Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Sasa hivi hamuwajali YATIMA wala kuwapa mwanga pindi wazazi wao wote wawili wanapofariki , mnawaacha njia panda kabisa , kibaya zaidi hata mambo muhimu yakibinadamu mnawaachaniza si kama zamani mlivyokuwa mnawashika mikono , kuna waliokuwa na ndoto kubwa lakini mpaka sasa wameshindwa kutimiza ndoto zao ,na wamekata tamaa , serikali za vijiji hazioni thamani yao , na hata ndugu wanaosalia kusema wawasaidie watimize ndoto zao ni baadhi yao tu .

Je ni lini serikali itaingilia kati kuhakikisha inawashika mkono watu hawa?
Hbr za Leo. Kila Siku tunatangaza kuhusu kuimarisha mifumo ustawi na rufaa zake. Kila mwenye uhitaji wa huduma za ustawi pa kuanzia ni ofisi ya serikali ya mtaa wake ambapo, atakutana na Afisa Ustawi. Kama hayupo kwenye ngazi hiyo, anaenda kwa mkurugenzi wa Halmashauri au ofisi ya mkuu wa wilaya. Ngazi hizi nchi nzima wapo.

Anaona amekwama, kuna ngazi ya mkoa, kote wapo.

Huko Nako amekwama, kuna simu za wizara kituo cha huduma kwa wateja, namba 0734986503 au 026 2160250. Imeonekana huko Nako mtihani, na mm napokea rufaa ujumbe kwenye simu yangu 0765345777 au 0734124191, natoa ushauri na maelekezo nn kifanyike.

Haya sasa nianzie hapa, nani kakwama wapi tafadhali. Nitumie sms Ili nibaini zaidi shida Iko ngazi ipi ya mfumo.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Hongera Mhe. kwa kuaminiwa pia hongera kwa kutupa nafasi ya kutoa dukuduku letu.
mi hoja yangu inaweza kuwa tofauti kidogo , lakini utufikishie kwa Rais kwani wahusika hawataki kulishughulikia.
suala la watoto wa darasa la Nne kulazimishwa kwenda kukao Boarding kwa shule zilizosajiliwa kama DAY SCHOOLS, hii ni unyanyasaji na hili limefanyiwa utafit kwa nchi za ulaya.
nafahamu wapo ambao wanapenda lakini naomba lakini tunaojua na ambao tumepata matatizo kwa watoto wetu tunaombi dogo tu, tupewe haki yetu kama usajili wa shule ulivyo.
nyuma ya hili kuna rushwa kubwa saana kwa viongozi wa wizara ya elimu, wenye shule kwa umoja wanatoa rushwa kubwa. ndiyo maana tunaomba Rais aingilie kati.
Chukua namba zangu hapo juu unipatie sms ya mfano wa shule moja inayofanya ukorofi huo Ili nimpe waziri wa elimu mfano kamili tafadhali. Lakini elimu pia wanazo namba zao kwa kero zote za shule. Naweza kukupatia pia

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Chukua namba zangu hapo juu unipatie sms ya mfano wa shule moja inayofanya ukorofi huo Ili nimpe waziri wa elimu mfano kamili tafadhali. Lakini elimu pia wanazo namba zao kwa kero zote za shule. Naweza kukupatia pia

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Mhe. kwenye hili suala watu wa Wizara ya Elimu hawezi kushughulikia kwasababu ndo wanufaika wa hizo Rushwa kutoka kwa wamiliki wa shule.
kitu cha kwanza , ada ya mtoto anapoingia darasa la nne inaongezeka karibu 400% hivyo ni chanzo cha mapato na ili kulifumbia macho pesa inapelekwa kwa viongozi wa wizara ya Elimu.
japo mimi shida yangu sio gharama shida yangu Treatment ya watoto. Mhe Waziri embu fikiria mtoto wako wa miaka 8 yuko mbeya , Njombe au Iringa, afu wamelazimsha akae Boarding, mtota anaamshwa saa 10 aoge maji ya Baridi !! (just imagine) afu saa 11 asubuhi aingie darasani. (casually , watakuambia ooh , maji ya moto yapo- ni uongo tu) visiting day ndo wanaweka maji ya moto.
ndo maana kwa ukubwa wa nguvu iliyoko nyuma ya hili suala tunamuomba Mhe. Rais, Mama samai aingilie kati.
kuna nguvu kubwa inatumika nyuma ya hili suala.
 
Kwanza kabisa nipende kukupongeza wewe Mh.waziri Kwa kazi Yako nzuri ya kupigania maendeleo katika wizara hii nyeti Sana ya jinsia na maendeleo ya jamii. Niwe mkweli sijawahi kukufuatilia kama kipindi hiki na wakati ukiwa ktk wizara ya Elimu. You are one of the best leader we have in Tanzania, note that. Unaweza usijue ni Kwa kiasi gani watanzania wanakubali kazi Yako lakini jipime mwenyewe ktk kukamilisha malengo Yako na ya Taifa Kwa ujumla na mwisho Kila atakaye taka kuuliza atajibiwa na kazi zako.
Naomba Sasa nishauri kitu muhimu ambacho nadhani Kwa hekima na nafasi na upeo ulionao unaweza kutathmini Kwa mapana zaidi na kuona kama Lina tija katika jamii yetu au la.
Mimi kitaaluma ni mwalimu na Bado nipo kazini. Nimefanya kazi Kwa takribani miaka 15 Hadi Sasa. Nilichokibaini ni kuwa ktk Shule nyingi Sana hususani vijijini suala la gender violence ni tatizo kubwa kuliko linvyozungumziwa huko juu na viongozi au hata vyombo vya habari. Sehemu nyingi za vijijini matukio ya watoto kipata mimba na wazazi kumalizana na wahusika, au mimba kutolewa au watoto wenye mimba kutelekezwa ni maisha ya kawaida kabisa. Yaani ni kama kawaida na ukionekana unafuatilia ili kulichukulia hatua za kisheria utaishia ktk matatizo. Hapa Kuna msemo unasema nani atamfunga paka kengere?
Naomba nishauri haya yafuatayo ili kumlinda mtoto wa kitanzania
1. Kila Shule wanapoajiliwa walimu WA msingi na sekondari awepo pia afisa jinsia mmoja.
Kazi zake
A. Kufundisha maswala mtambuko ya kijinsia, Hali, na wajibu.
B. Kutoa taarifa Moja Kwa Moja Kwa wizara husika ya jinsia ikiwa atagundua hakuna usawa au Kuna ukiukwaji wa haki.
C. Kutathmini mahitaji ya jamii ktk kuteleleza usawa WA kijinsia
D. Kusimamia masuala ya Afya na usalama wa mwanafunzi shuleni na hata kufuatilia changamoto zinazoathiri ujifunzaji wa mwanafunzi.
2. Afisa jinsia awe anawajibika ktk ofisi ya waziri au Kwa naibu waziri wa jinsia na maendeleo ya jamii. Kwakufanya hivi itachochea haki na uwajibikaji wa watendaji wa SERIKALI za vijiji na wilaya. Na kwakuwa itakuwa ndiyo kazi yao jamii itakuwa na msemaji na muonaji WA karibu.
Mwisho napenda kumpongeza pia Mh. Rais wetu Dr. Samia Kwa kazi nzuri anayoifanya ktk nchi yetu. Nchi imetulia na maendeleo yanasonga mbele.
 
Ubarikiwe, nimepokea, maoni yako yana mashiko. Shukrani [emoji1431]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
 
Salaam Mheshimiwa!
Kwa ufupi mambo kadha! Kwanza ni Jina la Wizara yako. Tunamaanisha nini tunaposema "Jinsia"!!? Kama tunamaanisha Wanaume pekee yao, then ni sawa Wizara kutumia jina hilo, kama tunamaanisha Jinsia =Me &Ke, then kwanini tunasema "....Jinsia, Wanawake....." Hii "Jinsia" ni kitu gani hasa!!?

Pili ni kuhusu Matokeo ya Mitihani ya Darasa la Saba na Kidato cha nne 2023 na muktadha wake kwenye suala zima la "Jinsia" hapa kwetu. Nafahamu hili liko chini ya wizara ya elimu na pia Utawala Bora na ni rahisi kudhani halihusiani na wizara yako, lakini kwamba mara huu Wavulana wameonekana kufanya vizuri zaidi kwa umbali mkubwa kuliko wasichana katika jamii ambayo (in my opinion) imekanganyikiwa kati ya radical feminism na misogynism, linatoa dalili gani ya Ustawi wa Jamii ndani ya miaka 10 ijayo ambapo wanafunzi hawa watakuwa ndiyo workforce ya jamii yetu!!?

