Tupeane mbinu za kuweza kujidhibiti na uraibu wa soda

Tupeane mbinu za kuweza kujidhibiti na uraibu wa soda

Kunywa maji ya baridi sana kila mara unapopata hamu ya soda,fanya hivo kila siku baada ya mwezi mmoja njoo ulete mrejesho.
kama hamna fridge? maana kununua maji naonaga hasara
Ukianza kupata stomach burns utaacha hivo vitu mwenyew
unaweza ukapata na bado ukanywa , mfano mimi
1)Akikisha chakula chako kikuu kiwe ugali,hapo soda kwisha habari yake. ugali ni adui namba moja wa kinywaji cha soda

2) asilimia 80% ya kiu au hamu ya soda tunayo pata siyo ya kweli ...kama ukipata kiu au hamu ya soda basi kabla ya kunywa soda kunywa maji kwanza kisha ukiona hamu ya soda bado ipo ndipo nunua soda unywe, very simple and perfect method [emoji108] it work 100%
ugali?? 🤣🤣🤣 yani mimi nikila ugali ndo natafuta soda iliko yani vinarandana sana hasa nikila vitu vya michuzi, naonaga pepsi inakata shombo
Mimi nikimaliza kula ugali ndo napata kiu ya Pepsi balaa ili nisukumizie ukae sawa
🤣tena ukila vitu vya michuzi kuna kqshombo flani unajiskia kama ukakate na pepsi
 
Dah binadamu tunatofautiana sanaaa yaani kwamba nikose usingizi kisa soda? Ukinipatia soda mpk nimalize chupa jasho linanitoka, naweza maliza mwaka bila kuonja soda lakini sasa siku ikipita sijapata vitu vikali nahisi ulimwengu umenitenga.
 
Nikuambie kitu, hata maji haya maji yanayotiririka ukiyazidisha mwilini yanaleta athari kubwa tu. Nina bro wangu yeye alikuwa anakunywa hadi lita 5 kwa siku, siku akajisikia vibaya, kwenda hospital akaambiwa apunguze unywaji wa maji, asizidishe lita 3, hasa ukizingatia anakaa sana zaido ya kutembea.
Kila kitu kikizidi ni hatari
 
Soda ni hatari kwa kuleta kisukari hasa fanta orange na milinda zote
Muwe mnaweka na vithibitisho na vyanzo vyake ili kupunguza mijadala.

Kwa hiyo nami nikiibuka na hoja bin vuu kuwa kufanya mapenzi kuna madhara, bila kuambatisha "tabu zake", ndonakuwa nimemaliza?
 
Watu wengi sana wanapambana na uraibu wa sigara, pombe na madawa ya kulevya. Lakini wakishaushinda uraibu huo hujikuta wameangukia kwenye uraibu mwingine hatari lakini usio ongelewa. Uraibu huo sio mwingine ila unywaji wa soda, hasa mazingira yenye joto kama mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga , Lindi na Mtwara

Soda hasa za Pepsi na Coca Cola (baridiiiiii) hushuka vizuri sana kipindi cha joto kali. Ubaridi, usukari na ladha ya kupurudisha huleta msisimko fulani amazing mwilini. Msisimko huu ukikunogea unakufanya uwe teja wa soda.

Wengi walioacha kunywa pombe hujikuta wanaangukia kwenye urahibu huu na kuwa mateja kabisa.

Tupeane mbinu mbalimbali za kuushinda urahibu wa soda, maana rafiki yangu baada ya kuacha pombe sasa kwa siku ni lazima agonge Pepsi baridi tatu, anasema yeye bila Pepsi siku haijaisha.
Dawa hii hapa kaka
_ (1).jpg
 
kuacha uraibu wa soda inawezekana kabisa ni swala la maamuzi,pia mbona kuna juisi natural kabisa ,Kama za miwa,strawberry,ukwaju na nanasi tena ni zina flavour nzuri kuliko ata hizo soda
 
Mimi nikimaliza kula ugali ndo napata kiu ya Pepsi balaa ili nisukumizie ukae sawa
Angalia mboga unayotumia kulia ugali ...ndimu au limao ni muhimu kwenye mboga ya ugali au kachumbali yenye ndimu au limao
Pia nimekupa kanuni mbili zenye kufanya kazi kwa pamoja kama ukila ugali unapata kiu au hamu ya soda tumia kanuni namba 2 kabla ya kutumia soda ikigoma hiyo kimbia mbio kanunue soda labda una kisukari cha kushuka
 
Muwe mnaweka na vithibitisho na vyanzo vyake ili kupunguza mijadala.

Kwa hiyo nami nikiibuka na hoja kuwa kufanya mapenzi kuna madhara, bila kumbatisha "tabu zake", ndonakuwa nimemaliza?
Hauhitajiki uthibitisho wowote ule mkuu,wewe piga zako soda bariiiiidi bila shida yoyote.

Mwana anakuonea wivu unavyoenjoy soda yako.
 
kama hamna fridge? maana kununua maji naonaga hasara

unaweza ukapata na bado ukanywa , mfano mimi

ugali?? [emoji1787][emoji1787][emoji1787] yani mimi nikila ugali ndo natafuta soda iliko yani vinarandana sana hasa nikila vitu vya michuzi, naonaga pepsi inakata shombo

[emoji1787]tena ukila vitu vya michuzi kuna kqshombo flani unajiskia kama ukakate na pepsi
Kumbe jibu langu linakufaa nimekujibu kabla ya kuona hii komenti utakuta jibu mapishi mabovu ugali viendane na mapishi sahihi ya mboga ndimu au limao ni muhimu na kachumbali
 
Watu wengi sana wanapambana na uraibu wa sigara, pombe na madawa ya kulevya. Lakini wakishaushinda uraibu huo hujikuta wameangukia kwenye uraibu mwingine hatari lakini usio ongelewa. Uraibu huo sio mwingine ila unywaji wa soda, hasa mazingira yenye joto kama mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga , Lindi na Mtwara

Soda hasa za Pepsi na Coca Cola (baridiiiiii) hushuka vizuri sana kipindi cha joto kali. Ubaridi, usukari na ladha ya kupurudisha huleta msisimko fulani amazing mwilini. Msisimko huu ukikunogea unakufanya uwe teja wa soda.

Wengi walioacha kunywa pombe hujikuta wanaangukia kwenye urahibu huu na kuwa mateja kabisa.

Tupeane mbinu mbalimbali za kuushinda urahibu wa soda, maana rafiki yangu baada ya kuacha pombe sasa kwa siku ni lazima agonge Pepsi baridi tatu, anasema yeye bila Pepsi siku haijaisha.
Mkuu Bujibuji nimejifunza neno jipya la kiswahili leo urahibu. Kumbe ndo addiction kwa kiingereza.
 
Back
Top Bottom