Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Nimesoma shule moja Tausi (yule muigizaji mfupi) ana pacha wake anaitwa Rose Mdegera. Mkorofi ni sijawahi kuona.

Sec mi nikiwa primary mshua anafundisha Tosamaganga basi nakaa kota alikua anasoma mdogo wake Prof J Black Rhyno alikua anaimba sana kwenye graduu
pacha wake nae mfupi?
 
Niliisoma primary na bwana mdogo anaitwa moshi katemi pale Isenga primary mwanza,,,kipindi icho nilikua naimba rap nilikua nakubalika kinoma,,,,nakumbuka niliushangaza umati siku ya kuhitimu nilivonata na biti kwenye mziki mkubwaaa na sikuwahi ifanyia mazoezi biti amabayo watu waliikalia chimbo miezi ili waje kufunika.

Washkaji hawakuamini kwa umahili niliouonesha walidhani niliwaibia kitambo kumbe walaaa.
Kipindi hicho moshi katemi (Mo-MUSIC) alikua shabiki yangu,,,leo hii mi ndo shabiki na mziki nlitupa kuleee nikapendana na shule ya medicine ndo nmezamia huko mazima
Medicine inaharibu sana vipaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwayu huyo mdogo wangu, enzi hizo single digits za ilikuwa kitu Cha kawaida.

Nadhani atakuwa anamzunguzia Donald Chavilla alikuja baada ya kuondoka Kwayu mwaka 2005 mwishoni. Huyu Chavilla hakukaa sana, alivyoondoka Chavilla ndiyo akaja Ngozye, lakini kabla ya Ngozye kuwa Head kuna madam anaitwa Ngoda aliwahi kukaimu hiyo nafasi
 
Kwayu huyo mdogo wangu, enzi hizo single digits za ilikuwa kitu Cha kawaida.
Sent using Jamii Forums mobile app

Enzi za Kwayu na Chavilla, zero zilikuwa chache sana, unakuta division 1 ziko 100 au 90. Yaani ukiwa miongoni mwa waliopata zero shule nzima inajua flani kapata zero. Kuna jamaa alimaliza 2003 tulikuwa tunaishi naye kitaa, jamaa alizungusha pale azania, yaani mtaa mzima ulijua na shule nzima ilijua. Zero zilikuwa chache mno.
 
mw
Nimesona na ROMA mkatoloki pale USAGARA SEC wakati huo yeye ni basketballer anaetegemewa na shule huku mm ndo mwanamuziki bora zaidi pale.
Nakumbuka alikuwa anakuja kunipa ushauri akiwa na ANTONIO NUGAZ huyu wa Clouds (msemaji wa YANGA)
Jamaa walikuw wananikubali sana japo kuwa walinitangulia kidogo ila walinitambua mchango wangu.

Hata ile ngoma ya Roma (TANZANIA ) tumeplay kwa first time mahome SAHARE SEPOCHO 1

Ila chukushangaza wenzangu wametoboa mimi kibarua changu KUBET

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanza au?
 
Back
Top Bottom