Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
- Thread starter
- #81
Twin bank hoi😂Kilometers zaidi ya 56 kwenda na kurudi.. Nilifika home twin bank za manii ziko hoi😂
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Twin bank hoi😂Kilometers zaidi ya 56 kwenda na kurudi.. Nilifika home twin bank za manii ziko hoi😂
Yes, najua. Kuwa mwanamke tu ni utajiri tosha.Mimi wa kike niwe nahela zakati za juu mie sio sawa nawewe
Wengi tu niliowamini marafiki ,wapenzi hatari .sana ningekuwa tajiri kama ningekuwa na,akili ya utambuziWanaume wangapi?
KumbeeeYes, najua. Kuwa mwanamke tu ni utajiri tosha.
Yeeeh!!Kumbeee
Nyumbanitu?Shetani ni muhuni Kama wahuni wengine, hizo purukushani zote na mbuzi na kuku unaambulia usaa.
Kama ni ule msitu wa Iringa kuna watu majasiri waliwahi kuingia bila madawa yoyote, hakuna chochote kilichofichwa na wajerumani, jamaa walikuwa na kifaa chenye remote sensing, kinacho detect madini, hakuna kitu pale, jamaa wapo hadi leo Wala hakuna mzimu uliwadhuru, hofu mbaya sana.
Kuna afisa misitu aliwaonya kuhusu mizimu mikali ya pale, yeye alibakia nje ya msitu akitetemeka nusura kujikojolea akiamini jamaa wanaenda kufa, waliporudi akataka kuwakimbia anafikiri ni mizimu sio watu wa kawaida
Nguvu za Giza na kila aina ya negative energies ni Jambo baya kabisaWengi tu niliowamini marafiki ,wapenzi hatari .sana ningekuwa tajiri kama ningekuwa na,akili ya utambuzi
Ziwani kuna unyama sana unafanyikaTulikuwa mwaroni ukerewe tumelala. Tunalinda mitumbwi na engine, mafuta ya petroli watu wasije Iba ghafla bin vuu wakatokea watu 8 pale sisi tupo wawili tu gemani tumelala
tukaambiwa mko chini ya ulinzi, tukamwagia maji ya baridi kinoma ghafla tukapigwa paba nyingi sana mgongoni tukaambiwa Aya hapo mnasamaki wangapi tukasema miatano kwa makadirio tunaomba msituue kumbuka hapo ni satisa usiku 🥶oya tukalazimishwa kula samaki wabichi Kila mmoja wetu huku tunachezea bapa nilitapika kishenzi, jamaa wakanibeba wakanitupa kwenye maji na mwenzangu vile vile 🙌uvuvi sitaki kuusikia
Mzee kule. Sio poa alafu kuna Ile unapiga kazi labda inapatikana 25M labda boss anaacha ata Sita milion mugawane wafanya kazi wote muliopo tuseme labda mpo 10, mara unadhulumiwa ukileta mdomo unaweza Ata nyongwa uskuZiwani kuna unyama sana unafanyika
Hadithi ya Kalumakenge vile🙂Nikauza mbuzi, nikahamia kwa mjomba Kijiji jirani, nikajitibu huko hadi nikapona. Mganga kanisababishia GONO, Hawana sio mganga, ni Yule binti yake. Hapana sio Yule binti aliyenisababishia GONO, Ila ni Yule MZUNGU WA Jambo Toto!!! Hapana naye namsingizia tu, Ila ni zile Mali za Ujerumani. Hapana nazo nazisingia, ni tamaa zangu tu zankupata utajiri wa mang'amung'amu. Yessss..... Hili ndio jibu sahihi. Mizimu imenipiga kabla hata sijavamia msitu wa tambiko.
KwaniniWanaume ndio maana mnakufa mapema
Petrol inaua nyoka ?Sitasahau, nilipewa deal na Wazungu fulani kutoka Nairobi Kenya, wakanipa na mtaji wa mabanda kabisa. Wakaniletea vifaranga vya ñyoka, na wataalam wa kunifundisha kuwafuga, nikawafuga wakaja baada ya miezi mitatu, wakavuna sumu ya nyoka, na nikapatiwa kiwango kizuri sana cha fedha za kigeni.
Wakaja tena baada ya miezi mitatu mingine, nikalipwa vizuri zaidi ya mwanzo.
