Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni.

Asalaam Alaykum.

Mheshimiwa Waziri, nakupongeza sana kwa ujasiri wa kuja mwenyewe kujitambulisha na kutaka kwa uwazi kabisa kujuwa kero zinazotusibu kwenye jamii.

Hongera kwa hilo, uwe na moyo mkunjufu wa kuyabeba utayokumbana nayo hapa.

Kuna mengi sana ya kukushauri na kukujuza ambayo kwa kubaki kusubiri ripoti za ofisi tu usingeyapata.

Hapa utustahamilie kwa kuwa humu tuna lugha za marika tofauti na miono tofauti na namna ya uwasilishaji wa kila mmoja wetu unaweza kuwa ni tofauti na mwengine.

Chukulia tu kuwa tupo hapa basi kuna yanayokuhusu kuyafanyia kazi na kuyatatuwa, au kwa muda mfupi au wa kati na hata yatayohitaji muda mrefu.

Post yangu hii kwa leo ni ya kukukaribisha tu, sitokuchosha na kero nizionazo.

Karibu sana, Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu za ziada za kuitumikia jamii.

Kumbuka tu: Kuitumikia jamii ni kufanya kazi ya Mwenyezi Mungu. No more no less.

Karibu sana.
 
Mama pole na hongera kwa Kazi pia;
Mama angalia hapa watoto

ila sasa sina uhakika kama ndiyo Wizara yako inayohusika, lakini nina uhakika kwa vyovyote vile ujumbe umefika/ utafika

Dkt. Gwajima D

Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Lini utumwa wa ndugu zetu walemavu utakomeshwa? Kwa nini tusichukue taarifa za ndugu zetu wahusika kisha tujue ndugu zao baada hapo naamini tatizo litaisha
 
IMG-20230627-WA0013.jpg

😍🤗🇹🇿 tumepiga hatua sasa, Wizara yenu ya Jamii kama tulivyoahidi, katika kupanua wigo wa kuifikia jamii, tumefungua kituo cha kupokea simu za wananchi kama inavyosomeka hapo. Karibuni Sana.

Nami nafurahi kuwa, wakati tukijipanga kwenye hatua hii, nilikuwa mstari wa mbele nikisaidiana na ile namba 116 na namba za Maafisa Ustawi wa Jamii nchini kote kupokea hoja za Wananchi kupitia simu nilizotangaza huku mimi mwenyewe nikionesha mfano maana shida za wananchi leo zilihitaji linalowezekana leo hiyo. Sasa tumeimarika zaidi, karibuni mfurahie huduma zetu.

Nawashukuru wote walioshirikiana nasi kwenye kipindi chote cha mpito hadi hatua hii💪🤗
 
View attachment 2670116
[emoji7][emoji847][emoji1241] tumepiga hatua sasa, Wizara yenu ya Jamii kama tulivyoahidi, katika kupanua wigo wa kuifikia jamii, tumefungua kituo cha kupokea simu za wananchi kama inavyosomeka hapo. Karibuni Sana.

Nami nafurahi kuwa, wakati tukijipanga kwenye hatua hii, nilikuwa mstari wa mbele nikisaidiana na ile namba 116 na namba za Maafisa Ustawi wa Jamii nchini kote kupokea hoja za Wananchi kupitia simu nilizotangaza huku mimi mwenyewe nikionesha mfano maana shida za wananchi leo zilihitaji linalowezekana leo hiyo. Sasa tumeimarika zaidi, karibuni mfurahie huduma zetu.

Nawashukuru wote walioshirikiana nasi kwenye kipindi chote cha mpito hadi hatua hii[emoji123][emoji847]
Mheshimiwa,
Mtanzania mimi,
Nimemaliza shahada ya uchumi wa maendeleo ya jamii (Community Economic Development ), 2022.
Ni karibu mno, ila ni mbali na uzoefu kabisaa, unanisaida vipi mtu kama mimi ambae nahitaji kupata uzoefu kuingia kwenye harakati za kupambania ajira sehemu mbali mbali.

[emoji22] So sad, volunteering now ni kama tunatafuta ajira, yaan kuipata kama mtu anaetafuta lulu shambani.

Mimi hapa, naitafuta hata sehemu ya kujitolea basi, nipate uzoefu tu, najua mengi yatakuja kupitia hivyo.
Kwa sasa na kwa kada yangu bila kuanza kujitolea mheshimiwa ni ngumu sana kuajiriwa.

Naomba msaada wako mheshimiwa.
Nipo mkoa wa KIGOMA.
Ahsante.
 
