Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

Mkuu Ethos ninakufuatilia kwa karibu zaidi, nipo na telegram pia ila kutumia Google sheet naona kuna changamoto ya user friendleness hasa kuselect items zinazoinvolve table nzima kama unatumia simu
 
Mkuu Ethos ninakufuatilia kwa karibu zaidi, nipo na telegram pia ila kutumia Google sheet naona kuna changamoto ya user friendleness hasa kuselect items zinazoinvolve table nzima kama unatumia simu
Yes ni Kweli.. Google Sheet Kwenye simu ina changamoto kidogo... Hasa Aina ya simu pia... Kwenye Tablet inakuwa rahisi zaidi ila usikate tamaa..

Ukipata muda kidogo Kwenye Computer endelea kujifunza
 
Yes ni Kweli.. Google Sheet Kwenye simu ina changamoto kidogo... Hasa Aina ya simu pia... Kwenye Tablet inakuwa rahisi zaidi ila usikate tamaa..

Ukipata muda kidogo Kwenye Computer endelea kujifunza

Samahani Ethos nataka kujua, Nina document yangu ipo kwenye Excel lakini nikiprint haziji na page namba, nataka kujua kuweka page namba kwenye Excel ili niki print na page namba zitokee.
 
Samahani Ethos nataka kujua, Nina document yangu ipo kwenye Excel lakini nikiprint haziji na page namba, nataka kujua kuweka page namba kwenye Excel ili niki print na page namba zitokee.
Asante Kwa Swali lako zuri ambalo litafanya na wengine wajifunze

Nenda click page layout >>>page setup clink kimshale ambacho kipo upande wa chini karibu na formula bar halafu itakuletea dialog box ya page setup kama inavoonekana hapa chini..
ae295f3c1e9a03e091e73f48290b383e.jpg

Bonyeza Header and Footer kama Unataka page namba zionekane juu click header halafu utachagua options then click OK
ec5e7b8a6401cb70d1c7dccec8264376.jpg
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mk
TIP OF THE DAY :

Tumia Google Sheet Kwenye simu yako sio lazima. Uwe na Computer

Ingia play store andika Google Sheets halafu pakua..

Anza kufuatilia vitu vidogo vidogo wadau wanavyouliza hapa hata kama ukiwa safarini au kijiweni unapiga story..

Waswahili wanasema haba na haba hujaza kibaba...

Ukisha ipakue Kuna templates ambazo zimeshatengenezwa unaweza ukacheza nazo kupata maujuzi pia..

Kuna ya Calendar, Attendance Kwa walimu na hata Financial Statements Kwa wahasibu

Nitazielezea huko mbeleni

Enjoy!
Mkuu hiyo financial statement inapatikana kwa simu?
 
Nimekuwa nikipokea PM nyingi.. Kutokana na kubanwa na Majukumu mengine itakuwa sio rahisi kuwasiliana na mtu Kwenye simu...

Tutumie uzi huu kuuliza maswali na pia hakikisha upo kwenye Group la telegram ambapo nitaweka video fupi mara Kwa mara ili kurahisisha uelewa...

Asanteni sana!
 
VLOOKUP UPDATE

Umekuwa ukisikia watu wanazungmzia VLOOKUP kazini na kwingineko ??

Ngoja nikurahishie kidogo uielewe haraka sana kwa kukutajia mazingira ambayo inaweza kutumika
  • Kwenye Duka la jumla au rejareja- pale ambapo unataka kujua bei ya kila bidhaa ndani ya sekuende moja ukiwa umekaa... Kama uliziorodhesha bidhaa zote vizuri na na umetengeneza formula hii vizuri utakuwa unaingiza tu jina na itakuletea bei yake au taarifa uitakayo hapo hapo hata kama bidhaa zipo 10,000
  • Mwalimu kama unataka kujua marks za mwanafuzi fulani kwa haraka unaweza kuitumia pia kumbuka unaweza kutumia CRTL+F lakini VLOOKUP ndio ipo haraka zaidi
  • Wale watu wa Store kama unataka kujua namba ya bidhaa, tarehe iliyoingizwa au thamani yake VLOOKUP Itakutafunia ndani ya sekunde moja
 
Kuna video nimeitengeneza kule Kwenye Group... Nitazidi kuelezea endelea kufuatilia
Mkuu msaada kwenye hii kitu hapo ili kufanya jumla ya bei iwe hapo chi na jumla ya mauzo na jinsi ya kuweka TZS katika hizo hela hapo kwa kutumia kanuni mkuu,ahsanteh
Screenshot_2016-11-22-14-18-15.png
 
Mkuu msaada kwenye hii kitu hapo ili kufanya jumla ya bei iwe hapo chi na jumla ya mauzo na jinsi ya kuweka TZS katika hizo hela hapo kwa kutumia kanuni mkuu,ahsantehView attachment 437887
Hapo chini mwisho kabisa andika
=SUM (E3:E8)

Kuweka TZS nenda Kwenye Format >>> Currency halafu chagua $ TZS huwa haipo ila ukisha click unaweza edit na kuweka TSHS na ku drag

Nakushauri uweke juu uandike TZS mwanzo ili ijulikane tu kwamba hizo namba zipo katika TZS
 
Nimekuwa nikipokea PM nyingi.. Kutokana na kubanwa na Majukumu mengine itakuwa sio rahisi kuwasiliana na mtu Kwenye simu...

Tutumie uzi huu kuuliza maswali na pia hakikisha upo kwenye Group la telegram ambapo nitaweka video fupi mara Kwa mara ili kurahisisha uelewa...

Asanteni sana!
Hapo sawa mkuu...naomba na mimi niunge mkuu
 
Back
Top Bottom