Pre GE2025 Tusaidianeni. Kwanini wabunge wengi wamepata Bachelors na Masters kutoka Open University? Kuna siri gani kwenye hicho chuo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Na wewe kama unataka Masters bila ya kusomea nenda fasta Open University utaipata. Pesa yako tu.
 
Flexibility in time to do other things does not EASE the complexity of the study, and it might MAKE it worse. Some go for years beyond normal semester to complete their study. Do not mention that again.
 
Open University kwanza 90% wanaoenda kusoma huko ni watu wanaofanya kazi na wanasomea vitu ambavyo viko related na kazi zao, anasoma kitu anacho practice kila siku kwahiyo ni nguvu sana kutoka ukiwa Empty unatoka ukiwa na uelewa mkubwa zaidi.

Tofauti na yule anaesoma full time yuko chuo anajaza theories kichwan ambazo hajawahi ku practice hata siku moja, akienda field lazima aanze kufundishwa mambo upya maana kajaza theory kichwani tu, hakuna ambae anasoma open University na hajui anasoma kwa malengo gani, au ataitumia vipi hiyo elimu, wengi wanaosoma ni wafanyakazi na wanasomea wanachofanya.
 
Flexibility in time to do other things does not EASE the complexity of the study, and it might MAKE it worse. Some go for years beyond normal semester to complete their study. Do not mention that again.
Nice but Faq
 
Umesahau UDOM, ni hela zako tu, wanafanyiwa mitihani, research.... and the likes, Chuo ni UDSM, hivyo vingine ni High School zilizochagamka
 
Kwa wote walioshindwa kujiunga na vyuo vingine. Neno huria, kupata degree huria. Huenda mzee Kihiyo nae alisoma chuo huria.
 
Umesahau UDOM, ni hela zako tu, wanafanyiwa mitihani, research.... and the likes, Chuo ni UDSM, hivyo vingine ni High School zilizochagamka
Hta UDSM ni sawa tu vyuo vingine! Elimu ya Tanzania haitofautiani. Tumewafnyia interview watoto wengi tu vyuo tofauti tofauti hakuna tofauti! wanaojiongeza wanafanya vizuri siku hizi elimu inaptikana kirahisi sana ni juhudi za mtu wala siyo chuo
 
Mbona wengine hujaweka mwaka waliosoma isipokuwa Bashungwa?
Funny enough hata Lukuvi naye!?
 
Daaah niona Musukuma nae eti kavaa kofia ya round naona kinyaa!
 
Sababu kwanini wabunge wengi au viongozi wa umma wanapata degree za Bachelor’s na Master’s kutoka Open University (kama Open University of Tanzania – OUT) mara nyingi inahusiana na mfumo wa masomo wa chuo hicho na namna unavyowiana na ratiba zao zenye shughuli nyingi. Hapa kuna baadhi ya sababu kuu:


  1. Flexibility ya Masomo:
    Open University inatoa mfumo wa Open and Distance Learning (ODL) ambapo wanafunzi hawalazimiki kuhudhuria darasani kila siku. Wabunge na viongozi wengi wanakuwa na ratiba ngumu, hivyo mfumo huu unawapa nafasi ya kusoma wakati wao wa ziada bila kuathiri majukumu yao ya kikazi.
  2. Kujipangia Ratiba:
    OUT inaruhusu wanafunzi kujipangia ratiba zao za kusoma na kufanya mitihani. Hii inawapa nafasi wabunge kusoma bila kuacha kazi zao. Wanaweza kusoma nyakati za usiku, mwishoni mwa wiki, au likizo.
  3. Upatikanaji wa Programu Mbalimbali:
    OUT inatoa program nyingi za shahada, uzamili, na hata uzamivu. Wabunge wengi wanatumia nafasi hii kuchagua kozi zinazowiana na kazi zao za uongozi na maendeleo ya jamii, kama Public Administration, Political Science, na Law.
  4. Urahisi wa Ada na Gharama Nafuu:
    Ada za OUT ni nafuu ukilinganisha na vyuo vingine vikuu vya ndani na nje ya nchi. Hii inawavutia watu wengi, hata wale wenye kipato cha kati.
  5. Kufanikisha Malengo ya Kisiasa na Kitaaluma:
    Wabunge na viongozi wengi wanahitaji shahada ili kuongeza sifa zao kielimu, hasa kwa nafasi za kisiasa na uongozi. OUT inawapa nafasi ya kufanikisha hilo bila kuhitaji kuacha nafasi zao za kazi.
  6. Mfumo wa Kujitegemea:
    Wanafunzi wa OUT wanategemea sana self-study kwa kutumia vitabu, majarida, na nyenzo za kidijitali. Hii inaendana vizuri na watu waliopo kazini ambao tayari wana uzoefu wa kujitegemea katika kujifunza na kupanga majukumu yao.
  7. Mitihani na Vituo Nchi Nzima:
    OUT ina vituo vya mitihani na huduma karibu kila mkoa, hivyo wanafunzi hawalazimiki kusafiri umbali mrefu kuhudhuria vipindi au mitihani. Hii ni faida kubwa kwa wabunge wanaohitaji kuwa karibu na majimbo yao.

Kwa hiyo, hakuna “siri” bali ni urahisi na unyumbufu wa mfumo wa OUT unaowasaidia wale wenye majukumu mengi kufanikisha malengo yao ya kitaaluma bila kuacha kazi zao.

© Jackson94
 
Hta UDSM ni sawa tu vyuo vingine! Elimu ya Tanzania haitofautiani. Tumewafnyia interview watoto wengi tu vyuo tofauti tofauti hakuna tofauti! wanaojiongeza wanafanya vizuri siku hizi elimu inaptikana kirahisi sana ni juhudi za mtu wala siyo chuo
Vyuo vina interview ya nini?
 
Una matope kichwani. Shida nini? Ingekuwa hizo degree wanapata toka secondary ambayo haina ithibati ya kutoa hiyo bachelor ndio ulalamike. Ok let say wote hizo bachelor wangezipata udcm au udom so what? Kenge wewe.
Mweleweshe usimutukane
  • OUT ni chuo sawa na vyuo vingine;
  • OUT ni chuo chenye ithibati;
  • Course zake ni zingativu sawa na vyuo vingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…