Tupeleke watoto shule za kiingereza, Tuache kupotoshana kwa kauli za kimasikini kusifia kayumba na kusingizia shule za kiingereza zinaharibu watoto.

Tupeleke watoto shule za kiingereza, Tuache kupotoshana kwa kauli za kimasikini kusifia kayumba na kusingizia shule za kiingereza zinaharibu watoto.

yaani usome kwa muda wa miaka 15, au wewe uwe ndo na umri wa miaka 15? fafanua kidogo?
Ili Ku-master lugha inamuhitaji MTU kutumia miaka 15 na kuendelea , hayo mambo ya Ras simba na British utaishia kuzungumza salamu Ila kuwa na ufahamu wa lugha huwezi
 
Masikini tunauziwa kingereza kwa bei ghali tukidanganywa ndo elimu yenyewe hiyo.

Kujua kingereza na huna maarifa yoyote Kichwani kutokana na mfumo mbovu wa elimu hakuwezi kukusaidia chochote.

Mataifa makubwa yaliyofanikiwa kielimu yametumia lugha mama kufundisha watu wao. Sisi tunataka kukumbatia kingereza ili iweje???

Taifa lipi lililoendelea kielimu Kiasi cha kujitegemea kiteknolojia n.k kwa kufundishia lugha ya kigeni ili tulitumie Kama reference?

Tufundishe watu wetu kwa lugha yetu, na kingereza kifundishwe kama lugha.
 
Ili Ku-master lugha inamuhitaji MTU kutumia miaka 15 na kuendelea , hayo mambo ya Ras simba na British utaishia kuzungumza salamu Ila kuwa na ufahamu wa lugha huwezi
ni lugha yeyote au kiingereza tu?
 
Wabongo ni wajinga kweli, kama juzi kati kuna mTanzania mmoja nilikuwa nabishana nae, namuambia watoto wa matajiri wana akili kuliko watoto wa masikini kwa asilimia kubwa, na pia mtoto wa mtu mwenye uwezo kiuchumi ana exposure kubwa na pia probability ya maisha yake mbeleni kuja kuwa bora na asilimia za kutengeneza career yake ni kubwa.

mtu anabisha.

Namuambia hata uduni wa chakula tu unapelekea mtoto akili yake kuwa butu, inabidi ifike wakati wa Tanzania mfahamu kwamba umasikini sio sifa ni laana.

Unakuta mtu anampeleka mtoto shule ilimradi kisa na yeye alisomea huko, kama una uwezo hata kumpeleka mtoto shule ada yake ni Mil 12 kwa mwaka mpeleke mtoto, tuacheni ujinga.

Sehemu kubwa watoto wanapata marafiki huko na kuwa na connection.
 
Kujua Kwa ufasaha lazima usome miaka kuanzia 15 years ndo utakaa sawa
Mkuu abby Chan’s anaongea lugha nne, ana miaka mingapi?

Kuna dada ni my Egypt anasubiria wageni kwenye ma pyramid anaongea lugha 10 tofauti ana miaka 24.
 
Kuna vitu vingi sana watanzania hawajui kuhusu hizi English Medium, na hapa nitakupa mwanga.

1. Shule za English medium hazifanani kiubora na sio rahisi kugundua hizo tofauti unless uwe mwerevu.

2. Shule za English medium hazina uratibu mzuri wa mamlaka kufuatilia misingi na ubora wa kielimu unaotolewa hapo.

3. Msingi mkuu wa uanzishwaji na uendeshwaji wa English Medium karibu zote ni biashara na sio huduma.

4. Kiingereza ndio kichaka kikuu cha kufichia udhaifu wa ubora wa elimu katika English medium zote.

5. English medium zimejikita zaidi kwenye mbwembwe za kumtengeneza mtoto kukua katika misingi ya tamaduni za kizungu.
 
Mtoto kufahamu kingereza hakumfanyi awe na akili au ufahamu zaidi.

Ni sawa na kuuliza mbona tunafeli somo la kiswahili na wakati ndiyo lugha tuyaoongea kila muda.

Vivyo hivyo hivyo hata kufahamu kiswahili hakumfanyi mtoto awe na akili.
Isipokuwa unapokuwa unaifahamu lugha ya kufundishia inarahisisha sana kuelewa kinachofundishwa.

Achana na akili/mawazo ya kijimajima, eti uzalendo.
 
Mimi mzarendo.
 
Sehemu ya kumptia mtoto elimu bora ya msingi wa maisha yake ya kila siku ni Madrassa, zingine zote ni ziada tu.
Yaani we mama shukuru upo tanzania kwa hicho kimbelembele chako arabuni ungeshanyongwa.
 
Masikini tunauziwa kingereza kwa bei ghali tukidanganywa ndo elimu yenyewe hiyo.

Kujua kingereza na huna maarifa yoyote Kichwani kutokana na mfumo mbovu wa elimu hakuwezi kukusaidia chochote.

Mataifa makubwa yaliyofanikiwa kielimu yametumia lugha mama kufundisha watu wao. Sisi tunataka kukumbatia kingereza ili iweje???

Taifa lipi lililoendelea kielimu Kiasi cha kujitegemea kiteknolojia n.k kwa kufundishia lugha ya kigeni ili tulitumie Kama reference?

Tufundishe watu wetu kwa lugha yetu, na kingereza kifundishwe kama lugha.
Unayo hoja ya msingi sana, swali la msing je
kiswahili hakina misamiati ya kutosha. Kuna baadhi ya sekta kama science na technology ukitafsiri jambo unajikuta huna msamiati wa kuweka unaacha lilivyo. In short kasi ya kukua kwa misamiati ya kiswahili inazidiwa mbali na kasi ya kukua kwa maarifa ya dunia ambayo mostly yanaandikwa kwa kiingereza. Kama nchi bado hatuna rasilimali/resources za ku-keep up na kutafsiri maarifa yoote ikiwemo vitabu.

Siku sheria za nchi wakianza kuandika kiswahili tutaanza kusogea ila kwa ulimwengu wa sasa hatutegemei waTZ wazaliwe wafe humu humu nchini. Mtu yoyote makini lazma kumaster kiingereza na lugha zingine kma kifaransa, kichina.
 
Hata usome kingereza miaka 70 ukiingia kitaa miaka miwili tu ushasahau

Huwezi kudumu na lugha ambayo haizungumzwi popote sio mtaani, msikitini, hospitalini wala popote pale. Kingereza kwa Tanzania ni kwa ajili ya kuangalizia movies na story za youtube basi
 
Back
Top Bottom