Pre GE2025 Tusaidianeni. Kwanini wabunge wengi wamepata Bachelors na Masters kutoka Open University? Kuna siri gani kwenye hicho chuo?

Pre GE2025 Tusaidianeni. Kwanini wabunge wengi wamepata Bachelors na Masters kutoka Open University? Kuna siri gani kwenye hicho chuo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Na wewe kama unataka Masters bila ya kusomea nenda fasta Open University utaipata. Pesa yako tu.
 
Unajua msuli yatima wewe?
Unajua kusoma na majukumu?

Flexibility in time to do other things does not easy the complexity of the study, and it might makes it worse. Some the go for years beyond normal semester to complete their study. Do not mention that again.
Flexibility in time to do other things does not EASE the complexity of the study, and it might MAKE it worse. Some go for years beyond normal semester to complete their study. Do not mention that again.
 
Hapa watu wanamtolea mapovu tu mleta mada lakini kiuhalisia open watu wananunua matokeo/vyeti sana tu na uwezekano wa kutoka empty kabisa kichwani ni mkubwa mno, usicheze na msuli yatima. Si kubovu kwa 100% na Kuna products nzuri tu zinazotoka huko zile zinazojitambua, lakini ni sehemu inayotoa fursa kirahisi kwa wahuni kununua matokeo/vyeti zaidi ukilinganisha na vyuo vingine.

Nina mifano ya wadau wangu kadhaa.

Mfano mmojawapo ni ticha mmoja mdingi ni mtu wa mitungi sana 24/7 kalewa chakari na hana time ya kutulia home, yaani hata asipokunywa yeye yupo tungi alishalewa jumla.

Sasa huyo dingi wakati naanza kumfahamu kumbe alikuwa anachukua bachelor ya education, alikuwa first year. Ajabu hakuwa na PC, simu janja wala njia yoyote ya kupata materials za kujisomea wala huo muda wa kujisomea asingeweza kuwa nao. Hata kufanya mitihani kwa jinsi alivyokuwa sidhani kama alikuwa akienda.

Mzee kala mitungi weeee miaka 3 imeisha analeta cheti ni mabanda matupu na B+ za kuhesabu, ana first class! Tuliposhangaa mzee akasema siwezi kujitesa wala kufeli open university wakati nina hela. Mzee kaendelea na mitungi kapata ajali kaumia kichwani sasa ni kama chizi.
Open University kwanza 90% wanaoenda kusoma huko ni watu wanaofanya kazi na wanasomea vitu ambavyo viko related na kazi zao, anasoma kitu anacho practice kila siku kwahiyo ni nguvu sana kutoka ukiwa Empty unatoka ukiwa na uelewa mkubwa zaidi.

Tofauti na yule anaesoma full time yuko chuo anajaza theories kichwan ambazo hajawahi ku practice hata siku moja, akienda field lazima aanze kufundishwa mambo upya maana kajaza theory kichwani tu, hakuna ambae anasoma open University na hajui anasoma kwa malengo gani, au ataitumia vipi hiyo elimu, wengi wanaosoma ni wafanyakazi na wanasomea wanachofanya.
 
Flexibility in time to do other things does not EASE the complexity of the study, and it might MAKE it worse. Some go for years beyond normal semester to complete their study. Do not mention that again.
Nice but Faq
 
Wakuu,

Nilikuwa napitia pitia CV za wabunge hapa wakuu.

Hawa ndio wabunge, ambao wana degrees na masters kutokea kwenye hicho chuo cha Open University:

  • Assenga Abubakar Damian – Mbunge wa Kilombero – Bachelor of Arts in Political Science
  • Innocent Bashungwa – Mbunge wa Karagwe – Masters of International Affairs (2016-2020)
  • Oscar Ishengoma Kikoyo – Mbunge wa Muleba Kusini – PhD, Open University
  • Ndaisaba Ruhoro – Mbunge wa Ngara – Masters in Project Management
  • Flaurent Laurent Kyombo – Mbunge wa Nkenge – MBA, Open University
  • Geofrey Mizengo Pinda – Mbunge wa Kavuu – Bachelor's Degree
  • Sebastian Simon Kapufi – Mbunge wa Mpanda – Bachelor's in Law
  • William Lukuvi – Mbunge wa Ismani – Masters in Political Science
  • Davidi Kihenzile – Mbunge wa Mufindi Kusini – LLB
  • Joseph Mkundi – Mbunge wa Ukerewe – MBA

Hawa ni wachache tu, naamini kuna wengi ambao wamesoma kwenye hicho chuo.

Swali langu ni kwanini wabunge wengi wamepata degrees na masters kwenye hicho chuo?

Ndio kusema kwamba hiki chuo kina hadhi kuliko UDSM au kupata degree hapo ni rahisi?
Umesahau UDOM, ni hela zako tu, wanafanyiwa mitihani, research.... and the likes, Chuo ni UDSM, hivyo vingine ni High School zilizochagamka
 
Kwa wote walioshindwa kujiunga na vyuo vingine. Neno huria, kupata degree huria. Huenda mzee Kihiyo nae alisoma chuo huria.
 
Umesahau UDOM, ni hela zako tu, wanafanyiwa mitihani, research.... and the likes, Chuo ni UDSM, hivyo vingine ni High School zilizochagamka
Hta UDSM ni sawa tu vyuo vingine! Elimu ya Tanzania haitofautiani. Tumewafnyia interview watoto wengi tu vyuo tofauti tofauti hakuna tofauti! wanaojiongeza wanafanya vizuri siku hizi elimu inaptikana kirahisi sana ni juhudi za mtu wala siyo chuo
 
Wakuu,

Nilikuwa napitia pitia CV za wabunge hapa wakuu.

