Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Kuna Mwalimu mmoja anaitwa RUBA alikuwepo Mara Sekondari miaka ya 90, huyu mwalimu ni mnoko hana mfano....halafu huwa hacheki na mtu yeyote, hata walimu wenzake. Siku moja nilidokoa maharage jikoni, kiraja akaniona akanichongea kwa RUBA. Siku ya Jumatatu wakati tukiwa assembly ground akaniita na kuanza kunichana mbele za wanafunzi mbele. Kisha alinipa adhabu ya kupanda majani kwenye korongo lililokuwa karibu na Physics laboratory. Basi akawa anaifuatilia kinoma...aliniambia nimwaguile maji zile nyasi hadi ziote...na kama mnavyojua ukame wa Musoma, nilikomaje! Sitamsahau mshenzy yule kamwe!
 
hii mkuu peleka jukwaa la jokes hapa tunataka tujadili mambo ya kutusaidia kielimu.unapotosha maana ya jukwaa.
 
Basi unaambiwa kwamba kuna mwalimu anaitwa Bachubila. Jina la utani tulikuwa tunamuita Ruba. Huyu ticha alikuwa hacheki na mtu yeyote yule. Tangu nianze fomu wani mpaka namaliza fomu foo sikuwahi kumuona akicheka. Usiombe ukutane na Ruba hujachomekea shati, hujahudhuria assembly au ukiwa umetoroka shule--utajuta kuzaliwa!

Kuna siku alinitaka niokote makombo ya chakula nimpelekee alishie kuku wake, nikamdis. Siku 1 alinivizia nikiwa natoka DH akanizaba konzi kidogo nizimie! Kisha alinipa adhabu ambayo niliifanya wiki nzima bila ku-attend class. Nilikomaje!

Sasa huyu bwana kiingereza chake kilikuwa na matege. Siku 1 kuna mwanafunzi wa fomu tuu alimpiga mwanafunzi wa fomu wani mbele yake, Ruba akadakia: 'WHY YOU BEAT FORM ONE IN MY FRONT?'. Hapa alikuwa na maana kwamba: 'KWANINI UNAMPIGA FOMU WANI MBELE YANGU?'. Bora hata alipokuwa hajui kiingereza, angekijua angekuwa mnoko zaidi. Kwa kweli mwalimu huyu alikuwa mtata sana, hakuna mwanafunzi shuleni kwetu Mara Sekondari asiyemfahamu huyu ticha mnoko.

Nilishauri thread iende jukwaa la utani lakini nimecheka sana.teh teh teh.
 
Kabobe sabasaba sec mtwara ni balaaa bora ukutane na nyati
 
zanaki mwl mwarike jamani mnokoooo na alikua anaongea kiingereza mnacheka hadi bas
 
Kuna mwakaringa a.k.a kibana wa kibasila enzi izo npo pale 2001-2004 usipochomekea shati lazima akubane,siku moja alipigwa getini unoko wote ukaisha

Mwakalinga ni bonge la Ticha. Mtakua marafiki na ukikosea anakubadilikia. Ana mawaidha... Binti hii tabia haikupendezi, haikupendezi kabisa.
Nilikuja kukutana nae wakati fulani alikua AICC Arusha kwenye Mkutano fulani akiwa Mkalimani wa Kifaransa.
 
Kuna Mwalimu alikuwa anaitwa HAYATI MAREHEMU MAITI SENGOVI! Dah ilikuwa ni noma alikuwa baraaaaa! Alifika shule kwa Mara ya kwanza akajitambulisha kuwa alikufa na akafufuka kijiji kizima kilitikisika hiyo ilikuwa miaka ya 1988/ alikuwa ni tishio jamani.
 
Back
Top Bottom