Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Tena Mazengo sekondari na wakaacha machata yao mule.

Albert Mangwea - RIP
Moses Bushagama (MEZ B) - RIP
Haji Nura.
Athumani Kabongo (Dark Master)

Mangwea.
Jamaa mpole na mkimya sana. Alikuwa anapenda Basket Ball na alikuwa fundi wa ku dunk na ku score 3 points. UMISETA kitaifa Mwanza mwaka 2000 ndio alikuwa best Basket Baller na aliipa sifa kemkem Mazengo secondary hadi shule kupewa zawadi ya Computer achilia mbali zawadi zake.
Alikuwa si wa kuhudhuria sana class hasa alivyofika form III muda mwingi nje ya class akikariri mashairi. Nimewahi mshuhudia akikariri mashairi ya Vulindela (Brendah Fassie) huku anaehakikisha anaimba sahihi jamaa mmoja alikuwa anaitwa Jose by then alikuwa namba 1 goalkeeper wa Mazengo.

MEZ B.
Toz fulani na mtoto wa kishua enzi hizo. Anatembea kwa mwendo wa mdundo Alikuwa Day schooler. Alikuwa anapenda sana Basket Ball ila mkali wao alikuwa Mangwea. Mez B alikuwa hajionyeshi kama anaimba but alipoibukia hata sijui.

Haji Nura.
Anaenda Mazengo 1998 as one of the best student wa mkoa wa Shinyanga kwa waliomaliza la 7 1997. Alikuwa na akili sana class but muda mwingi aliwekeza kwenye muziki. Nakumbuka kuna siku tukiwa form II tulipishana nae maeneo ya History Block nikiwa naimba baadhi ya mashairi ya Do for love (2PAC) basi akawa amependa sana na kuniuliza ahhh kumbe wewe ni mdau but kiukweli sikuwa that deep. Of course jamaa alikuwa na kipaji maana katumbuiza sana kule Makole Club la Aziz enzi hizo. Nakumbuka alikuwa anaimba Wimbo fulani wa kuji introduce kuwa "nasoma mazengo, kidato cha tatu" ila hapa anaiga wimbo wa Sisqo wa Thong Song (Ukiusikiliza utaelewa). Jamaa alikuwa anaweza.

Dark Master.
Dah! Nikiwa form 1 yeye Form 4. Walikuwa wakorofi sana hasa kwenye room yao pale bweni la Mwenge. Yeye anakaa room number 1 up na mimi number 4 up. Waliosoma Mazengo hapa wananielewa vizuri. Siku moja ilikuwa jumamosi jamaa wamekula ugali na samaki mkavu then wamechafua room sana. Dark Master anakuja room kwetu ananiita wewe form 1 njoo hapa kufika room ananiambia safisha room iwe safi huku wamekula wao. Nikaanza kugoma jamaa akanikaba na kunibamiza dirishani ananiuliza unasafisha husafishi ilibidi nijitetee nasafisha ngoja nikachukue ufagio. Alivyoniruhusu ikabidi nitoke nje ya bweni maana mlango ulikuwa karibu na chumba chao. Jamaa ananifuatilia nimefika chini tayari nikamwambia naenda kwa head master (Enzi hizo Msasa anatisha hatari) kukusemea maana unanionea. Jamaa ilibidi aombe msamaha kwakuwa walikuwa wanamfahamu alivyo huyo Mkuu wa Shule.
Kwa ufupi jamaa alikuwa mkorofi kulingana na company yake maana walikuwa ni watu wa kitu cha Arusha.

Upande Mwingine.
Nimesoma na Nick Mbishi but mie nikiwa Bachelor yeye Diploma. Sina story za huyu dogo lakini alikuwa ni mtu wa kuimba mengi kuhusu chuo na kuhamasisha mambo mazuri hasa kwa wanafunzi.

Asanteni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu standard seven drop out anaweza kutunga mistari kweli?
Barnaba ila Acha kudanganya uma kuwa ulifika sec tena siku ya mtihani wa Taifa ukatoroka ili kwendavkufanya odition THT, niongo wapo wanaokujua ambao ulisoma nao mkwawa Premary kigogo
Wanasema shule yenyewe uliacha Kati hukumaliza ndg
Ila Ruge alikupika na akakupanga ukiwa maarufu sema hivi kuhusu Elimu yako ili kulinda heshima

Wasanii acheni uongo kuhusu Elimu zenu.

