Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Dr. Mwaijande mzumbe Dcc ni balaaa, alinikamatia almost nusu ya class kny public policy huyu jamaa hafai hata kwa bure
 
wa ngaleku primary school huyu anaitwa malamsha ni chapombe mbaya kwa umarufu wake wa kipigo aliitwa 'sukuma dawati' sasa akitaka kukupa kipondo anakwambia ingiza kichwa kwenye dawati by then jiwe mgongoni sasa kinachofuata stiki mpaka unahisi huna makalio
 
mwalimu sapula. sawala primary
na baiskeli yake ya sasa mtanikoma unoko
 
Shule ya msingi mengeni kuna mwalimu alikuwa ana itwa kiwoli a.k.a komredi kipepe
 
Shule ya msingi mengeni kuna mwalimu alikuwa ana itwa kiwoli a.k.a komredi kipepe

Hahahahahahah.....eti Komredi Kipepe--huyu, bila shaka, alikuwa mtata kuliko maelezo!
 

Hahahahahaha!....huyu alikuwa DIKTETA si mchezo!
 

Hahahaha! Mkuu, inaonekana hata wewe ulikuwa mtundu balaa--hao walimu wanoko kwa kweli ulikuwa ukiwapa wakati mgumu sana. Kama vile nakuona jinsi ulivyokuwa ukichumbua hivyo visiki. Umenikumbusha mbali-- hata mimi wakati nikiwa Sekondari ya Nyansincha niliwahi kupewa adhabu ya kuchimba siki moja kubwa sana na mwalimu Elias Nyangi (alikuwa mwalimu wa Bible Knowledge).
 
Kinondoni Secondary School alikuwepo Mwalimu Shariff miaka hiyo. Sina hakika kama bado yupo. Huyu kama kungekuwa na mashindano ya unoko naona angenyakua kombe. Lakini pia JKT kulikuwa na maafande wanoko enzi hizo. Nakumbuka wakati nimepitia Mgulani JKT (831 JK) alikuwepo Meja Njogoro, ambaye alikuwa ni naibu kamanda wa kikosi (second in command au 2IC). Huyu alikuwa akikutana na wewe smart area lazima akutoe kasoro na kukupa adhabu ya kuruka kichura au kukata michongoma.
 
Kili boys second tulikuwa na ticha mmoja akiitwa kichefuchefu alikuwa mnoko sana.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 


Mama kitembe???,,
Bagabeach high school
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…