Tupeane mbinu za kuweza kujidhibiti na uraibu wa soda

Tupeane mbinu za kuweza kujidhibiti na uraibu wa soda

Kuna dada mmoja mama lishe bila Pepsi 3 Kwa siku??.. anahangaika kama anatafutwa na pride au finca..Bandani kwake soda za wateja anamilizaga yeye kwanza .. nikamuhesabia 3x30=90 ambapo 90x12=1080 soda Kwa mwaka SAWA na wastani wa kreti 45 Kwa mwaka....
 
Watu wengi sana wanapambana na uraibu wa sigara, pombe na madawa ya kulevya. Lakini wakishaushinda uraibu huo hujikuta wameangukia kwenye uraibu mwingine hatari lakini usio ongelewa. Uraibu huo sio mwingine ila unywaji wa soda, hasa mazingira yenye joto kama mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga , Lindi na Mtwara

Soda hasa za Pepsi na Coca Cola (baridiiiiii) hushuka vizuri sana kipindi cha joto kali. Ubaridi, usukari na ladha ya kupurudisha huleta msisimko fulani amazing mwilini. Msisimko huu ukikunogea unakufanya uwe teja wa soda.

Wengi walioacha kunywa pombe hujikuta wanaangukia kwenye urahibu huu na kuwa mateja kabisa.

Tupeane mbinu mbalimbali za kuushinda urahibu wa soda, maana rafiki yangu baada ya kuacha pombe sasa kwa siku ni lazima agonge Pepsi baridi tatu, anasema yeye bila Pepsi siku haijaisha.
Epuka kakaa vijiwe vya wanywa soda, wekeza kwenye matunda na tangawizi
 
Binafsi nataka niache kunywa juisi ya miwa na ugali
 
Soda ina uraibu gani mkuu kama sio kujiendekeza tu.
 
Back
Top Bottom