Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

1. Bushoke tumecheza nae sana mpira makole pale, yeye alikua anadaka
2.voice wonder tulikua tukakutana kwenye mechi za kitaa, makole vs airport uwanja wa shule ya msingi makole. Mpira wa makaratas yan sembo.
3. Mswaki producer, huyu bwana mdogo alikua anakuja sana coco record studio ya kwanza pale Dodoma. Tulikua tunafanyia kazi kigamboni Karibu na magorofa mengi. Dogo hakua producer alikua msanii tena anaiga sauti ya ngwair sikuwahi kudhan anaweza kufika mbali
4.Moni central zone nilimkuta Dom sec, Mimi nikiwa nafundisha jioni darasa la watu wazima. Siku moja Moni alinifata na kunifananisha na producer flan wa pale pale Dom makole. Bahati nzuri yule producer nilishafanya nae kazi coco record hivyo nikamuunganisha nae.

Watu wengi maarufu hawana tabia ya kuringa ila watu wana inferiority complex juu yao. Unakuta mtu akipitwa bila kusalimiwa anasema jamaa anaringa wakati mtaani watu kibao wanampita bila kusalimia na hakuna shida. Mnapishana husalimii ukitegemea Kama atakusalimia, akiuchuna lawama tayar.

Sent using Jamii Forums mobile app

wabongo pia hua tuna tabia ya kupangiana jinsi ya kuishi
kwa mfano mimi ni mtu mkimya, na muda mwingi kichwani nina matatizo yangu, najikuta mkimya na sisalimii watu sometime ,hii huwafanya watu kusema nalinga


Sent using Jamii Forums mobile app
 
2010 hiyo

Diamond na mwenzie bob junior nawadai hela yangu sh 600 niliwakopesha mayai mawili.walikuwa wateja zangu kila siku nikiwakuta nje pale sharobaro rekod mogomeni mapipa lazima wanunue au wakope kesho yake walipe sas kuna siku nimewakut nje walikuw watatu wakala mayai mnne kila mtu halafu mond na bob wakaomba niwakopeshe moja moja kila mtu watanilipa siku nikiwakuta ..

basi sijalipwa hadi leo hii kila siku naambiwa dogo mpole hela yako kesho mdogo wetu ila wananunua basi ikawa.. kesho kesho kesho had nikakata tamaa ila sijasamehe 600 yangu boss wangu alinisema sana
kwanini haujashtaki mkuu
 
kipnd chetu mlokoz ndo alikua jau sn

Nakumbuka Mlokoz alikuwa na Teacher mmoja anaitwa Lutwaza, ana tumbo kubwa hivi, dah hawa jamaa walitufanya tuishie mchikichini aisee yaan ukichelewa tu, ni shidaa, zinapigwa fimbo kama anauliwa nyoka. Ila kutoka miaka ya 90 kuja 2000 mwanzoni, Teacher mtata alikuwa Mchwa, dah! huyu kila aliyesoma Azania miaka ya 90 kuja 2000 huwa anamkumbuka
 
Nimesoma na jamaa mmoja jina la kistaa nicolyner alikuwa social prefect mzumbe sec Ila bdo hajatoka kimziki ila kuna dogo anajiita jozzination anaimba nyaturu trap atatoka mda sio mrefu mtamsikia kwa hewa akitamba.
 
Barnaba ila Acha kudanganya uma kuwa ulifika sec tena siku ya mtihani wa Taifa ukatoroka ili kwendavkufanya odition THT, niongo wapo wanaokujua ambao ulisoma nao mkwawa Premary kigogo
Wanasema shule yenyewe uliacha Kati hukumaliza ndg
Ila Ruge alikupika na akakupanga ukiwa maarufu sema hivi kuhusu Elimu yako ili kulinda heshima

Wasanii acheni uongo kuhusu Elimu zenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami nichangie huu Uzi! Shule ya msingi nimesoma na Happy Magese ( aliwahi kuwa miss Tz) Shule inaitwa Kiwandani kule Mtibwa, alinizidi madarasa 5 ! Alikuwa anacheza sana Netball! Sekondari - Mafinga sec siku hizi inaitwa JJ Mungai nilisoma na Rashidi Abdala Makwilo a.k.a Chidi benz mtoto wa Ilala! Pia mkuu wa wilaya ya Kinondoni Daniel Chongole tulikuwa nae Mafinga sec!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngozye ukikaa vibaya unakula bonge la mkofi!!

5 PCM mwanangu mashola kakutana mlangoni na ngozie, akala bonge la mkofi! Dk 2 shavu loote alama ya mkono.
Oy kaveli mwanao mashola yuko wapi skuizi ..kitambo sana
 
Back
Top Bottom