Tuanzie hapo!
 
Samahani kwa kuchelewa kuona hoja yako. Jinsia kwenye utekelezaji wetu ni dhana ya kupanga Kila mpango kwa jicho la kuweka mazingira wezeshi kwa shughuli za maendeleo zinazofanywa na wanawake na shughuli za maendeleo zinazofanywa na Wanaume. Mfano, kwenye Kila jamii, ziko shughuli ambazo inafahamika kabisa kuwa hizi hufanya wanawake mathalani, kutafuta Kuni za kupikia huku Afrika. Je mipango yetu kwenye bajeti ya serikali imetenga asilimia ngapi za fedha kwa ajili ya kuwezesha mfano upatikanaji wa Nishati mbadala Ili wanawake waachane na kwenda kutafuta Kuni porini ambako ndiko wanapoteza muda wa masomo, wanakatiliwa, na wakija kupika afya zinaharibika wakati huo huo kazi hiyo hawawezi kumtuma Mtoto wa kiume.

Usipotenga fedha vizuri eneo hili, unaendelea kudidimiza Jinsia ya kike kwenye maendeleo ya elimu na afya na kushindwa kuilinda dhidi ya ukatili.

Haya niishie kwanza hapa uje tuone kama tumeelewana au niendelee na mifano ya bajeti ambayo ina mizani ya usawa w kijinsia.

Shukrani. Kuuliza ni safi sana kwa uelewa wa pamoja. [emoji1431]

Hoja ya pili ya kuachana kwa matokeo ya ufaulu wa watoto wa kike na kiume pia ni mfano wa ukosefu wa usawa wa kijinsia kwenye mazingira ya kusoma. Kuna jambo limepungua kwenye mazingira ya Jinsia mojawapo hapo.

Matokeo ya baadae ni kuparaganyika kwa mzania wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii kwa kuwa, asiyeelimika huku anatakiwa Kulea Kizazi chake atakinyima tu stahiki za malezi Bora mfano labda; kwa mazingira ya Leo lishe Bora kwa watoto inaenda sambamba na uelewa na kukubali mtoto ale nini siku 1000 za kwanza na Hadi miaka 8 kipindi ambapo ubongo unakua hadi 90%, mtu ambaye hana elimu atagubikwa na ubishi, Imani potofu nk je unadhani haitakuwa na athari kwenye makuzi ya mtoto?

Karibu kwa mjadala.
Mjadala ni jambo jema sana ubarikiwe [emoji1431]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Sikia @ummymwalimu na nyie @nhiftz iko hivi mimi siwezi kufanya MVA kwa elfu 5 yaan nyie muibe hela za wachangiaji then mtupe sisi mzigo tumekubaliana tutakachokuwa tunakifanya ni kumuandikia mgonjwa akanunue vifaa vyote famasi saiz utakua na kadi yako na hela mfukoni lazima utoe.
 
Samahani kwa kuchelewa kuona hoja yako. Jinsia kwenye utekelezaji wetu ni dhana ya kupanga Kila mpango kwa jicho la kuweka mazingira wezeshi kwa shughuli za maendeleo zinazofanywa na wanawake na shughuli za maendeleo zinazofanywa na Wanaume. Mfano, kwenye Kila jamii, ziko shughuli ambazo inafahamika kabisa kuwa hizi hufanya wanawake mathalani, kutafuta Kuni za kupikia huku Afrika. Je mipango yetu kwenye bajeti ya serikali imetenga asilimia ngapi za fedha kwa ajili ya kuwezesha mfano upatikanaji wa Nishati mbadala Ili wanawake waachane na kwenda kutafuta Kuni porini ambako ndiko wanapoteza muda wa masomo, wanakatiliwa, na wakija kupika afya zinaharibika wakati huo huo kazi hiyo hawawezi kumtuma Mtoto wa kiume.

Usipotenga fedha vizuri eneo hili, unaendelea kudidimiza Jinsia ya kike kwenye maendeleo ya elimu na afya na kushindwa kuilinda dhidi ya ukatili.

