Basi Nenda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 20,774
- 47,866
1. Bushoke tumecheza nae sana mpira makole pale, yeye alikua anadaka
2.voice wonder tulikua tukakutana kwenye mechi za kitaa, makole vs airport uwanja wa shule ya msingi makole. Mpira wa makaratas yan sembo.
3. Mswaki producer, huyu bwana mdogo alikua anakuja sana coco record studio ya kwanza pale Dodoma. Tulikua tunafanyia kazi kigamboni Karibu na magorofa mengi. Dogo hakua producer alikua msanii tena anaiga sauti ya ngwair sikuwahi kudhan anaweza kufika mbali
4.Moni central zone nilimkuta Dom sec, Mimi nikiwa nafundisha jioni darasa la watu wazima. Siku moja Moni alinifata na kunifananisha na producer flan wa pale pale Dom makole. Bahati nzuri yule producer nilishafanya nae kazi coco record hivyo nikamuunganisha nae.
Watu wengi maarufu hawana tabia ya kuringa ila watu wana inferiority complex juu yao. Unakuta mtu akipitwa bila kusalimiwa anasema jamaa anaringa wakati mtaani watu kibao wanampita bila kusalimia na hakuna shida. Mnapishana husalimii ukitegemea Kama atakusalimia, akiuchuna lawama tayar.
Sent using Jamii Forums mobile app
wabongo pia hua tuna tabia ya kupangiana jinsi ya kuishi
kwa mfano mimi ni mtu mkimya, na muda mwingi kichwani nina matatizo yangu, najikuta mkimya na sisalimii watu sometime ,hii huwafanya watu kusema nalinga
Sent using Jamii Forums mobile app