Hawa ndio wabunge, ambao wana degrees na masters kutokea kwenye hicho chuo cha Open University:

  • Assenga Abubakar Damian – Mbunge wa Kilombero – Bachelor of Arts in Political Science
  • Innocent Bashungwa – Mbunge wa Karagwe – Masters of International Affairs (2016-2020)
  • Oscar Ishengoma Kikoyo – Mbunge wa Muleba Kusini – PhD, Open University
  • Ndaisaba Ruhoro – Mbunge wa Ngara – Masters in Project Management
  • Flaurent Laurent Kyombo – Mbunge wa Nkenge – MBA, Open University
  • Geofrey Mizengo Pinda – Mbunge wa Kavuu – Bachelor's Degree
  • Sebastian Simon Kapufi – Mbunge wa Mpanda – Bachelor's in Law
  • William Lukuvi – Mbunge wa Ismani – Masters in Political Science
  • Davidi Kihenzile – Mbunge wa Mufindi Kusini – LLB
  • Joseph Mkundi – Mbunge wa Ukerewe – MBA

Hawa ni wachache tu, naamini kuna wengi ambao wamesoma kwenye hicho chuo.

Swali langu ni kwanini wabunge wengi wamepata degrees na masters kwenye hicho chuo?

Ndio kusema kwamba hiki chuo kina hadhi kuliko UDSM au kupata degree hapo ni rahisi?
Daaah niona Musukuma nae eti kavaa kofia ya round naona kinyaa!
 
Sababu kwanini wabunge wengi au viongozi wa umma wanapata degree za Bachelor’s na Master’s kutoka Open University (kama Open University of Tanzania – OUT) mara nyingi inahusiana na mfumo wa masomo wa chuo hicho na namna unavyowiana na ratiba zao zenye shughuli nyingi. Hapa kuna baadhi ya sababu kuu:

  1. Flexibility ya Masomo:
    Open University inatoa mfumo wa Open and Distance Learning (ODL) ambapo wanafunzi hawalazimiki kuhudhuria darasani kila siku. Wabunge na viongozi wengi wanakuwa na ratiba ngumu, hivyo mfumo huu unawapa nafasi ya kusoma wakati wao wa ziada bila kuathiri majukumu yao ya kikazi.
  2. Kujipangia Ratiba:
    OUT inaruhusu wanafunzi kujipangia ratiba zao za kusoma na kufanya mitihani. Hii inawapa nafasi wabunge kusoma bila kuacha kazi zao. Wanaweza kusoma nyakati za usiku, mwishoni mwa wiki, au likizo.
  3. Upatikanaji wa Programu Mbalimbali:
    OUT inatoa program nyingi za shahada, uzamili, na hata uzamivu. Wabunge wengi wanatumia nafasi hii kuchagua kozi zinazowiana na kazi zao za uongozi na maendeleo ya jamii, kama Public Administration, Political Science, na Law.
  4. Urahisi wa Ada na Gharama Nafuu:
    Ada za OUT ni nafuu ukilinganisha na vyuo vingine vikuu vya ndani na nje ya nchi. Hii inawavutia watu wengi, hata wale wenye kipato cha kati.
  5. Kufanikisha Malengo ya Kisiasa na Kitaaluma:
    Wabunge na viongozi wengi wanahitaji shahada ili kuongeza sifa zao kielimu, hasa kwa nafasi za kisiasa na uongozi. OUT inawapa nafasi ya kufanikisha hilo bila kuhitaji kuacha nafasi zao za kazi.
  6. Mfumo wa Kujitegemea:
    Wanafunzi wa OUT wanategemea sana self-study kwa kutumia vitabu, majarida, na nyenzo za kidijitali. Hii inaendana vizuri na watu waliopo kazini ambao tayari wana uzoefu wa kujitegemea katika kujifunza na kupanga majukumu yao.
  7. Mitihani na Vituo Nchi Nzima:
    OUT ina vituo vya mitihani na huduma karibu kila mkoa, hivyo wanafunzi hawalazimiki kusafiri umbali mrefu kuhudhuria vipindi au mitihani. Hii ni faida kubwa kwa wabunge wanaohitaji kuwa karibu na majimbo yao.

Kwa hiyo, hakuna “siri” bali ni urahisi na unyumbufu wa mfumo wa OUT unaowasaidia wale wenye majukumu mengi kufanikisha malengo yao ya kitaaluma bila kuacha kazi zao.

© Jackson94
 
Hta UDSM ni sawa tu vyuo vingine! Elimu ya Tanzania haitofautiani. Tumewafnyia interview watoto wengi tu vyuo tofauti tofauti hakuna tofauti! wanaojiongeza wanafanya vizuri siku hizi elimu inaptikana kirahisi sana ni juhudi za mtu wala siyo chuo
Vyuo vina interview ya nini?
 
Una matope kichwani. Shida nini? Ingekuwa hizo degree wanapata toka secondary ambayo haina ithibati ya kutoa hiyo bachelor ndio ulalamike. Ok let say wote hizo bachelor wangezipata udcm au udom so what? Kenge wewe.
Mweleweshe usimutukane
  • OUT ni chuo sawa na vyuo vingine;
  • OUT ni chuo chenye ithibati;
  • Course zake ni zingativu sawa na vyuo vingine
 
Back
Top Bottom