Tusahau kuindoa CCM kupitia ballot box

Ukombozi wa kweli ni kwenda mbinguni. Duniani tupo na ukombozi wa kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi.
Usidhani kila mtu unae muona katika maisha yako ni muumini wa hizo imani, kulikuwa hakuna sababu ya msingi ya wewe kunielezea mimi maswala ya mbinguni wakati mimi hapa nazungumzia taifa, CCM na ukombozi.

Zingatia muktadha wa kila eneo ulipo.
 
Hata Afrika kusini ilipata uhuru 1930, lakini akina Mandela walipambana dhidi ya makaburu kutoka kwenye ubaguzi wa rangi.

Bila machafuko sioni chochote kubadilika. Hizi porojo za amani ili tuendelee kutawaliwa kwa shuruti ni kupoteza muda.
Machafuko peleka kwenu huko somalia. Sisi watanzania tunautaratibu wetu. CCM ni chama chenye nguvu barani Africa. Matatizo yenu ndani ya vyama vyenu msitafute mchawi.
 
Usidhani kila mtu unae muona katika maisha yako ni muumini wa hizo imani, kulikuwa hakuna sababu ya msingi ya wewe kunielezea mimi maswala ya mbinguni wakati mimi hapa nazungumzia taifa, CCM na ukombozi.

Zingatia muktadha wa kila eneo ulipo.
Sasa unataka ukombozi gani!?
KISIASA
KIUCHUMI
KIUTAMADUNI
 
Jitahidi kuzingatia ninayo andika ili usizalishe maswali yasiyo na maana.
Wewe unasema unataka ukombozi, nami nakuuliza unataka ukombozi gani!? Kama hujui ukombozi unaouhitaji utaweza kweli kutetea hoja zako!?
 
TANU ilikaa miaka mingapi chini ya utawala wa wakoloni!?

..ilianzishwa 1954 tukapata uhuru 1961. Kwa hiyo ni miaka 7.

..kinachonishangaza ni Muingereza kuwa na utu kuliko hawa Watanzania wenzetu wa Ccm.

..kwa mfano, kulifanyika uchaguzi mwaka 1958 na Muingereza hakuengua mgombea hata mmoja wa Tanu.

..Sasa fast forward mpaka uchaguzi wa 2019 na 2020 ambako Tume ya Uchaguzi chini ya Ccm iliengua maelfu ya wagombea wa upinzani.

..Je, ni lazima uwe Ccm li utendewe haki na uwe huru hapa Tanzania?

..Mazingira hayo ndio yanayonifanya nisionee fahari Uhuru na nchi yetu.
 
Mungu anasema atatupigania na atatushindia na sisi tutakaa kimya. Mungu siku akitaka kuwatoa atawafarakanisha na hata wenyewe baadae hawatoamini. It's a matter of time
 
Sasa tunarudi kwetu hapa. CHADEMA ilianzishwa 1992 mpaka leo 2022 ni miaka 30 hawana ofisi. Je, hizi ndizo siasa za kutaka kuongoza nchi!?
 
Machafuko peleka kwenu huko somalia. Sisi watanzania tunautaratibu wetu. CCM ni chama chenye nguvu barani Africa. Matatizo yenu ndani ya vyama vyenu msitafute mchawi.

CCM ni chama kikubwa, lakini kubwa jinga, na kiko hadi leo madarakani kwa uoga wa wananchi. Maana kama ni wizi wa kura wanaufanya waziwazi maana hawana uwezo tena wa kushinda uchaguzi. Hivyo tukiacha uoga CCM itazikwa kaburi moja na KANU ya Kenya. Machafuko tu ndio njia ya kurejesha heshima ya box la kura.
 
Wewe unasema unataka ukombozi, nami nakuuliza unataka ukombozi gani!? Kama hujui ukombozi unaouhitaji utaweza kweli kutetea hoja zako!?
Zingatia nilicho kuambia, kuwa unapaswa kuzingatia ninacho andika ili ujiepushe wewe kuuliza maswali yasiyo na maana.

Una kumbuka kuwa hilo swali uliniuliza mwanzo na nikalitolea jawabu lake.

Jitahidi kuweka umakini katika kila jambo maishani mwako na jiepushe na mihemko isiyo na maana, maana haina afya yoyote kwako.
 
KANU linganisha na TANU. Mizizi ya CCM ni mirefu. Shughulikieni matatizo yenu kabla ya kunyoshea vidole wengine.
 
Unaandika maneno mengi sana. Nimekuuliza swali unataka ukombozi gani!?
 
Kwahiyo lengo la kutaka katiba mpya ni kuitoa ccm madarakani? 😲
Mbona kazi mnayo basi,, hiyo katiba mtaandika peke yenu au?
 
KANU linganisha na TANU. Mizizi ya CCM ni mirefu. Shughulikieni matatizo yenu kabla ya kunyoshea vidole wengine.

Matatizo yetu ya wizi wa kura au? Nyie machafuko yakitokea mtanyoosha maelezo.
 
Matatizo yetu ya wizi wa kura au? Nyie machafuko yakitokea mtanyoosha maelezo.
Nimekuambia issue zenu za machafuko toka Somalia hapa hayafui dafu.
Ndio maana kuna vyombo vya dola kuzuia machafuko na watu wenye mawazo mabaya kama wewe.

Tafuta pesa kijana, achana na mawazo ya kishetani.
 
Unaandika maneno mengi sana. Nimekuuliza swali unataka ukombozi gani!?
Zingatia nilicho kujibu mwanzo kwa hili swali lako, huwa sipendi majibizano yasiyo na maana hiyo ndiyo desturi yangu.
 
Nimekuambia issue zenu za machafuko toka Somalia hapa hayafui dafu.
Ndio maana kuna vyombo vya dola kuzuia machafuko na watu wenye mawazo mabaya kama wewe.

Tafuta pesa kijana, achana na mawazo ya kishetani.

Huko Zimbabwe, Sudan nk watu walipoandamana hakukuwa na vyombo vya dola? Ngoja machafuko yatokee ndio ukatafute kazi ya halali na sio hii ya kujipendekeza kwa viongozi majizi ya kura ili upate mlo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…