Tupeane mbinu za kuweza kujidhibiti na uraibu wa soda

Tupeane mbinu za kuweza kujidhibiti na uraibu wa soda

Wengine tupo kwenye mkwamo;
Jioni Jägermeister/Konyagi
Asubuhi soda.

Hatujaja kulinda Dunia
 
Niliacha uraibu wa pombe na soda, miaka zaidi ya saba sasa, hamna ujanja au mbinu, walk away, acha tu!!!
 
Nacho shukuru mungu sijawahi kuwa controlled na kitu chochote had mimi mwenyew nijickie naweza kaa hata miez mitatu sjanywa soda
Just imagin npo sehemu yenye joto kal sana lakn huwez nkuta na maji baridi😒
 
Muhanga wa Pepsi nipo mbioni kuziacha hadi sasa nina mwezi mmoja sijainywa, nakunywa sana maji na juice,

Ila uraibu wangu mimi ni Big G [emoji43]‍[emoji94]
Guys siwezi kukaa bila kutafuna Big G niliwahi kujaribu kukaa wiki moja nilihisi nachanganyikiwa, nikazitafuta bila kupenda.
 
Watu wengi sana wanapambana na uraibu wa sigara, pombe na madawa ya kulevya. Lakini wakishaushinda uraibu huo hujikuta wameangukia kwenye uraibu mwingine hatari lakini usio ongelewa. Uraibu huo sio mwingine ila unywaji wa soda, hasa mazingira yenye joto kama mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga , Lindi na Mtwara

Soda hasa za Pepsi na Coca Cola (baridiiiiii) hushuka vizuri sana kipindi cha joto kali. Ubaridi, usukari na ladha ya kupurudisha huleta msisimko fulani amazing mwilini. Msisimko huu ukikunogea unakufanya uwe teja wa soda.

Wengi walioacha kunywa pombe hujikuta wanaangukia kwenye urahibu huu na kuwa mateja kabisa.

Tupeane mbinu mbalimbali za kuushinda urahibu wa soda, maana rafiki yangu baada ya kuacha pombe sasa kwa siku ni lazima agonge Pepsi baridi tatu, anasema yeye bila Pepsi siku haijaisha.
Mi niliamua tu, kuwa Sasa naacha soda, since 2003 till today soda NEHI
 
1)Akikisha chakula chako kikuu kiwe ugali,hapo soda kwisha habari yake. ugali ni adui namba moja wa kinywaji cha soda
Mimi nikimaliza kula ugali ndo napata kiu ya Pepsi balaa ili nisukumizie ukae sawa
 
Binafsi karibu na nimeweza kushinda uraibu wa energy ilifika kipibdi nisipokunywa asubuhi siku yangu haiendi kabisa. Japo napata shida sana ila nakaribia kushinda hii tamaa
 
Mimi nilijitahidi kuacha yaani niliifosi nafsi kuwa ninahitaji kuacha soda na nikaacha.Na Huwa Ile arosto ya soda Huwa sinaga kabisa mda mwingine napewa soda nashindwa maliza.
 
Watu wengi sana wanapambana na uraibu wa sigara, pombe na madawa ya kulevya. Lakini wakishaushinda uraibu huo hujikuta wameangukia kwenye uraibu mwingine hatari lakini usio ongelewa. Uraibu huo sio mwingine ila unywaji wa soda, hasa mazingira yenye joto kama mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga , Lindi na Mtwara

Soda hasa za Pepsi na Coca Cola (baridiiiiii) hushuka vizuri sana kipindi cha joto kali. Ubaridi, usukari na ladha ya kupurudisha huleta msisimko fulani amazing mwilini. Msisimko huu ukikunogea unakufanya uwe teja wa soda.

Wengi walioacha kunywa pombe hujikuta wanaangukia kwenye urahibu huu na kuwa mateja kabisa.

