Pale Morogoro Sec Sch kulikuwa na eneo maalum la kupaki Baiskeli za wanafunzi miaka hiyo. Enzi hizo Mji wa Morogoro ulikuwa na dala dala moja tu... lilikuwa basi moja tu la Mzee Chambo... na route ilikuwa ni Kihonda - Mjini. Kwa changamoto za usafiri, wazazi wengi waliwamilikisha Baiskeli watoto wao.
Miongoni mwetu wanafunzi wa Moro Sec tulikuwa na tabia, ukiwa na kijisafari chako cha fasta unamtafuta mwana mwenye Baiskeli.... Unamuazima.... kuepusha usumbufu huu... ilikuwa unaenda PARKING unaangalia Baiskeli isiyo na lock... unasepa kisha unairudisha kimya kimya kabla muda wa masomo haujaisha!
Hiki ni kipindi SQUEEZER alishaanza mziki na Mshkaji wake anaitwa Isaac .... (huyu Isaac sintamzungumzia). Squeezer alichukua Baiskeli ya Mwanafunzi mmoja mdada... yule mdada alikuwa mpole sana .... na Baiskeli yake ilikuwa nzuri tu... Squeezer aliichukua Baiskeli ile kwa dhamira akapige mishe zake kisha arudi shuleni!
Mambo yakawa mengi.... Squeezer hakuweza kuwahi kurudi shule katika muda kabla ya masomo kuisha.... bint mwenye baiskeli yake alikuwa ameingia shift ya mchana (Moro Sec kulikuwa na shift enzi hizo, sijui sasa) ambao wanatoka saa 12 jioni.... bint katafuta Baiskeli mpaka Kiza... hola.... huku na huko .... baiskeli haionekani! Basi mwishowe wanafunzi wenzie wakamshauri aripot kwa walimu wachache waliopo kuwa 'kaibiwa baiskeli yake'.
Kuibiwa Baiskeli ndani ya shule lilikuwa ni tukio kubwa sana na si la kawaida.... mara chache sana kutokea.... So kwa kuwa ilikuwa jioni na kiza kishatanda, basi bint yule (F1 au F2, Squeezer alikuwa F3) ilibidi arudi home na wenzie kwa Miguu. Balaa ilikuwa asubuhi iliofuata.... kilinuka shule nzima.... bahati mbaya sana.... ktk main suspects... kura ikanidondokea mimi ...... sijawahi kujua mpk leo why (ukiacha utundu, sijawahi kuwa na records za matukio)!
Kwa kuwa kimeshanuka.... shule nzima walijua kwamba kuna baiskeli imeibwa.... na alieba baiskeli ni (niite Thom).... I see.... nilikuwa na wakati mgumu sana ..... kwanza ndio tunaelekea mwishoni mwa F4...... pia msala wa aina ile sio msala mdogo....nilijua hapa Polisi inanihusu.... tatu, nilikuwa sina namna yyt financially ya kulimaliza lile soo, ukijumlisha na aibu ya kujulikana shule nzima kuwa Thom ni kibaka...
wakati seke seke limepamba moto na tayari Mkuu wa Shule kashatuma watu, niitwe kwa Mahojiano ..... ndio akajitokeza Squeezer na kunipa full story kuhusu Baiskeli, na ukweli kwamba Baiskeli haijaibwa wala nini... Baiskeli alienda kupiga nayo mishe na akairudisha very late.... ipo safi kabisa.... na baiskeli iko chini ya mikono salama ya Mlinzi wa shule.... ambapo Mlinzi mwenyewe anakuja Shuleni kwenye lindo jioni kuanzia saa 12... lakini Mlinzi alimuambia Mwl mmoja tu kuwa Baiskeli ipo... yule Mwl hakuwepo wkt wa seke seke...
To shorten the story.... Squeezer alinipanga nipambane kivyangu mpk mwisho lkn endapo Maji yatazidi Unga, nimtose kwa kumtaja yeye.... amalizie Msala ili kuniokoa mimi .... pia nisalimike na kuwa ktk nafasi nzuri ya kumaliza F4 na kufanya ''pepa'' .... Mungu sio John.... niliumaliza ule msala bila kumtaja Squeezer, mwenye Baiskeli yake akakabidhiwa na mm shule ikaisha salama...!