Wakanipeleka Nairobi kwenye ofisi zao, kwa gharama zao. Hakika nikaona maisha nimeyapatia.
Waliporudi mara nyingine ikawa ndio mwisho wa kuja kwao, wakaniachia mijoka mingi na nisijue pa kuwaweka.
Siku nikaamua Bora mabanda niya spray petrol nyoka wote wafe.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa
Hata wewe sasa ushakuwa lishangaziHapana mlokole wetu ni hivi huo mwaka naogeshwa sio naoga
Ukija jua hujui ndio alikukwamishaNguvu za Giza na kila aina ya negative energies ni Jambo baya kabisa
Tupo live mkuu😂😂😂
Utajiri ni roho aisee. Nakumbuka mwaka 2017 kuna familia fulani waliniambia Wana kiwanja wanauza kipo maeneo mazuri sana ufukweni kabisa. Sasa mimi nikawa nawaaambia Madalali na ile familia ilikuwa ni ya Mzee mmoja ambaye ameshawahi kuwa Waziri, balozi wa nchi kama 6 tena zile kubwa duniani.
Kwa sababu ile familia wenye mali ni wanawake na wameishi sana nje za nchi mambo ya kutafuta wateja yalikuwa ni mageni kwao.
Sasa kuna dalali fulani nilimfuata baada ya kuelekezwa na watu ni kaongea naye nikamwambia kuna eneo lipo sehemu fulani ni 1650 sqm lina ukuta na servant quarter nikamwambia linauzwa usd laki 5 na kuna asilimia ya 5 udalali hapo. Basi yule dalali akaniambia kuna mtaalam yupo Kisiju tukienda kuongea naye hili jambo ni simple sana na mimi huwa na tumia sana yaani pale nikumuambia na yeye atasoma dua tu haichukui wiki mbili Tajiri atatutafuta mwenyewe.
Nilamuuliza anapatikana wapi huyo mtaalam? Akaniambia kisiju nauli kama 35 elfu kila mtu na inabidi twende na sukari, mikate, kahawa kumpelekea kama zawadi. Basi nikamfuata yule Mama ambaye ni Dada mkubwa wa familia tena alikuwa ni Afisa mkubwa wizara fulani nyeti sana.
Nilipomweleza akaniambia kama ni hivyo sawa akanipa na nauli ya kwenda huko Kisiju. Siku ya kwenda tukanunua mikate, sukari kilo 1 na kahawa ya Africafe. Aisee ile safari ilikuwa ni mbali mno. Tulipandia gari Mbagala kuelekea huko Kisiju, tukafika sehemu kama njia panda tukashuka kwenye gari. Tukachukua bodaboda aisee ni mbali halafu ni porini kweli kweli. Nadhani ni umbali kama wa Makumbusho mpaka Pugu. Kufika pale yale mazingira yanaogopesha mnoo. Nyumba ipo katikatya pori yamepaki magari mazuri kuna generator kubwa sana, TV nchi 45 ipo nje tu na kijumba cha hovyo hovyo. Mali za yule mtaalam zipo nje nje na hakuna wa kugusa.
Hatukumkuta yule mtaalam aisee nilipaniki na kuanza kuwachenjia bodaboda na niligombezana nao sana. Nyie mnajua mtu hayupo halafu mmetuleta mpaka huku iwaje?
Nilikua najiamini hata yule Mzee dalali akaniona aisee huyu Kijana na mwanaume kweli. Wale bodaboda wakaanza kuleta uswahilini nikawaambia pikipiki zenu nimeshazipiga picha na ninazituma polisi nyie ni matapeli waliogopa nikawaambia turudisheni haraka stendi nikawapa elfu 40 tu badala ya 70 elfu.
Yule mtaalam kumbe alikuwa ameenda Dar nyumbani kwake maeneo ya Mbagala ikabidi tuunganishe mpaka Maji matitu Mbagala kutokea Kisiju kufika Mbagala mida ya saa 1 jioni tukakuta kuna shughuli mzito sana na hatukuweza kuonana naye maana alikuwa ameshakuwa katika hali nyingine kabisa sijui ndio alikuwa anazungumza na majini na damu ya imemwaga nyingi sana na nyingine ipo kwenye ndoo mbili za lita 20. Tukaambiwa na vijana wake ondokeni haraka sana njooni kesho kuna viumbe wazito wanaingia hapa.
Itaendelea
HakikaUkija jua hujui ndio alikukwamisha