Haya niishie kwanza hapa uje tuone kama tumeelewana au niendelee na mifano ya bajeti ambayo ina mizani ya usawa w kijinsia.

Shukrani. Kuuliza ni safi sana kwa uelewa wa pamoja. [emoji1431]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Sikia @ummymwalimu na nyie @nhiftz iko hivi mimi siwezi kufanya MVA kwa elfu 5 yaan nyie muibe hela za wachangiaji then mtupe sisi mzigo tumekubaliana tutakachokuwa tunakifanya ni kumuandikia mgonjwa akanunue vifaa vyote famasi saiz utakua na kadi yako na hela mfukoni lazima utoe
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Hongera sana mama kwa kuweka jukwa hili! Hii ni ishara nzuri kwamba unawajibika vyema kwa watanzania!

Naamini masuala ya kufungua NGOs yapo chini ya wizara yako kama sikosei, nikijua hilo basi nitakuekeza machache yanayotukera. Asante
 
Watanzania wazee wanakufa ,waanateseka mitaani hakuna huduma za afya ,wazee hawana pesa za matibabu .

Viongozi mpo ty .
 
Hongera sana mama kwa kuweka jukwa hili! Hii ni ishara nzuri kwamba unawajibika vyema kwa watanzania!

Naamini masuala ya kufungua NGOs yapo chini ya wizara yako kama sikosei, nikijua hilo basi nitakuekeza machache yanayotukera. Asante
Hbr za asubuhi. Karibu eleza tafadhali

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mama Dkt. Gwajima D Tafadhali huduma za IVF zifikiriwe ziwemo kwenye kitita kikubwa cha bima ya afya, gharama za IVF ni kubwa na zinatesa. Kwa sasa ukienda kv Dar IVF bima kubwa haipati kibali utazungushwa hadi ukome. We need your intervention. Kukosa mtoto ilhali technology inaweza kusolve na means za bima zipo inatesa sana nafsi Mheshimiwa...Tafadhali liwekeni Sawa hili suala na Wizara ya Afya.
 
Samahani kwa kuchelewa kuona hoja yako. Jinsia kwenye utekelezaji wetu ni dhana ya kupanga Kila mpango kwa jicho la kuweka mazingira wezeshi kwa shughuli za maendeleo zinazofanywa na wanawake na shughuli za maendeleo zinazofanywa na Wanaume. Mfano, kwenye Kila jamii, ziko shughuli ambazo inafahamika kabisa kuwa hizi hufanya wanawake mathalani, kutafuta Kuni za kupikia huku Afrika. Je mipango yetu kwenye bajeti ya serikali imetenga asilimia ngapi za fedha kwa ajili ya kuwezesha mfano upatikanaji wa Nishati mbadala Ili wanawake waachane na kwenda kutafuta Kuni porini ambako ndiko wanapoteza muda wa masomo, wanakatiliwa, na wakija kupika afya zinaharibika wakati huo huo kazi hiyo hawawezi kumtuma Mtoto wa kiume.

Usipotenga fedha vizuri eneo hili, unaendelea kudidimiza Jinsia ya kike kwenye maendeleo ya elimu na afya na kushindwa kuilinda dhidi ya ukatili.

Haya niishie kwanza hapa uje tuone kama tumeelewana au niendelee na mifano ya bajeti ambayo ina mizani ya usawa w kijinsia.

Shukrani. Kuuliza ni safi sana kwa uelewa wa pamoja. [emoji1431]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Nina maoni tofauti kuhusu dhana ya "kazi za kiume na kike" katika jamii kama nilivyo na maoni binafsi kuhusu kile kiitwacho "juhudi za kumkomboa Mwanamke" lakini hili haikuwa hoja yangu hapa, hoja ni "KAMA NENO JINSIA LINAWAKILISHA ME NA KE, KWANINI BADO KUWEKA UPENDELEO MAALUMU KWA KUTAJA JINSI MOJA YA KE!? MQNTIKI YAKE NINI!?

