tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
- Thread starter
- #241
Kuna Mwalimu mmoja anaitwa RUBA alikuwepo Mara Sekondari miaka ya 90, huyu mwalimu ni mnoko hana mfano....halafu huwa hacheki na mtu yeyote, hata walimu wenzake. Siku moja nilidokoa maharage jikoni, kiraja akaniona akanichongea kwa RUBA. Siku ya Jumatatu wakati tukiwa assembly ground akaniita na kuanza kunichana mbele za wanafunzi mbele. Kisha alinipa adhabu ya kupanda majani kwenye korongo lililokuwa karibu na Physics laboratory. Basi akawa anaifuatilia kinoma...aliniambia nimwaguile maji zile nyasi hadi ziote...na kama mnavyojua ukame wa Musoma, nilikomaje! Sitamsahau mshenzy yule kamwe!