Tupeni mrejesho mliowekeza kwenye mashamba ya miti

unauza bei gan mche wa paina na milongoti
 
Muhimu sana ukatie bima. Mimi nilikuwa nimepanda heka 100. Miti ilikuwa na miaka 6. Na nilipanda miti ya malawi ya miaka 10 unavuna. Lakini mwaka jana mwezi wa 8 hapo shamba lote liliungua moto. Kuna wajinga walikuwa wanagombania shamba la urithi,mmojawao akaamua kulichoma hilo shamba,ambalo lilikuwa umbali kama wa mita 500 kutoka shambani kwangu. Mashamba mengi sana yaliungua. Wakati linaungua shamba langu nilikuwa kwenye proces ya kukatia bima. Lakini mwaka huu nafanya mpango nipande parachichi. Mwisho miti inalipa saaaaana. Lakini nakushauri kama ndio unataka kuanza kuwekeza huko kwenye miti. Panda parachichi mkuu. Miaka mi3 unaanza kuvuna. Na soko lipo kubwa sana,kuna kiwanda kimefunguliwa na rais juzi kati kiko Rungwe mbeya. Kuna kiwanda kinajengwa njombe. Kuna soko liko Italy. Panda parachichi mkuu
 
vp mkuu heka ya miti yenye miaka 2-3 huwa unauzaje/wanauzaje na mm mwaka huu nataka niingie huko
 
vp mkuu heka ya miti yenye miaka 2-3 huwa unauzaje/wanauzaje na mm mwaka huu nataka niingie huko
Mimi sio muuzaji wa miti chini ya miaka 15. Halafu bei sio uniform na wakati mwingine bei huwa inaathiriwa na shida za muuzaji hasa kwa miti midogo. Mapanda sasa hivi wanauza Tsh 1.5M mpaka 2.5M kwa eka kwa miti ya umri huo.
 
Mkuu Malila karibu sana, Hizi nondo zako hasa kwenye ujasiria mali ni rotuba tosha kichwani mwangu Sijui ndugu yako kanyagio alipoteaga wapi?
Mlachake bado uko Iringa mkuu?

Kanyagio bado tuko wote sana. Tulipofanya yetu Mufindi tukahamia Njombe pamoja. Bado tunakimbiza miti ya mbao. Baadae tukaenda wote Mkuranga kule. Sio muda mrefu atavuna kitu cha ukweli pande za Mufindi.
 
Kuna kitu wanaita fireline, yaani unaacha kama hatua kumi au ishirini kutoka kwa shamba la jirani
Mimi huwa naweka mpaka 40 meters, lakini moto wenye Kimbunga huwa unavuka.
 
Mkuu Malila karibu sana, Hizi nondo zako hasa kwenye ujasiria mali ni rotuba tosha kichwani mwangu Sijui ndugu yako kanyagio alipoteaga wapi?
Baada ya mabadiliko ya utawala, mambo mengi yalibadilika sana, watu wanatembea chinichini sana.
 
Mlachake bado uko Iringa mkuu?

Kanyagio bado tuko wote sana. Tulipofanya yetu Mufindi tukahamia Njombe pamoja. Bado tunakimbiza miti ya mbao. Baadae tukaenda wote Mkuranga kule. Sio muda mrefu atavuna kitu cha ukweli pande za Mufindi.
Safi sana man. Iringa nilihama tango 2012 nipo huku kwa wazaramo
 
Pines huwa nauza Tsh 80/ na mlingoti Tsh 100/
Uko njombe sehem gan
 
njia ya kwenda songea
Ule uliokula mpaka miti ya jimbo kuu la njombe ulilamba na yako pia? Mi shamba moja lilipona kimiujiza aisee. ule moto ndo uliishia kwenye shamba langu.
 
Kwa nini unalazimika kurudia neno changamoto mara nyingi hivyo mkuu ? Ungeandika tu 'zipo changamoto zifuatazo' halafu ukazitaja tu moja moja.
 
Kwa nini unalazimika kurudia neno changamoto mara nyingi hivyo mkuu ? Ungeandika tu 'zipo changamoto zifuatazo' halafu ukazitaja tu moja moja.
Nilikuwa nimepiga cha Makambako, nisamehe bure

🤣😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…