Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

Mkuu ubarikiwe sana kwa hii elimu nimefanikiwa kwa urahisi sana niliwaza kutenganisha ingenichukua more than 2 weeks but nimeifanya kwa dk chache ila kuna suala kama zipo nying umedrag kama umeweka pale mwanzo uliweka 2 digit ikakutana na 3 digit utapata tofaut so inabidi urekebishe kwanza
Ni kweli usemavyo mkuu ndio maana nilikupa angalizo ..hiyo ni rahisi sana...kuna zaidi ya hiyo ila ni complex kidogo nashukuru kama imekuwezesha kufanya kazi yako... Endelea kufuatilia
 
namaanisha kwa mfano kwenye kila cell ndani ya column ina neno lenye herufi tano, kila herufi ya nne kwenye hilo neno ni S au H. Sasa nataka kusoti ambazo herufi yake ya nne ni S zikae pamoja na zile ambazo ni H zikae pamoja. Tunafanyaje

Nimekupata vizuri...

hapo unatumia =LEFT(A1,5) kwa CELL ya kwanza halafu utafanya hivyo hivyo kwa CELL ya pili so utapata Column mbili zenye H na S the utatengeneza column ya tatu kwa ajili ya kuziunganisha kwa kutumia =CONCATANATE(E1,E2) hapo E1 na E2 ni CELLS amabzo H na S zipo respectively... cheki short video kwenye group
 
Naomba kujua tofauti ya RANK,
COLUMN
CELL
RANK = Ni Function Kwa ajili ya Kupanga namba na kuzipa nafasi.. Mfano unapotaka kujua wa kwanza hadi wa mwisho katika darasa au mashindano

COLUMN ni sawa ule mpangalio wa vibox katika Excel Kushuka Hizi hupewa herufi A B C D....

ROW hupewa Namba 1,2,3...

CELL ni lugha katika Excel inayotumika kuelezea neno au namba ipo katika sehemu ipi mfano ukiandika A1 ina maana ni katika Column ya A Row ya 1


Angalizo : Hayo ni maelezo rahisi Kwa beginner
 
Mkuu kwa mara nyingine naomba mwongozo wa jinsi kurekebisha alama za watahiniwa katika somo la JIOGRAFIA I mean z-score kwa kutumia ms exelView attachment 439828
Asante kwa swali lako zuri ndugu Ta Castor... Kwanza ningependa kufahamu kama majawabu uliyopata huko juu yalikusaidia kufanikisha kazi yako ?

Turudi kwenye swali lako... Z score inawezekana kabisa ... Angalia video fupi niliyoiweka kama kutakuwa na swali zaidi niulize
 
Hakika umenisaidia sana nlikuwa sifahamu kitu kuhusu kuoanga matokeo kwa kutumia exel nkikuwa natumia kichwa ndipo nachapa sasa hv naona ni simple like ABC.
 
Hakika umenisaidia sana nlikuwa sifahamu kitu kuhusu kuoanga matokeo kwa kutumia exel nkikuwa natumia kichwa ndipo nachapa sasa hv naona ni simple like ABC.
Karibu sana mkuu... Hebu angalia hiyo ya Z Score halafu kama kutakuwa na swali karibu ili nielezee zaidi maana sijajua Kwenye matokeo huwa mnaishia wapi
 
Kaka,,Ethos nimefanya majaribio ya VLOOKUP ili kuweka bidhaa na bei auto...kila nikiijaru mwishon hailet matokeo..naambiwa kuna error....nifanyeje
 
Kaka,,Ethos nimefanya majaribio ya VLOOKUP ili kuweka bidhaa na bei auto...kila nikiijaru mwishon hailet matokeo..naambiwa kuna error....nifanyeje
Hongera Kwa kujaribu.. Naomba uweke picha kidogo nitajua tatizo
 
Hongera Kwa kujaribu.. Naomba uweke picha kidogo nitajua tatizo
b1678bfd32b3600d1b88da01eae20052.jpg
 
Hii z score ndo nini tena mkuu??
Wanatumiaga walimu kurekebisha matokeo... Unakumbuka shule ya msingi ulikuwa ukipata 100 na wa mwisho akipata 0 unaweza ikapunguzwa hadi ukapata 70 baada ya kurekebisha... Waalimu watakuelezea kiundani zaidi ngoja waje
 
Ukitumia Function ya Rank ni lazima ukibadilisha na nafasi yake itabadilika... Ila hakikisha ile jumla umeipata kwa kutumia Function ya SUM na sio manually
Nimekupata mkuu ila nilichotaka kujua kama kuna uwezekano wa Total Auto Sorting. Kumbe utatakiwa u-sort upya.
 
Mkuu nashukuru Sana kwa darasa hili

Naomba unisaidie kitu hapa
Nataka kutengeneza amortization table ambayo ipo hivi .. .

Mr. X amekopa Tshs 2,000,000/ ambayo riba Ni 10% muda wa mkopo Ni miezi 10 nataka nitengeneze hiyo amortization table inayoonyesha kila mwezi anatakiwa arejeshe Tshs. 220,000/ na baada ya miezi 10 awe na balance ya Tshs. 0/
Asante
 
Naomba kuuliza nawezaje kuandaa division ya mwanafunzi kwa kutumia grade? Mfano division I,II,III,IV,FLD
 
Mada tamu sana hii, wengi wetu tupo makazini lakini excel inatupiga mueleka
 
Mkuu nashukuru Sana kwa darasa hili

Naomba unisaidie kitu hapa
Nataka kutengeneza amortization table ambayo ipo hivi .. .

Mr. X amekopa Tshs 2,000,000/ ambayo riba Ni 10% muda wa mkopo Ni miezi 10 nataka nitengeneze hiyo amortization table inayoonyesha kila mwezi anatakiwa arejeshe Tshs. 220,000/ na baada ya miezi 10 awe na balance ya Tshs. 0/
Asante
swali zuri sana mkuu... hapo lazima uielewe function ya PMT..

Kwanza andaa schedule yako inayoonesha
B
1 Interest 10%
2 Months 10
3 Principal 2,000,000

Uki click katika cell yeyote ukaandika =PMT itakuletea format ifuatayo

PMT(rate, nper, pv, [fv], [type])

  • Rate hapo kwenye rate ndio riba yenyewe kwahiyo andika 10% lakini kumbuka kugawanya kwa 12 so itakuwa B1*12

  • Nper Hapo andika idadi ya miezi unayotaka mkopo ulipwe...

  • Pv Kiasi cha mkopo principal

  • Fv hapo weka 0 na kwenye type weka 0
Then enter....
 

Attachments

  • IMG_20161127_122233.jpg
    IMG_20161127_122233.jpg
    293.1 KB · Views: 89
Learn programming, specifically Visual Basic for Applications (Excel VBA). Andika macros for any problem you want automated. Utaonekana mchawi mbona....
 
Back
Top Bottom