Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Unaweza kukuta hata password ya kuingia JF kashaisahau....
[emoji28] jamani mbona nipo na hili tulifanyia kazi kikamilifu kwenye Uzi uliofunguliwa na mleta taarifa? Haya ahsanteni sana. Ila kwa kuwa mambo ni mengi pia, mtu akiona ana emergency, tulifungua call center ya wizara siku za kazi, Namba 0734986503 na landline ya
026 2160250. Vilevile, kuna namba 116 ya taarifa za ukatili kwa watoto, hii ni saa 24 Kila siku. Vyote hivyo vimeshindikana, hata mimi huwa napokea rufaa moja kwa moja kwa namba 0765345777. Tabu wapi wapendwa[emoji28]

Ahsanteni kwa kujali. Naomba tuendelee na ushirikiano huu daima. Mbarikiwe sana [emoji1241][emoji120]
 
😅😅😅 Siyo kweli kabisaaaaaa. Sema hili jambo tulifanyia kazi kupitia Uzi wa yule aliyeleta taarifa. Maafisa wa Dawati la jinsia walienda hadi Kijijini kwa Binti, wakamchukua, wakampeleka hospitali kwa vipimo. Wazazi na muoaji wakakimbia. Kama kawaida jamii inapenda kulindana. Ila wanatafutwa. Binti Yuko mikononi mwa ustawi. Na yule alijifanya Mchungaji naye kumbe haikuwa kweli. Alikimbia. Anyway, tunamshukuru alitoa taarifa akipatikana sasa atajuana na Polisi, RB. 802/2023. Haya ahsanteni kwa ufuatiliaji wenu makini, tuendelee kushirikiana daima, jamii yetu, umoja wetu 🤝🇹🇿💪
 
[emoji28] jamani mbona nipo na hili tulifanyia kazi kikamilifu kwenye Uzi uliofunguliwa na mleta taarifa? Haya ahsanteni sana. Ila kwa kuwa mambo ni mengi pia, mtu akiona ana emergency, tulifungua call center ya wizara siku za kazi, Namba 0734986503 na landline ya
026 2160250. Vilevile, kuna namba 116 ya taarifa za ukatili kwa watoto, hii ni saa 24 Kila siku. Vyote hivyo vimeshindikana, hata mimi huwa napokea rufaa moja kwa moja kwa namba 0765345777. Tabu wapi wapendwa[emoji28]

Ahsanteni kwa kujali. Naomba tuendelee na ushirikiano huu daima. Mbarikiwe sana [emoji1241][emoji120]

Dkt mi natafuta kazi ya kujitolea nime specify course ya Community and development studies..

Nataman tu kufanyia Kazi kile nilichokisoma.
 
Hili sasa ungeandika wizarani Ili upate mwongozo wa kitaalamu kuhusu ombi lako.
 
[emoji28] jamani mbona nipo na hili tulifanyia kazi kikamilifu kwenye Uzi uliofunguliwa na mleta taarifa? Haya ahsanteni sana. Ila kwa kuwa mambo ni mengi pia, mtu akiona ana emergency, tulifungua call center ya wizara siku za kazi, Namba 0734986503 na landline ya
026 2160250. Vilevile, kuna namba 116 ya taarifa za ukatili kwa watoto, hii ni saa 24 Kila siku. Vyote hivyo vimeshindikana, hata mimi huwa napokea rufaa moja kwa moja kwa namba 0765345777. Tabu wapi wapendwa[emoji28]

Ahsanteni kwa kujali. Naomba tuendelee na ushirikiano huu daima. Mbarikiwe sana [emoji1241][emoji120]
Basi mheshimiwa Waziri, mimi nimeamua kukupenda ....
 
Swala la mapenzi ya jinsia moja, sioni mikutano ya kulikemea hili.
 
Mambo ya uharibifu kwenye jamii yanayofanywa na baadhi ya watu wazima na akili zao ni mengi. Yote tumekuwa tukiyasema na kuchukua hatua na zaidi tumeyapangia mpango wa hatua mbalimbali endelevu.

Kati ya ajenda hizo, kesho pia tuna press ya kuelimisha na kukemea watoto kutumika kinyume na sheria ya mtoto kwenye kumbi za starehe na mambo aina hiyo. Soma kiambatisho tushirikiane tafadhali watu wapenda ustawi wa watoto:

(ilipandishwa humu JF Jukwaa la Habari na Hoja mchanganyiko), tafadhali ndugu yetu 'dimaa' nisaidie kuivuta ije hapa Ili elimu ianze na sisi humu, kichwa cha habari ni:

"Washereheshaji na Watanzania kwa ujumla, tuzingatie Sheria ya mtoto " na maudhui yaliyomo ni kama inavyosomeka hapa chini:

"Ndugu Wafuatiliaji wa Habari za Wizara ya Jamii, Salaam!

Ahsanteni kwa ufuatiliaji wenu makini na maoni yenu mara kwa mara.

Kuna Video inasambaa ikionyesha Watoto wakitoa SHOW usiku kwenye sherehe fulani na kucheza wimbo kwa miondoko isiyofaa kwa rika lao.

Napenda kukumbusha wanajamii kuwa: Ni kosa kisheria kuwatumia hivyo Watoto kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto na 21 ya Mwaka 2009 (iliyorekebishwa Mwaka 2019) na kipande cha sheria hiyo nimeambatisha hapo kwenye bango lenye sehemu ya picha.

1) Naomba tusaidiane nani anawajua wazazi wa watoto hawa? Anitumie SMS kwenye 0765345777 tafadhali.

