FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,
Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.
Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.
Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.
Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.
Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).
Karibuni.
Asalaam Alaykum.
Mheshimiwa Waziri, nakupongeza sana kwa ujasiri wa kuja mwenyewe kujitambulisha na kutaka kwa uwazi kabisa kujuwa kero zinazotusibu kwenye jamii.
Hongera kwa hilo, uwe na moyo mkunjufu wa kuyabeba utayokumbana nayo hapa.
Kuna mengi sana ya kukushauri na kukujuza ambayo kwa kubaki kusubiri ripoti za ofisi tu usingeyapata.
Hapa utustahamilie kwa kuwa humu tuna lugha za marika tofauti na miono tofauti na namna ya uwasilishaji wa kila mmoja wetu unaweza kuwa ni tofauti na mwengine.
Chukulia tu kuwa tupo hapa basi kuna yanayokuhusu kuyafanyia kazi na kuyatatuwa, au kwa muda mfupi au wa kati na hata yatayohitaji muda mrefu.
Post yangu hii kwa leo ni ya kukukaribisha tu, sitokuchosha na kero nizionazo.
Karibu sana, Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu za ziada za kuitumikia jamii.
Kumbuka tu: Kuitumikia jamii ni kufanya kazi ya Mwenyezi Mungu. No more no less.
Karibu sana.