Tupeane mbinu mbalimbali za kuushinda urahibu wa soda, maana rafiki yangu baada ya kuacha pombe sasa kwa siku ni lazima agonge Pepsi baridi tatu, anasema yeye bila Pepsi siku haijaisha.
Tukimaliza masomo ya sekondari ama chuo bila kusomea kozi ya MD na kuwa wataalamu wa afya, saazingine tunaishi kitaa kwa kujishuku shuku sana na kujishitukia sana ujue!

Hivi shughuli zote ngumu tunazopambana nazo, twaweza kuhofia kupata madhara kwa vinywaji vywepesi kama soda!

Ninavyojua hakuna madhara yoyote apatayo mtu kwa matumizi ya vyakula kwa viwango cha kawaida.

Si soda tu, chochote ukikitumia kupita kiasi kina madhara.

Na maradhi kwa mfano kisukari ni ugonjwa utokanao na hitilafu ya kongosho ama kurithi na siyo kwa ajili ya matumizi ya vyakula vitamutam!

Dah!

Mi naona watu wengi wanabagua bagua vyakula kwa uoga wa habari za kukaririshwa!

Basi kama ni hivyo, dunia hii siyo fair kwa kweli!

Ukiwa na kipato, marufuku kutumia vinono!

Ukiwa masikini unavitafuta vinono lakini hauvipati kwa kukosa pesa!

Anayestahili atumbue maisha ni mtu wa namna gani hapa duniani, maana maisha bora ni pamoja na kugonga msosi wa adabu?
 
Hapa ninapo soma huu uzi ninakunywa orange yangu taratiiibu wala sina pressure.

Kuacha soda inategemea na mazingira yako unayoishi au unayofanyia kazi.
Assume kazini kwako au nyumbani kwako umezungukwa na wauza soda, kuacha kunywa soda sahau kabisa.
 
Sku izi kla ktu kibaya sjui mnataka tukule au tukunywe nn sjui

Ila acheni kututisha sana kla mtu atakufa nazan tuenjoy tu maisha
 
Mimi nikiwa kama meneja masoko wa Pepsi na coca-cola kampani nashauri Tunywe soda lakini tunywe kwa kiasi,once kila kitu lazima kifanyike kwa kiasi.

Pointi kubwa hapa ni kiasi wakuu,ukizidi kunywa maji kuna madhara yake, ukizidi kunywa chai ni madhara, ukidhidi kunywa soda ni madhara.

Zingatieni hapo kwenye kiasi wakuu unaweza ukaacha uraibu wa kunywa soda ukayavamia Maji ukanywa kwa wingi ukapata madhara vile vile.

Coco-cola, Believing is magic
Pepsi dare for more
 
Soda ni hatari kwa kuleta kisukari hasa fanta orange na milinda zote
 
kutoka mo energy hadi pepsi😃

wakupe ubalozi kabsa maana kupitia uzi huu tayari pepsi kainuliwa ngoja na mimi nikajaribu nioneckm ntakuwa na huo uraibu.
 
Na hizi energy drink zinaua kibofu kila muda ni kwenda kukojoa
 
baada ya supu asubuhi then ushushie na pesi, coca au sprite. Ile feeling yake we acha tu.
 
View attachment 2480410
Tujaribu kuhamia kwenye maji safi na salama yaliyoongezwa kipande cha limao 🍋 na chumvi ya mawe kodogo tu
Nikuambie kitu, hata maji haya maji yanayotiririka ukiyazidisha mwilini yanaleta athari kubwa tu. Nina bro wangu yeye alikuwa anakunywa hadi lita 5 kwa siku, siku akajisikia vibaya, kwenda hospital akaambiwa apunguze unywaji wa maji, asizidishe lita 3, hasa ukizingatia anakaa sana zaido ya kutembea.
 
1)Akikisha chakula chako kikuu kiwe ugali,hapo soda kwisha habari yake. ugali ni adui namba moja wa kinywaji cha soda

2) asilimia 80% ya kiu au hamu ya soda tunayo pata siyo ya kweli ...kama ukipata kiu au hamu ya soda basi kabla ya kunywa soda kunywa maji kwanza kisha ukiona hamu ya soda bado ipo ndipo nunua soda unywe, very simple and perfect method [emoji108] it work 100%
Aisee
 
Back
Top Bottom