2. Tutakaa kikao na Chama cha washereheshaji (MCs) tuzungumze kuhusu mchango wao kwenye kulinda maadili ya watoto katika kazi zao kwa mujibu wa sheria ya watoto iliyotajwa hapo juu.

3. Pia, tutakaa kikao na Wadau wengine wote ambao kupitia shughuli zao wanaweza kusababisha kuvunjwa kwa sheria hii.

Hata hivyo, wakati tukiandaa hayo, natanguliza rai kuwa, jamii yote TUWENI MAKINI na KUMLINDA MTOTO. Sheria iko mtandaoni, TUSOMENI na TUZINGATIE vinginevyo kuna sehemu ya jamii itakutana na changamoto endapo Sheria itatekelezwa kikamilifu.
IMG-20230908-WA0068.jpg
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Binafsi, naomba ulitazame na hili hapa chini

Dkt Gwajima D

Nakutakia siku njema.

Hivi karibuni tulimsikia Dr. Harrison Mwakyembe akitutaarifu Watanzania kuwa kuna wimbi la taasisi zisizo za kiserikali zinazosambaza majanga ya ushoga na usagaji kwa jamii. Wizara yako ina mikakati ipi na inachukuwa hatua zipi kuikinga jamii na majanga hayo?

Habari zisizo rasmi, hao waeneza majanga wamelenga sana sehemu zenye watoto kwa wingi kama vituo vya kulelea "yatima", nimeweka yatima kwenye "inverted commas" kwa sababu naamini asilimia kubwa ya viltuo havina yatima wa ukweli.

Niliwahi kuandika hivi kuhusu vituo vya kulelea "yatima":

Nalo la vituo vya yatima mnalitazama vipi?

Kuna ushauri wa kuhudumia yatima ambao ntakupa baada ya kumaliza hayo ya hapo juu kwanza.
 
Dkt. Gwajima D
Pole na kazi
Msaidie huyu dada kuhusu haki ya watoto wake
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Karibu
 
Tafuteni watu wenye uwezo na weledi wa Kusoma, Kudadavua na Kutambua Discrimination, prejudice, or antagonism against people especially Tanzanians, based on their race, ethnicity and or religion. Ni muhimu kabla hatijafikia sehemu mbaya Kijamii(kisaikilojia) ir atleast spearhead something to stop this nonesense.

Nashauri muwe na Intergovernmental organisation kati yenu, polisi mtandao, TCRA, Wizara za Mambo ya Nje, na Mambo ya Ndani na wajumbe kutoka social media companies muanza kutokomeza Ubaguzi na Ugaidi(Bullying) wa mitandaoni.

Tafadhali rejea Uzi huu hapa

Kutambua uwezo wa akili kati ya mtu mweusi na mweupe angalia Korea Kaskazini na Iran dhidi ya Mataifa ya Afrika

Kama unafikiri hakuna la kuangalia.

Disregard.

Asanteni.
Wenu katika kujenga Nchi.

CC: Maxence Melo
 
Ngoja nisome, ahsante Sana kwa muda wako.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Naiomba Serikali yangu sikivu iboreshe huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum. (Wenye ulemavu).

Waangalie namna bora ya kulinda haki zao kama watoto wengine wa kawaida.

Na pia kuongeza elimu katika Jamii zetu kuhusu umuhimu wa kuwapa mahitaji yao ya msingi kama elimu.
 
Ahsante Sana, nitawasilisha maoni haya kwenye Wizara mama ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, kwa Waziri mwenye dhamana Prof Ndalichako. Shukrani Sana kwa maoni yako. Ubarikiwe [emoji1666][emoji1241]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Wanawake walioko kwenye ndoa walipwe kwa kazi za nyumbani wanazofanya. Wanaume watoe mahali, walete mahitaji nyumbani, wawalipe wamama kwa vijikazi vya nyumbani na mkiachana mgawane mali. 😁😁😁 daaaaaah! Tunakoelekea ni kuzuri sana
Hatari sana! Sheria zetu Bado zina makengeza!
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Tuwekeze zaidi kwenye familia zetu za kitanzania ambapo hakuna yatima
 
Sasa hivi hamuwajali YATIMA wala kuwapa mwanga pindi wazazi wao wote wawili wanapofariki , mnawaacha njia panda kabisa , kibaya zaidi hata mambo muhimu yakibinadamu mnawaachaniza si kama zamani mlivyokuwa mnawashika mikono , kuna waliokuwa na ndoto kubwa lakini mpaka sasa wameshindwa kutimiza ndoto zao ,na wamekata tamaa , serikali za vijiji hazioni thamani yao , na hata ndugu wanaosalia kusema wawasaidie watimize ndoto zao ni baadhi yao tu .

Je ni lini serikali itaingilia kati kuhakikisha inawashika mkono watu hawa?
 
Hongera Mhe. kwa kuaminiwa pia hongera kwa kutupa nafasi ya kutoa dukuduku letu.
mi hoja yangu inaweza kuwa tofauti kidogo , lakini utufikishie kwa Rais kwani wahusika hawataki kulishughulikia.
suala la watoto wa darasa la Nne kulazimishwa kwenda kukao Boarding kwa shule zilizosajiliwa kama DAY SCHOOLS, hii ni unyanyasaji na hili limefanyiwa utafit kwa nchi za ulaya.
nafahamu wapo ambao wanapenda lakini naomba lakini tunaojua na ambao tumepata matatizo kwa watoto wetu tunaombi dogo tu, tupewe haki yetu kama usajili wa shule ulivyo.
nyuma ya hili kuna rushwa kubwa saana kwa viongozi wa wizara ya elimu, wenye shule kwa umoja wanatoa rushwa kubwa. ndiyo maana tunaomba Rais aingilie kati.
 
Back
Top Bottom