Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,203
- 37,906
Umesoma nae wapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umesoma nae wapi?
Tanga School = Tanga Technical? Basi mimi nlisoma nae A level
Yes ni Tanga tech. Umesoma nae Ununio?Tanga School = Tanga Technical? Basi mimi nlisoma nae A level
Tena Mazengo sekondari na wakaacha machata yao mule.
Nimesoma na Mheshimiwa Sugu shule ya Msingi Ligula,Mtwara.
Tukiwa darasa la pili tulikaa dawati moja na alikuwa ni rafiki yangu sana,tukitoka darasani muda wa saa tano tunakwenda nyumbani kwetu Ligula B tunachota korosho kwenye debe(korosho first grade za kutoka kiwanda cha korosho Likombe ambazo huwa zinauzwa nje ya nchi) tunaweka kwenye mifuko ya kaptura tunakula baadae anakwenda nyumbani kwao kiyangu.
Alikuwa anajulikana kwa jina la Joel.
yes
Hlf sijui kwanini shuleni waislamu huwa hawapendi kuingia kwenye vipindi vyao vya dini
Hata shuleni kwetu wengi walikuwa wanaingia kwenye darasa la dini la kikristo,mpk shehe anashtaki kwa walimu
Sent using Jamii Forums mobile app
Umenikumbusha mbali sana.Pale Morogoro Sec Sch kulikuwa na eneo maalum la kupaki Baiskeli za wanafunzi miaka hiyo. Enzi hizo Mji wa Morogoro ulikuwa na dala dala moja tu... lilikuwa basi moja tu la Mzee Chambo... na route ilikuwa ni Kihonda - Mjini. Kwa changamoto za usafiri, wazazi wengi waliwamilikisha Baiskeli watoto wao.
Miongoni mwetu wanafunzi wa Moro Sec tulikuwa na tabia, ukiwa na kijisafari chako cha fasta unamtafuta mwana mwenye Baiskeli.... Unamuazima.... kuepusha usumbufu huu... ilikuwa unaenda PARKING unaangalia Baiskeli isiyo na lock... unasepa kisha unairudisha kimya kimya kabla muda wa masomo haujaisha!
Hiki ni kipindi SQUEEZER alishaanza mziki na Mshkaji wake anaitwa Isaac .... (huyu Isaac sintamzungumzia). Squeezer alichukua Baiskeli ya Mwanafunzi mmoja mdada... yule mdada alikuwa mpole sana .... na Baiskeli yake ilikuwa nzuri tu... Squeezer aliichukua Baiskeli ile kwa dhamira akapige mishe zake kisha arudi shuleni!
Mambo yakawa mengi.... Squeezer hakuweza kuwahi kurudi shule katika muda kabla ya masomo kuisha.... bint mwenye baiskeli yake alikuwa ameingia shift ya mchana (Moro Sec kulikuwa na shift enzi hizo, sijui sasa) ambao wanatoka saa 12 jioni.... bint katafuta Baiskeli mpaka Kiza... hola.... huku na huko .... baiskeli haionekani! Basi mwishowe wanafunzi wenzie wakamshauri aripot kwa walimu wachache waliopo kuwa 'kaibiwa baiskeli yake'.
Kuibiwa Baiskeli ndani ya shule lilikuwa ni tukio kubwa sana na si la kawaida.... mara chache sana kutokea.... So kwa kuwa ilikuwa jioni na kiza kishatanda, basi bint yule (F1 au F2, Squeezer alikuwa F3) ilibidi arudi home na wenzie kwa Miguu. Balaa ilikuwa asubuhi iliofuata.... kilinuka shule nzima.... bahati mbaya sana.... ktk main suspects... kura ikanidondokea mimi ...... sijawahi kujua mpk leo why (ukiacha utundu, sijawahi kuwa na records za matukio)!
Kwa kuwa kimeshanuka.... shule nzima walijua kwamba kuna baiskeli imeibwa.... na alieba baiskeli ni (niite Thom).... I see.... nilikuwa na wakati mgumu sana ..... kwanza ndio tunaelekea mwishoni mwa F4...... pia msala wa aina ile sio msala mdogo....nilijua hapa Polisi inanihusu.... tatu, nilikuwa sina namna yyt financially ya kulimaliza lile soo, ukijumlisha na aibu ya kujulikana shule nzima kuwa Thom ni kibaka...
wakati seke seke limepamba moto na tayari Mkuu wa Shule kashatuma watu, niitwe kwa Mahojiano ..... ndio akajitokeza Squeezer na kunipa full story kuhusu Baiskeli, na ukweli kwamba Baiskeli haijaibwa wala nini... Baiskeli alienda kupiga nayo mishe na akairudisha very late.... ipo safi kabisa.... na baiskeli iko chini ya mikono salama ya Mlinzi wa shule.... ambapo Mlinzi mwenyewe anakuja Shuleni kwenye lindo jioni kuanzia saa 12... lakini Mlinzi alimuambia Mwl mmoja tu kuwa Baiskeli ipo... yule Mwl hakuwepo wkt wa seke seke...
To shorten the story.... Squeezer alinipanga nipambane kivyangu mpk mwisho lkn endapo Maji yatazidi Unga, nimtose kwa kumtaja yeye.... amalizie Msala ili kuniokoa mimi .... pia nisalimike na kuwa ktk nafasi nzuri ya kumaliza F4 na kufanya ''pepa'' .... Mungu sio John.... niliumaliza ule msala bila kumtaja Squeezer, mwenye Baiskeli yake akakabidhiwa na mm shule ikaisha salama...!
Mwaka gan hiyo babuNimesoma na comedian TR PAUL advanced level KAHORORO HIGH SCHOOL BUKOBA ,alikuwa anasoma EGM mie PCM ,kiuweli jamaa alikuwa comic sn hasa tulikuwa tunakutana kwenye kipindi cha PURE mathematics na GS,View attachment 1393399
Sent using Jamii Forums mobile app
Alaaaah ina maana huyu. Jemes delicious na umber rutty hawajasoma na mtu yoyote humu JF wacha niendele kusoma comment bac.Uzuri wa huu uzi ukidanganya lazima uumbuke [emoji23]. Kama hujasoma na cellebrity tulia tu.
Sent using Jamii Forums mobile app