Sent using Jamii Forums mobile app

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Msanii Zola d mwili nyumba zamani alikuwa rafiki yangu wa kalamu, enzi hizo, kuwasiliana sana alinikaribisha kwake, na pia manwater kabla ya kujulikana nafahamiana naye, zamani nilipenda niwe star wa mziki, afande sele nimemjua tayar star., kishule nilisoma na mdogo wa Oten.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekaa na wolper kitaa kimoja Knyama Alimaua enzi hizo kabla hajawa staa, Alikiba alikua anakuja kujilia vyake karibu kila siku dah! Enzi hizo walper alikua anajiweka kitom boy tom boy.
Wakati anauza vitu vya promosheni, au anajifunza ufundi chereani jina bado hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma na Mheshimiwa Sugu shule ya Msingi Ligula,Mtwara.

Tukiwa darasa la pili tulikaa dawati moja na alikuwa ni rafiki yangu sana,tukitoka darasani muda wa saa tano tunakwenda nyumbani kwetu Ligula B tunachota korosho kwenye debe(korosho first grade za kutoka kiwanda cha korosho Likombe ambazo huwa zinauzwa nje ya nchi) tunaweka kwenye mifuko ya kaptura tunakula baadae anakwenda nyumbani kwao kiyangu.

Alikuwa anajulikana kwa jina la Joel.
Sugu maarufu kwa jina la May,kiyangu alikua anakaa kwa mama ake mdogo au shangazi yake Mama Rungu,Sugu msela kitambo sana tangu yuko mdogo halaf always alikua na dream kubwa kuliko umri wake
 
Sijasoma nao, ila wengi tunafahamiana kabla ya wao kua maarufu na hata sasa...



Cc: mahondaw
 
Adam mchomvu - akiwa fala pale mbeya fm. Anajiita tall wa ajabu katufanyiaga za kutosha, mc kwenye mashindano ya underground kupiga story ilikuwa sana.

Izzo B, tangu yupo sangu tunakesha studiobeya rekods, anarekod wimbo wake wa kwanza "pisha nipite" analeta geto tusikilize, huku tunakula mjani

Dumelang
 
Adam mchomvu - akiwa fala pale mbeya fm. Anajiita tall wa ajabu katufanyiaga za kutosha, mc kwenye mashindano ya underground kupiga story ilikuwa sana.

Izzo B, tangu yupo sangu tunakesha studiobeya rekods, anarekod wimbo wake wa kwanza "pisha nipite" analeta geto tusikilize, huku tunakula mjani

Dumelang
Underground acha tu, kuzaraulika, mi sina hamu, nimekata tamaa wakat water kaniita anisaidie, nyege zote ziliniisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami nichangie huu Uzi! Shule ya msingi nimesoma na Happy Magese ( aliwahi kuwa miss Tz) Shule inaitwa Kiwandani kule Mtibwa, alinizidi madarasa 5 ! Alikuwa anacheza sana Netball! Sekondari - Mafinga sec siku hizi inaitwa JJ Mungai nilisoma na Rashidi Abdala Makwilo a.k.a Chidi benz mtoto wa Ilala! Pia mkuu wa wilaya ya Kinondoni Daniel Chongole tulikuwa nae Mafinga sec!

Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha ya chidibenz yalikuaje kipindi hiko

One love
 
Kapiga sana, enzi hizo wolper ni mzuri hanuki mdomo tofauti na sahiv kawa waajabu mpk ananuka mdomo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umeajuaje mzee

One love
 
Maisha ya chidibenz yalikuaje kipindi hiko

One love
Jamaa alikuwa mpole sana huwezi amini na kauzembe fulan hivi alikuwa nako! Sema mambo ya kuimba na kurap yeye na wenzie waliokuwa wanatokea Dar walipenda sana! Kitambo sana miaka ya 2000 mwanzoni hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu standard seven drop out anaweza kutunga mistari kweli?

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
Asa sii walifundishwa pale THT kutunga na kuimba na pia lengo la THT ilikua kuchua wale wanaotoka ktk mazingira magumu na kuwapa juzi mbalimbali hivyo ilikua haijalishi una Elimu ya form ngapi ama laa lengo ni kukufundisha kuimba na kuigiza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom