Swala la mapenzi ya jinsia moja, sioni mikutano ya kulikemea hili.
Mambo ya uharibifu kwenye jamii yanayofanywa na baadhi ya watu wazima na akili zao ni mengi. Yote tumekuwa tukiyasema na kuchukua hatua na zaidi tumeyapangia mpango wa hatua mbalimbali endelevu.
Kati ya ajenda hizo, kesho pia tuna press ya kuelimisha na kukemea watoto kutumika kinyume na sheria ya mtoto kwenye kumbi za starehe na mambo aina hiyo. Soma kiambatisho tushirikiane tafadhali watu wapenda ustawi wa watoto:
(ilipandishwa humu JF Jukwaa la Habari na Hoja mchanganyiko), tafadhali ndugu yetu 'dimaa' nisaidie kuivuta ije hapa Ili elimu ianze na sisi humu, kichwa cha habari ni:
"Washereheshaji na Watanzania kwa ujumla, tuzingatie Sheria ya mtoto " na maudhui yaliyomo ni kama inavyosomeka hapa chini:
"Ndugu Wafuatiliaji wa Habari za Wizara ya Jamii, Salaam!
Ahsanteni kwa ufuatiliaji wenu makini na maoni yenu mara kwa mara.
Kuna Video inasambaa ikionyesha Watoto wakitoa SHOW usiku kwenye sherehe fulani na kucheza wimbo kwa miondoko isiyofaa kwa rika lao.
Napenda kukumbusha wanajamii kuwa: Ni kosa kisheria kuwatumia hivyo Watoto kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto na 21 ya Mwaka 2009 (iliyorekebishwa Mwaka 2019) na kipande cha sheria hiyo nimeambatisha hapo kwenye bango lenye sehemu ya picha.
1) Naomba tusaidiane nani anawajua wazazi wa watoto hawa? Anitumie SMS kwenye 0765345777 tafadhali.
2. Tutakaa kikao na Chama cha washereheshaji (MCs) tuzungumze kuhusu mchango wao kwenye kulinda maadili ya watoto katika kazi zao kwa mujibu wa sheria ya watoto iliyotajwa hapo juu.
3. Pia, tutakaa kikao na Wadau wengine wote ambao kupitia shughuli zao wanaweza kusababisha kuvunjwa kwa sheria hii.
Hata hivyo, wakati tukiandaa hayo, natanguliza rai kuwa, jamii yote TUWENI MAKINI na KUMLINDA MTOTO. Sheria iko mtandaoni, TUSOMENI na TUZINGATIE vinginevyo kuna sehemu ya jamii itakutana na changamoto endapo Sheria itatekelezwa kikamilifu.