Tatizo liko wapi? TEC wameweka bayana kwanini hawaungi mkono mkataba.
Mlitaka wanyamaze tu kwani wanahudumia watu au hewa?
Kama walicho andika hakina maana si muwapuuze tu kama mnaweza?
Mahali popote pakiwa na ombwe kuna kitu kita kuja kujazia ombwe, upende usipende.
Serikali inaweza kuendelea kutekeleza kila kitu itakavyo, lakini wanaojielewa huwa hawasiti kueleza hofu zao. Na muda ni mwamuzi mzuri.
Msiwasakame TEC, hii siyo mara ya kwanza kutoa waraka. Mnasahau, ni kama vile huu ni waraka wa kwanza kutoa mtazamo tofauti na mamlaka.
Yatapita kama yalivyopita, ila ukweli hauchelewi kujidhihirisha.
TEC mkiona la kutafadhalisha msiache, maana tulio tarajia kufanya wajibu tulio wapa wamejipa jukumu la kupitisha mambo muhimu kwa mihemko.