Tupia picha zinazoonesha uzuri wa nchi yetu ya 🇹🇿 🇹🇿 🇹🇿

Tupia picha zinazoonesha uzuri wa nchi yetu ya 🇹🇿 🇹🇿 🇹🇿

images (5).jpeg
 
Nilikuwa nataka nianze kuuliza hivi uzuri wa hii nchi ni mapori tu na wanyama ndio nikaziona hizi 📸 🔥🔥🔥😄
Bro ila mapori, uasilia na mazingira nayo uzuri wa nchi yetu. Kuna siku nikiwa naishi Iringa, tulipokea wageni fulani toka Misri pale Nduli na kuwapeleka sehemu moja panaitwa Dabaga. Kule mahali pana Baridi sana na pana mashamba makubwa ya miti na parachichi. Sehemu ile ina greenish ya ajabu. Wale Waarabu wa Kimisri walichanganyikiwa kwa ukijani ule, mashamba ya miti ya mipine na uoto wa asili wa mito, maji maji pamoja na Ukungu. Jamaa wakawa wanapiga picha na kurekodi kila mahali. Walikuwa na furaha kwa kuona hali ile kwani kwao hakuna kitu kama hiko. Binafsi nilijifunza kuwa ushamba haupo kwenye manyumba, magari na maghorofa tu kumbe hata hali ya Mazingira nayo yanaweza kumfanya mtu awe mshamba na avutiwe nayo.
 
Back
Top Bottom