Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Hakuna watu nawaonaga mapimbi kama watuma salamu redion πŸ˜‚πŸ˜‚ chesco mzee wa matunda na manka mushi
bila kumsahau mzee lawena msonda maana mi namsikiaka tangu nipo mtoto.. πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Izzo b
Emmanuel simwinga
Mbozi sec then southern highland (form four-2005)
Alikaa iromba
Until alihamia dar
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Am not sure this is true but
Roma kasoma pcm pale old moshi then akafukuzwa kulikua n mgomo nadhan was 2006 au 2005,yeye na karibia hlf ya darasa wakapelekwa shule inaitwa magamba(ilikua chuo) sijajua hii isagara amesoma lini nbut sidhan pia kama ni busraa kukubishia
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abbot hakua na umaarudu wowote mbeya
Labda pandahill
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] dmx ulikuwa wamfahamu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani kama atakuwa anamkumbuka. DMX alianza form 1 mwaka 2003, 2004 form 2 akafeli, akarudia, tukasoma naye, then tukamaliza naye 2007, kwahiyo badala ya kumaliza form 4 mwaka 2006 akamaliza 2007. Kijana alikuwa mkorofi sana. Generation ya azania kutoka 2001 mpaka 2007, ilikuwa na watu maarufu kama wakina Zinde, Mpeta Bizzo, Reddish Brown, Kipande shebby, Kisamo (Msanii), G sparker, Dogo Tifu, Michael Jonhson Nguli (mchambuzi wa michezo Azam), Kuna mtu anaitwa Popo, BMB na wengine kibao wazee wa kitengo mawe.
 
Lebo ya kijani..tumemaliza mwaka mmoja ila nilikuwa jirani yako..ila dmx alivyofeli form2 kidogo alipunguza utata..unakumbuka sekeseke la kuwapiga makonda baada ya kufariki yule dogo wa form1..sijui tulikuwa form 3 vile au form..sikumbuki vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani tulikuwa form 3. Yes ni kweli kijana alipofeli form 2 alipunguza utata kidogo mana jina lilikuwa kubwa mwili mdogo.
 
wewe nzovwe,kalobe au halengo unatokea
 
Wengine tumesona na Kinjekitile Ngwale enzi za vita vya MajiMaji.

For real ninesoma na Diplomatz na Y Thang wa Kwanza Unit Tambaza.


Sent using Jamii Forums mobile app
Teh! teh! wazee wa Tamba Clan. Mkuu kiranga kwenye ule uzi wa vurugu za tambaza, ulipokuwa unamuelezea Puza fala ulinikumbusha mbali sana. Nakumbuka ilikuwa mwaka 1993 au 1994 hivi nilikuwa na miaka kama 6 hivi, baada ya kutokea zile vurugu kuna mwanafunzi mmoja wa Tamba Boys alikimbizwa na polisi akaja akakimbilia kwa dada yake maeneo ya ilala. Akaingia ndani akajifungia akajificha juu ya dali. Basi wazee walikuja wakavunja mlango wakampandia huko huko wakaondoka naye. Nikikumbuka huwa nacheka sana.
 
Tulikuwa na fujo sana.

Sasa hivi watu madaktari, mainjinia, wachungaji, watu wa familia...

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…