Tupeni mrejesho mliowekeza kwenye mashamba ya miti

njia ya kwenda songea
Ndio njia kwenda songea. Tunaingilia pale kuna kibao cha frank yule aliwatika miche ya parachichi pale barabarani na kule ndani karibu na magereza ana shamba kubwa la maparachichi,nafikiri tayari ana soko Italy
 
Mkuu Mwaka Gani Vile 🙂
 
Ushauri wangu Ni kuwaa wawekezeeni watoto wenu wenye miaka 1-15 wao wakifika miaka 36 watawakumbuka sana so msipande kwaajili yenu
 
Mi ni mmoja wa washawishi wa kilimo cha miti na parachichi.Changamoto niliokutana nayo ni MOTO.shamba langu la miaka 4liliungua moto mwaka jana, mashamba mengine yanaendelea vizuri.kuna gharama za kutengeneza njia za kuzuia moto kila mwaka.haipungui lak3 kwa heka 10.kila mwaka.
Nimegundua kwamba kama shamba lipo barabarani milingoti ni mizuri zaidi inavumilia moto kuliko paini.
 
Kweli mkuu, ila watu ni walalamishi tu.njombe ardhi bado ipo kubwa tu ni nguvu zako tu.Siku hizi wameingia wapemba na kusomba mikaa bado mtu umekaa unalalana hakuna ajira.
 
Melia azedaracht

Ni jamii ya muarobaini
 
Mimi nimewahi poteza eka 350 za miti ya mbao na nguzo kwa msimu mmoja yenye miaka mitano. Lakini msimu uliofuata nikaotesha zaidi ya hizo. Nilichofanya ni kutafuta sababu ya moto ule. Nilijua chanzo chake nikarekebisha na nina songa mbele.
Chanzo ilikuwa nini mkuu?
 
Inaumri gani hii miti?
 
Hizi bei za mashamba ulizoweka hapa ni za kununua shamba na kulimiliki kabisa au kukodisha tuu?
 
Ku prone, kuna watu wengi wanataka kuni mkuu, kwanini kwako iwe gharama

Kwanini utoe hela mfukoni, wakati unacho prone chenyewe ni mali
Pande za iringa, njombe kuni ni bwerereee, hata mabanzi wanajibebea bure. Mikoa mingine sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…