Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Mwalimu Mchwampaka alikuwa ana makengeza, alikuwa balaa akikukamata haujachomekea hata ukiwa Kariakoo. Kuna siku alinikamata natoroka kupitia geti dogo la Jangwani nilikula mbata, sitasahau hiyo siku.Mungu ailaze roho ya marehemu Mchwampaka mahali pema peponi.Amina

Du, yaelekea huyo ticha alikuwa mkuda kama jina lake lilivyo--jina bayaaaaa!!! Hahahahahaha!!!!
 
Zuberi Hamisi aka Zediii.....Mbomayi Kati Primary School. Alikua anachapa km vile anampiga punda!
 
Ifakara high school kuna mwalimu alikua anaitwa NGUVU TGT daaah yule baba alikua chapombe afu alikua anapiga,nakumbuka tulikua tukienda shamba tunakoma 206_2008

Afu kuna huyu MAMA KAINJA mmmh huyu.mama kiukweli alikua na roho ya paka,roho mbayaaa, mnoko,akiongea anasisitiza,alikua anaogopeka kama chatu

Chuo kuna lecturer alikua anaitwa SAULE,mmh yani huyu anapenda kukomoa kwa maswalianapenda kumfanya mtu aone shule ngumu jamani
 
Katika shule/chuo hakosekani mwalimu msumbufu na ambaye huwafuatilia sana wanafunzi hata ktk mambo madogo madogo na kuwapa adhabu za ajabu ajabu.

Leo nataka tuwakumbuke walimu hawa pamoja na kujikumbusha vituko walivyowahi kuvifanya.

Mimi shuleni kwetu Mara Sekondari kulikuwa na mwalimu mmoja aliyeitwa Jigge. Basi siku moja kuna wanafunzi walitoroka kwenda mjini bila ruhusa. Na kibaya zaidi, walipokuwa huko mjini wakafanya fujo na kuharibu mali za wananchi. Taarifa zao zikafika shuleni. Ilikuwa jioni na kiza kilikuwa kimeanza kukolea. Mwalimu Jigge akapiga kengere. Wanafunzi wote tuliokuwepo shuleni tukakusanyika bwaloni na akaanza kuchuka roll call.

Ili kumkomesha mwalimu huyu, pamoja na kuwanusuru wale wanafunzi 'wahalifu' waliokuwa wamefanya tukio mjini, wanafunzi wakapanga kuzima umeme main switch na kumpopoa kwa mawe. Ghafla tu, umeme ulipozimika, mwalimu alichomoka kama mshale na kutokomea kizani. Wanafunzi walimtupia mawe lakini, kwa ile speed aliyochomoka, hakuna jiwe lililompata. Ana bahati sana.

Hicho ndo wazazi wenu waliwatuma kufanya shule?
 
Adv. Old moshi kulikua na mwl. Machomeko
o.lvl. Forest hill kulikua na mwl. Manage
 
Mwalimu wangu wa somo la kingereza alikuwa anaitwa mwalimu Swiswi ni maremu sasa" alikuwa mnoko sana
 
daaah aisee kuna mwalimu alikua anaitwa mnelamwana(mtwara tech)uyu jamaa ni balaa,,alikuaanaogopeka na wanafunzi na walimu wote ispokua mama mkulemba tu,,aliamishwa wakt tuko form3 na kupelekwa shule fulan ambapo alimpiga mwanafunz mateke ya tumbo na kumsababishia kulazwa hosp.ya mkoa ligula na kisha muhimbili,,,kwa tukio hilo alikua antembea na ulinzi maana wanakijiji walikua wanamwandama

dah aisee mnela mwana alikuwa kiboko,nakumbuka form one yangu nilitega paredi la asubuhi,nimetulia zangu azimio cell c,nikawa nacheki darini nawaambia masela hapa nikimsikia mnela napanda palee,ila namaliza tu mnela yuko mlangoni,daah nilichimba visiki wiki nzima karibu na masandube kule
 
shule ya msingi mapambano mwalimu mnoko Masilingi.
shule ya sekondari Al haramain mwalimu mnoko Ustadh Abdallah
Nalog off
 
Back
Top Bottom