Umefanya jambo jema kuanzisha mjadala huu....

Ila nafasi/cheo ulichonacho hapo wizarani, si nafasi ya kudumu! Maana ni mteuliwa wa Raisi!

Hivyo muda wowote aliekuteua akiamua....Unaweza usiwepo kwenye hiyo nafasi!

Hivyo kama ingependeza ungeanzisha page rasmi ya wizara kama wizara, na si kwa hii account Yako...

Ukianzisha page rasmi ya wizara kama wizara...page hiyo itaendelea kupokea maoni kama wizara hata pale utakapokuwa wewe haupo.

Hizo nafasi za kuteuliwa zinategemea sana maamuzi ya yule aliekuteua, ama wananchi waliokuchagua kama mbunge...then kuteuliwa kama waziri...

Hayo ni maoni yangu tu.
Maoni yako mazuri ila page hii ina umuhimu wake huku watu wanakuwa sio waoga kutoa waliyo nayo moyoni muache aendelee huku sisi tutampa mambo mengi sana mambo ya official yabaki kuwa official.Ukitaka kufaidi au kula rojo tamu usihangaike na mtafutaji wa chakula hangaika na mpishi utaifaidi kwa siri bila mtafutaji kujua.
Karibu dada yetu usirudi nyuma kikubwa hujavunja sheria ya nchi kiujumla wizara yako ina changamoto zake za kiaina aina
 
TATIZO NYETI LA NETI ZA MISAADA ZA KUZUIA MBU KWA NIA YA KUTOKOMEZA MALERIA.
Kichwa cha habari hapo juu, chahusika mh. Waziri.
Neti hizi badala ya kuzuia maleria zinaongeza na kwa upande wangu zilileta ugomvi na mama watoto wangu. Nitafafanua ila tatizo halisi kwa ufupi ni kuwa dawa zikiisha kwenye neti, huwezi kuzipata madukani wala huko zinapogawiwa bure neti hizi.
Cha ajabu nilikuja kugundua hizi neti zinaingiza mbu baada ya kuisha ile dawa( ili hakuna anayejua ndio ujue janga lilipo)

Ipo hivi, mke wangu alivyopata ujauzito alianza clinic. Huko clinik ya. serikali alipewa neti yenye dawa akaja nayo home. Tukatoa hii tuliyonayo tukaweka ya msaada. Mwanzo ilifanya vizuri, huoni mbu akikaa kaa juu ya neti.
sasa baada ya miezi kadhaa, kama miwili na zaidi, nikawa naona mbu wawili mpaka 5 ndani ya neti. Hapo nikaanza kumshutumu mke wangu kuwa akitoka kujisaidia usiku harudishii neti vizuri. Ikawa ugomvi mana alisema namsingizia yeye sio mshamba wa kutumia neti.
Kitu kingine nikagunduwa. kuwa dawa ya kuwafukuza mbu imeisha mana sasa mbu wanakaa juu ya neti. Na wakiwa ndani wanakuwa wameshiba damu waliotuuma. Nawaua kwa hasira na kumtupia shutuma mama watoto. Sasa alivyoenda kujifungua usiku huo nililala peke yangu, Alaaa, asubuhi nakuta mbu ndani ya neti wameshiba. Sikuamini nikahisi labda hizi neti zina kiini macho. Siku inayofuata nikafunga neti vizuri na nipo peke yangu. Asubuhi nikastajabu tena mbu hao, huwa hawazidi 6.
Nikachukua neti ile ya zamani nikaweka siku iliofuata ambapo mbu hawakuingia. Kuzichunguza nikakuta hizi neti za msaada zina matundu makubwa kulinganisha na ile ya mwanzo. Ndio nilipohisi lazima mbu wanaingia kupitia matundu hayo wakiwa wembamba. Pia unafahamu mbu ana uwezo wa kutambaa kama sisiminzi akitafuta upenya autakao kupita japo huwa hatambai umbali mrefu.
Ombi langu fuatilia kwa nini hizi neti zinagawiwa kwa wingi bila kuwaelimisha dawa zake zinapatikana wapi.
Mie ile neti sina mpango wa kuitumia tena labda kuwekea uzio wa vifaranga wasichukuliwe na mwewe au kunguru. Pia usishangae kuona neti hizi zinatumika huko mtaani, kwa matumizi yasiokusudia siri ndio hio nakumegea. Neti hizi zina nembo ya Taifa wala sio feki. Sifa yake kuu ni kuwa haiozi hata ukiifukia chini, lakini kumzuia mbu asikung'ate bila dawa zake ni kazi bure.
NAWASILISHA.
 
