana...
 
Mfanye development strategies nzuri mitaa imejaa mitaro kuko ovyoovyo pia msaidie wasiojiweza kwa kuwapa mitaji kutokana na idea ya biashara yake
 
Mheshimiwa Waziri Salaam

Wizara yako ni Nyeti sana kwa mstakabali wa nchi.

Naomba shugulikia haya yafuatayo


1. Changamoto ya Ndoa kuvunjika
Ndoa nyingi zinavunjika kutokana na ukosefu maadili kuanzia kwa familia , jamii na hata kwenye Makundi ya utetezi wa haki za wanawake.

Asilimia 95 ya ndoa huvunjwa na wanawake kutokana na makundi ya wanaitwa marafiki na kufuata mkumbo wa makundi mabaya na hatimae mwanamke hukosa utii huanza uzinzi na kuvunja ndoa...Ongeeni na wanawake Wenzenu watambue nafasi ya waume zao.

2.. Wanawake kuzaa kwa upasuaji hili ni janga kubwa zaidi...kila hospitali unayooenda hasa Miji Mikubwa kila mwanamke amezaa kwa upasuaji..Hili suala ni la kibiashara haiwezekani kila mwanammke hasa Dar apasuliwe mwanamke huyo huyo ukimpeleka Songea anazaa kwa kusukuma.

Jamani hili linaharibu sana Wanawake sana...
Ungemsaidia Mh.Waziri hizi asilimia ulizobainisha hapa umezipata wapi ,isije ikawa unazungumzia Takwinu za Familia yenu ,Halafu unafanya rejea kwenye masuala nyeti ya Kitaifa!
 
Mama mabinti huku p2 wamefanya pipi.

Tafadhari, elimu inatakiwa.
 
Back
Top Bottom