Tupeane mbinu za kuweza kujidhibiti na uraibu wa soda

Tupeane mbinu za kuweza kujidhibiti na uraibu wa soda

1)Akikisha chakula chako kikuu kiwe ugali,hapo soda kwisha habari yake. ugali ni adui namba moja wa kinywaji cha soda

2) asilimia 80% ya kiu au hamu ya soda tunayo pata siyo ya kweli ...kama ukipata kiu au hamu ya soda basi kabla ya kunywa soda kunywa maji kwanza kisha ukiona hamu ya soda bado ipo ndipo nunua soda unywe, very simple and perfect method [emoji108] it work 100%

Uzi ufunge
 
Watu wengi sana wanapambana na uraibu wa sigara, pombe na madawa ya kulevya. Lakini wakishaushinda uraibu huo hujikuta wameangukia kwenye uraibu mwingine hatari lakini usio ongelewa. Uraibu huo sio mwingine ila unywaji wa soda, hasa mazingira yenye joto kama mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga , Lindi na Mtwara

Soda hasa za Pepsi na Coca Cola (baridiiiiii) hushuka vizuri sana kipindi cha joto kali. Ubaridi, usukari na ladha ya kupurudisha huleta msisimko fulani amazing mwilini. Msisimko huu ukikunogea unakufanya uwe teja wa soda.

Wengi walioacha kunywa pombe hujikuta wanaangukia kwenye urahibu huu na kuwa mateja kabisa.

Tupeane mbinu mbalimbali za kuushinda urahibu wa soda, maana rafiki yangu baada ya kuacha pombe sasa kwa siku ni lazima agonge Pepsi baridi tatu, anasema yeye bila Pepsi siku haijaisha.
maji majii maji maji maji ya moto/kawaida
 
1)Akikisha chakula chako kikuu kiwe ugali,hapo soda kwisha habari yake. ugali ni adui namba moja wa kinywaji cha soda

2) asilimia 80% ya kiu au hamu ya soda tunayo pata siyo ya kweli ...kama ukipata kiu au hamu ya soda basi kabla ya kunywa soda kunywa maji kwanza kisha ukiona hamu ya soda bado ipo ndipo nunua soda unywe, very simple and perfect method [emoji108] it work 100%
Upo sahihi kabisa mkuu, hiyo kitu mara nyingi huwa nafanya na ninapata majibu positive kabisa ila watu wengi hawapendi maji upenda soda kama kifungua kinywa
 
Mimi nikiwa kama meneja masoko wa Pepsi na coca-cola kampani nashauri Tunywe soda lakini tunywe kwa kiasi,once kila kitu lazima kifanyike kwa kiasi.

Pointi kubwa hapa ni kiasi wakuu,ukizidi kunywa maji kuna madhara yake, ukizidi kunywa chai ni madhara, ukidhidi kunywa soda ni madhara.

Zingatieni hapo kwenye kiasi wakuu unaweza ukaacha uraibu wa kunywa soda ukayavamia Maji ukanywa kwa wingi ukapata madhara vile vile.

Coco-cola, Believing is magic
Pepsi dare for more
Dah kuuliza si ujinga, samahani mkuu naomba uelezee madhara ya kunywa maji kwa wingi mana nimeona hoja yako mpk nmeshangaa embu toa elimu kidogo mkuu
 
Mimi soda sina shida nazo nakunywa mara chache sana tena nikipiga pafu mbili tatu hamu inaisha labda kipindi hiki jua kali naweza maliza.
Shida yangu ni chai Mimi ni mlevi wa chai na sijui naachaje.
Siwezi kunywa vikombe viwili nikaridhika nakunywa chupa nzima mbaya zaidi siwezi jaza kikombe naweka nusu nakunywa nikimaliza naongeza kidogo kidogo mpaka inaisha.
Angalau sasa hivi najitahidi ila kuacha nimeshindwa.
 
Mimi nashukuru, leo naweza kusema natimiza miaka miwili.
Niliamua tu baada ya kuona uzito unaongezeka .
 
Sipo kote kinywaj changu kikuu ni maji soda sipendi hata kumaliza chupa ni mtihani
 
Kitu kingine kitimoto yaan nisipokula siku yabgu haiendi. Mpaka nimepima nimekutwa na mafuta mengi kwenye damu naiogopa sasa hivi
 
Swala la kuepuka kiu ya soda ni kunywa maji, kutumia juice ya matunda halisi ,kufanya mazoezi jioni then kupimzika yaani kulala mapema.
 
Dah kuuliza si ujinga, samahani mkuu naomba uelezee madhara ya kunywa maji kwa wingi mana nimeona hoja yako mpk nmeshangaa embu toa elimu kidogo mkuu
 
Back
Top Bottom