Aisee mimi utotoni, nilipachikwa jina la "Doctor Kizinja"! Niliitwa jina hilo mpaka umri wa shule nilpoandikishwa std I ndipo taratibu likaanza kufifia lakini kuna kina mama wa kitongoji nilikozaliwa mpaka leo nikikutana nao huniita jina hilo!
KISA CHA KUPACHIKWA JINA HILO
Ilikuwa kati ya umri wa miaka 4 hadi 5, Aisee niliugua nafkiri ilikuwa malaria au sulua, basi mama yangu alinipeleka hospitali kupatiwa matibabu. Huko hospitali alikuwepo Dr. akiitwa Doctor Kizinja, nilikua muoga wa sindano so alipotaka kunidunga sindano nilisumbua kidogo, basi akanichimba mkwara akisema wanijua mimi, mimi ni Doctor Kizinja, nitakuchapa fimbo! Basi nikatulia mtalaam huyo ambaye kwa sasa mstaafu akanidunga sindano aina ya KRISTA PENI, sindano hii kwa miaka ya nyuma kabla ya kupunguzwa nguvu ilikuwa inauma ni ajabu na imeshasababisha vilema kwa watu wengi sana! Ndugu yangu unaambiwa nililia njia nzima na toka siku hiyo mtu alikuwa akitaja jina la DR Kizinja, natimua mbio ndefu bila kugeuka nyuma mpaka ndani!