Tusahau kuindoa CCM kupitia ballot box

Akili kubwa inaweza kufanya yote, hata kushika dola ila sio kujenga ofisi ikifika hapo inabidi tukasome historia...,
 
Akili kubwa inaweza kufanya yote, hata kushika dola ila sio kujenga ofisi ikifika hapo inabidi tukasome historia...,
Kwenye mazingira ya Afrika
Ushindane na chama dola
Uimarishe Chama
Ufungue matawi
Usimamishe wagombea na kuwasapoti financial
Kipate uungwaji mkono kwa kuuza sera

Dah? Mzee unadhani uchumi ni kwenda gym kujaza misuli ya kifua[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mpaka hapo huna akili kubwa. Acha kubwabwaja. Unajiita akili kubwa kwenye akili zako tu. Lakini kiuhalisia wewe ni mbumbumbu.
 
Ukweli mtupu...

Wajitambue sasa wanaCCM wakimege chama...sisi wananchi tuko nyuma yao...it is either now or NEVER...

We are tired ..
 
Ukweli mtupu...

Wajitambue sasa wanaCCM wakimege chama...sisi wananchi tuko nyuma yao...it is either now or NEVER...

We are tired ..
Unadhani wewe ukichoka ndio issue?
 
Na Mkuu
Nisichokipenda kingine kwa CCM ni hicho,
Bila mawazo mapya, watu wapya unadhani hiki chama kitaweza kutatua matatizo ya Watanganyika?

Kusema watu wale wale na vizazi vyao huoni wanatengeneza ufalme au kifupi Upper Class

..siasa zimebadilika sasa hivi.

..mawazo mapya yalitakiwa yatoke upinzani.

..Magufuli ameturudisha kwenye chama kimoja.
 
Mpaka hapo huna akili kubwa. Acha kubwabwaja. Unajiita akili kubwa kwenye akili zako tu. Lakini kiuhalisia wewe ni mbumbumbu.
Asante mkuu
Ila hata akili kubwa haifanya kazi katika vacuum.

Mpaka walipofikia unatakiwa uwape kongole ikiwa kweli unatambua ilivyo ngumu kufanya harakati hasa Tanganyika.

Huku wengine wakisapotiwa na vyombo vya dola pamoja na deep state.
 
..siasa zimebadilika sasa hivi.

..mawazo mapya yalitakiwa yatoke upinzani.

..Magufuli ameturudisha kwenye chama kimoja.
Upo sahihi sana
Tanganyika na Urundi zinafanana kila kitu
CNDD FDD na CCM vinarandana kabisa
 
Kweli akili kibwa haiwez kuwa na makao makuu yake kwa miaka 30 ila ikipewa nchi inaweza kuifanya dubai kwa miaka kumi
 
Matibabu +kula juu yako huku ukitumia “fake ID “
 
Asante mkuu
Ila hata akili kubwa haifanya kazi katika vacuum.

Mpaka walipofikia unatakiwa uwape kongole ikiwa kweli unatambua ilivyo ngumu kufanya harakati hasa Tanganyika.

Huku wengine wakisapotiwa na vyombo vya dola pamoja na deep state.
Basi kama unategemea huyo unayeshindana naye akupe nafasi ya kumshinda; huu utakuwa wendawazimu nambari moja.

Kwa hiyo Malengo na Madhumuni ya CCM yatakuwa yafuatayo:-
(1) Kushinda katika Uchaguzi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande mmoja na Zanzibar kwa upande wa pili

(2) Kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi yetu na raia wake.

(3) Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha.

(4) Kusimamia utekelezaji wa Siasa ya CCM pamoja na kuendeleza fikra za viongozi waasisi wa vyama vya TANU na ASP, kama zilivyofafanuliwa katika maandiko mbali mbali ya Vyama hivyo

(5) Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika Jamii hifadhi ya maisha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria.

(6) Kuona kwamba katika Nchi yetu kila mtu aliye na uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi; na kazi maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu riziki yake.

(7) Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.

NAKADHALIKA.........
 
Machafuko pekee ndio yataruhusu mwenye ridhaa ya umma kukaa madarakani.
2025 inafika, vijana chipukizi wa uvccm wamekuwa wakijiandaa kushika nafasi za kuongoza uma kuanzia nafasi za kata mpaka mikoa huku wewe ukijiandaa na machafuko mwaka wa 7 huu.
 
Wakati wa chama kimoja ilikuwa ni hiyari kuchangia ccm? Una umri gani mkuu? Au umeanza kuishi Tanzania juzi kati?
 
2025 inafika, vijana chipukizi wa uvccm wamekuwa wakijiandaa kushika nafasi za kuongoza uma kuanzia nafasi za kata mpaka mikoa huku wewe ukijiandaa na machafuko mwaka wa 7 huu.

Vijana wa CCM hawajiandai kushika madaraka kwa ushawishi wa kisiasa, bali kwa kujipendekeza kwa wateuzi huku wakisubiri mbeleko ya vyombo vya dola kutangazwa washindi kwa shuruti. Hiyo itafika mwisho kwa machafuko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…