Wanawake walioko kwenye ndoa walipwe kwa kazi za nyumbani wanazofanya. Wanaume watoe mahali, walete mahitaji nyumbani, wawalipe wamama kwa vijikazi vya nyumbani na mkiachana mgawane mali. 😁😁😁 daaaaaah! Tunakoelekea ni kuzuri sana
 
Salam Kiongozi!
Elimu ya makundi maalumu bado ipo chini sana, watu wengi tumekariri tu wanawake, vijana na watoto). Mwawanda ya makundi haya ni finye sana kiuelewa.
 
Wanawake walioko kwenye ndoa walipwe kwa kazi za nyumbani wanazofanya. Wanaume watoe mahali, walete mahitaji nyumbani, wawalipe wamama kwa vijikazi vya nyumbani na mkiachana mgawane mali. 😁😁😁 daaaaaah! Tunakoelekea ni kuzuri sana
Tunakoelekea tutafika tumechoka sana
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Kuna habari hii hapa mheshimiwa Waziri.

Thread 'URGENT: Binti wa miaka 16 ameozeshwa kwa lazima kama mke wa pili, huko Laela, Sumbawanga' DOKEZO - URGENT: Binti wa miaka 16 ameozeshwa kwa lazima kama mke wa pili, huko Laela, Sumbawanga
 
TATIZO NYETI LA NETI ZA MISAADA ZA KUZUIA MBU KWA NIA YA KUTOKOMEZA MALERIA.
Kichwa cha habari hapo juu, chahusika mh. Waziri.
Neti hizi badala ya kuzuia maleria zinaongeza na kwa upande wangu zilileta ugomvi na mama watoto wangu. Nitafafanua ila tatizo halisi kwa ufupi ni kuwa dawa zikiisha kwenye neti, huwezi kuzipata madukani wala huko zinapogawiwa bure neti hizi.
Cha ajabu nilikuja kugundua hizi neti zinaingiza mbu baada ya kuisha ile dawa( ili hakuna anayejua ndio ujue janga likipo)
Ipo hivi, mke wangu alivyopata ujauzito alianza clinic. Huko clinik ya. serikali alipewa neti yenye dawa akaja nayo home. Tukatoa hii tuliyonayo tukaweka ya msaada. Mwanza ilifanya vizuri, huoni mbu akikaa kaa juu ya neti.
sasa baada ya miezi kadhaa, kama miwili na zaidi, nikawa naona mbu wawil mpaka 5 ndani ya neti. Hapo nikaanza kumshutumu mke wangu kuwa akitoka kujisaidia usiku harudishii neti vizuri. Ikawa ugomvi mana alisema namsingizia yeye sio mshamba wa kutumia neti.
Kitu kingine nikagunduwa. kuwa dawa ya kuwafukuza mbu imeisha mana sasa mbu wanakaa juu ya neti. Na wakiwa ndani wanakuwa wameshiba damu waliotuuma. Nawaua kwa hasira na kumtupia shutuma mama watoto. Sasa alivyoenda kujifungua usiku huo nililala peke yangu, Alaaa, asubuhi nakuta mbu ndani ya neti wameshiba. Sikuamini nikahisi labda hizi neti zina kiini macho. Siku inayofuata nikafunga neti vizuri na nipo peke yangu. Asubuhi nikastajabu tena mbu hao, huwa hawazidi 6.
Nikachukua neti ile ya zamani nikaweka siku iliofuata ambapo mbu hawakuingia. Kuzichunguza nikakuta hizi neti za msaada zina matundu makubwa kulinganisha na ile ya mwanzo. Ndio nilipohisi lazima mbu wanaingia kupitia matundu hayo wakiwa wembamba. Pia unafahamu mbu ana uwezo wa kutambaa kama sisiminzi akitafuta upenya autakao kupita japi hatambai umbali mrefu.
Ombi langu fuatilia kwa nini hizi neti zinagawiwa kwa wingi bila kuwaelimisha dawa zake zinapatikana wapi. Mie ile neti zina mpango wa kuitumia tena labda kuwekea uzio wa vifaranga wasichukuliwe na mwewe au kunguru. Pia usishangae kuona neti hizi zinatumika huko mtaani, kwa matumizi yasiokusudia siri ndio hio nakumegea. Neti hizi zina nembo ya Taifa wala sio feki. Sifa yake kuu ni kuwa haiozi hata ukiifukia chini, lakinu kumzuia mbu asikung'ate bila dawa zake ni kazi bure.
NAWASILISHA.
[emoji1690]
 
Back
Top Bottom