Tupia picha zinazoonesha uzuri wa nchi yetu ya πŸ‡ΉπŸ‡Ώ πŸ‡ΉπŸ‡Ώ πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Hahaaaaa, siku ya kwanza kupita hapo kidogo nife kwa pressure. Nilikaa seat ya nyuma kwenye Capricorn natokea Njombe. Yule Dereva Mwarabu akawa analitungua tu kushuka huo mlima hizo kona. Mpaka tunaumaliza huo mlima na hizo kona nipo Hoi.
Zile corners zinachukua urefu wa 27kms, kama siku hiyo ulikuwa na hofu basi naimani mpaka unafika chini ulikuwa hoi sanaπŸ˜„
 
Zile corners zinachukua urefu wa 27kms, kama siku hiyo ulikuwa na hofu basi naimani mpaka unafika chini ulikuwa hoi sanaπŸ˜„
We sikia tu kwa watu mkuu. Sasa nimezoea ila kuna siku nyingine nasafiri kwenye basi naenda Arusha kuna jamaa nadhani naye ilikuwa mara yake ya kwanza kupita ile njia. Alipiga "ukunga we derevaaaaaaa nenda taratibu utatuuaaaaaaaa" watu tukamshangaa. Jamaa alikuwa nyuma akaja mbele anahema na kutota Jason kweli. Tukamuuliza, nini shida. Anacheka tu.
 
Kwa mara ya kwanza kupita nilikuwa natokea Arusha kuja Iringa na private car na mwenzangu ndio alikuwa ana drive. Sikuwa na hofu bali nilienjoy ile view sana.
 
Mimi napata mashaka, kwa mikataba tuliyoingizwa huko uarabuni sijui kama tuna cha kujivunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…