Nadhani tunapotoka tunapotafuta usawa kati ya jinsi badala ya kutafuta usawa kati ya watu. Wakati notion kama "Sehemu kubwa ya mali inamilikiwa na wanaume kuliko wanawake" na hivyo tukaanza kutafuta namna ya kuondoa hilo bila kuzingatia maeneo mengine ya kidemografia kwenye jambo hili kama "Sehemu kubwa ya utajiri wa dunia inamilikiwa na si zaidi ya watu mia duniani, na si zaidi ya familia 10 duniani, na kwa zaidi ya asilimia 90 na watu weupe na kadhalika..." Au kwamba "idadi kubwa ya watu wote walioko jela ni wanaume, Sehemu kubwa ya watoto wanaokufa chini ya umri wa miaka mitano ni wa kiume, Sehemu kubwa ya watu wanaojiua ni wanaume, Sehemu kubwa ya askari wanaokufa vitani ni wanaume na kadhalika....", Tunakuwa tumeruhusu toxic feminism kuathiri sera zetu huenda kwa matakwa ya wafadhili wetu na hivyo huenda tunaharibu jamii zetu tukidhani tunazifanya za kisasa.
 
Heshima yako mheshimiwa Dr gwajima,
Nina tatizo linalohusiana na migogoro ya ndoa na haki za watoto baada ya ndoa kusambaratika,mke wangu aliondoka nyumbani mwezi juni2019 baada ya kutoa ujauzito aliokuwa kapachikwa na hawara yake,baada ya kujua kuwa nishajua kuwa katoa mimba na kuanza taratibu za vikao vya kufamilia kuhusiana na ujauzito huo ndo akaondoka mwnyw nyumbani huku kuniachia watoto wa4 wa mwisho akiwa umri wa miaka2 wakati huo.
Ndg zake hawakutaka kunipa ushirikiano hivyo nikawajulisha ndg zangu,nikaenda kituo cha polisi kitunda dawati la jinsia nikaambiwa atarudi tu.
Ghafla akaibuka na barua ya wito ya kituo cha polisi staki shari ukonga kwa madai kuwa nilitaka kumkata na panga ndio maana akaondoka nyumbani lakini akakosa ushahidi.
Akafungua shauri bakwata kata akashindwa kesi,akaenda wilaya ilala akashindwa keshi,akaenda kwa kadhi mkoa Dsm nako akaonekana ana makosa hivyo jambo hilo lijadiliwe kifamilia.
Akahamia ustawi wa jamii manispaa ya ilala ,
pale Nikaamriwa nikabidhi watoto wote kwa mama,nikamjibu siwezi kukabidhi watoto kwa sababu kwanza ndoa haijavunjika,pili shauri lipo kwa kadhi na katoa hukumu ambayo mke anatakiwa kutekeleza,
Pale nikaonekana mm ni mkorofi najifanya najua taratibu mke akasema nikimkabidhi watoto hatonidai chochote nikahitaji maandishi ya kisheria ili nisijeonekana nimetelekeza watoto,hapo ndo nikawa nimewasha moto,nikaambiwa tutakushughulikia mahakamani na utaijua nguvu ya wanawake.
Kesi ikapelekwa juvenile kisutu,lakini yaliyonikuta huko mungu mwenyewe anajua,mwisho wa siku nikapewa tuhuma kuwa nawatesa watoto nawanyima chakula yaani kila aina ya tuhuma ili mradi ninyanganywe watoto,hukumu ilivyotoka ikaamuru Mama apewe watoto,je mheshimiwa mimi kama baba sina haki ya kushiriki malezi ya watoto?au hawa ustawi wa jamii wapo kuwatetea wanawake hata kama mama ana makosa na wanaume hatuna haki maana ni mpaka mahakamani naambiwa hii ni gender issue kweli mheshimiwa?
Umri wa wa watoto ni miaka13 hao ni mapacha,miaka 10 na miaka 7,je mimi kama mzazi (baba) sina haki ya kulea watoto na kuwapatia haki za msingi?
Nakuomba mheshimiwa waziri Dr Dorothy Gwajima uliangalie jambo hili kwa makini kwa mstakabali wa makuzi ya watoto na haki zao kwa ujumla.
Natanguliza shukrani.
 
Ndugu yangu salaam. Awali ya yote pole Sana kwa kadhia hii. Pia hongera Sana kwa hekima, utulivu na ujasiri wa kuleta hoja yako hii. Haya kesho nitumie ujumbe kwenye sms namba 0765345777 nitaweza kuisoma na kukupa ushauri. Haya usiku mwema. Shukrani

Back
Top Bottom